Nadhani hujaelewa hili somo, kwa nini tumefikia hpa tulipo na tumefikia hapa tulipo leo na sio huko nyuma. Nataka nikueleze jambo moja very serious, ujue kuna mengi sana nyuma ya pazia. Makubwa ni matatu;
- Zanzibar kuna potential kubwa ya mafuta, na yakipatikana Zanzibar itakuwa kama Kuwait; kimapato, ukitumia GDP, the richest country in the world. Tangu ijulikane kuwa Zanzibar ina uwezekano mkubwa wa kuwa na mafuta, suala la nishati (mafuta na gesi) kuwa katika muungamo likawa ni kero ya muungano kwa upande wa Zanzibar, jambo la kuondolewa
- Zanzibar ni kisiwa cha kimkakati (strategic island) kiuchumi. Kuna mataifa kama Oman, UAR, Saudi Arabia nk, wako tayari kuingia makubaliano nao ili kiwe katika himaya zao na kuwaahidi Zanzibar mabilioni ya dola, kwamba wakikubali wataishi kama wako peoponi tayari na hakutakuwa na Mzaznibar masikini au asiye na nyumba ya kifahari, matibabu bire kwa wote, na kila mkazi atajengewa nyumba ya kisasa nk. Zanzibar hawawezi kuingia makubaliano kama hayo wakiwa sehemu ya Tanzania, na wakilazimisha basi itabidi JWTZ wachukulie ni uvamizi.
- Zanzibar ni kisiwa cha kimkakati (strategic island) kijeshi. Kuna mataifa kama USA, China, Russia nk, wako tayari kuingia makubaliano nao ili kiwe kituo chao cha kijeshi, na kuwaahidi Zanzibar mabilioni ya dola. Tanzania (bara) hawako tayari kuruhusu hili, kwa gharama yeyote ya kulinda muungano, hata kama ni kuwalea huku wanakukojolea kila siku.
Kwa hiyo basi, hizo ndio sababu za msingi zinafanya Zanzibar waone muungano kwa sasa unawazuia kuingia peponi, kulingana na ahadi wanazopewa kama wakiuvunja. Wanafanya kila njia ili kuwakera Tanzania bara kwa visababu vingi vidogovidogo lakini haya ndio mambo yaliyoko nyuma ya pazia.
Hawatasema sababu za kutaka kuvunja muungano, na haya mengine unayosikia ni kelele tu. Na aliethubutu kujaribu hili la kuiondoa Zanzibar katika muungano alikuwa ni Aboud Jumbe, ndio maana akaishia kutengwa kama mtu mwenye ukoma. In fact, ilitakiwa afungwe kwa uhaini. Aliyevujisha taarifa za kile Aboud Jumbe alitaka kufanya alikuwa ni Maalim Seif Sharif, hadi akazawadiwa Uwaziri Kiongozi. Lakini waliambiwa wazi, mtu mwingine yeyote akithubutu, JWTZ itaingia, na wakumbuke hatutahitaji kuweka boots on the ground in Zanzibar wakifanya uasi. Tunaweza kuwapiga tukiwa Bagamoyo.
Sasa, theory nyingine ya kutisha iliyopo ni kwamba hata Raisi Samia huenda anatumika kama kichocheo cha kuvunja muungano, akitumia nafasi yake kuwaudhi watu wa bara ili wafikie hatua kusema hawataki tena muungano. Watu wana theorize kwamba anafanya makusudi kuingia mikataba kama ya bandari, kuleta Wa-Zanzibar waajiriwe bara nk, kwa lengo la kuchochea hasira upande wa bara, hasira ambayo mwisho wake ni kuvunja muungano.
Angalia kwamba theory ya Raisi Samia kutumika kama kichocheo cha kuvunja muungano inakuwa na logic fulani kwa jinsi alivyong'ang'ania mkataba wa bandari. Ilikuwa ni kama ugomvi wa watu wa bara na Samia, na hakujali kuendelea kuwaudhi watu, hata viongozi wa dini, na wazee wa busara, kwa sababu hilo ndio lilikuwa lengo; wakasirike, waseme sasa muungano basi. Katika hali ya kawaida ya siasa, zile kelele zilipaswa kumfanya aseme basi tunaacha tumewasikia wananchi. Lakini akakaza uzi tu, japo upinzani wa juu sana aliokabiliana nao. Theory ni kwamba kulikuwa na sababu ya yeye kushika ule msimamo, na hiyo sababu haikuwa ya kiuchumi.
Na kuna vitu vingine vingi vinavyohusu kuwafungulia waarabu fursa upande wa bara, pamoja na mambo ya mbuga za wanyama nk. Haya yote yalionekana kuwa ni strategy, kwamba hata kama muungano utavunjika, uwepo wa hawa waarabu upande wa bara, waarabu wanaoonwa kuwa wajomba wa Samia na watu wa Zanzibar, kutakuwa na manufaa kwa Zanzibar. Na hata kuna watu wanasema haya mambo yanafanyika kwa coordination ya Zanzibar na Uarabuni.
Kuna mengi sana nyuma ya pazia. Suala ni kwamba, ni thory tu au yana ukweli ndani yake? Nilitaka kupost hili jambo kama thread inayojitegemea, lakini wewe sasa ndio umefanya niliseme. Haya ni baadhi ya mambo Nyerere alijua, na akawa na msimamo muungano usivunjwe kwa gharama yeyote ile. Hofu yake ilikuwa ni ya kuisalama. Lakini suala la Samia kuwa Raisi wa Tanzania limepeleka hili jambo katika level nyingine kabisa.