Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Upo sahihi..zile hofu za Waarabu na Ukomunisti hazipo tena!
Ni kweli Watsnganyika haturudhiki tena na jinsi Mambo yanavoenda! Ila Kuna watu wanajifanya hawaoni! Tunstaka Katiba ya Warioba!
 
Hoja hapa si kubaguana nadhani tuna exaggerate hili nyumba,gari na hata binadamu hufanyiwa ukarabati jinsi muda unavyokwenda ili kuviboresha na kuongezea uhai,jana leo na kesho ni vitu tofauti.Kupitia upya mifumo ie muungano kwa mahitaji ya sasa siyo kuupinga na kuleta ubaguzi tuache spinning.Tunaoshupaza shingo kuupitia upya ndiyo wavunja muungano kwa unafiki. wakemewe
 
Hakuna madhara yeyote, ni wazi Zanzibar hawataki huu muungano, tuwape kanchi kao walipe bill zao wenyewe, na wakitaka wamrudishe sultani sawa tuu, na wakitaka wajitangaze kabisa Islamic state under Sharia law, waende tuu na hata madeni tutawasamehe, huu sio muungano, kalikuwa kaproject ka mwalimu na Karume na fantasy zao za vita baridi za mabeberu na ukomunist
 
madhara yatakuwa makubwa kwa raia? raia gani? tueleweshe, serikali tatu Tanganyika watapata madhara gani, na zanzibar watapata madhara gani.
Serikali 3 zitasababisha hali ya changu ni changu pande zote kama Zanzibar wanavyofanya sasa hivi.
Matokeo yake, mfano tu, raia wa Zanzibar anayemiliki ardhi Tanganyika atanyang'anywa vinginevyo Zanzibar wakubali watanganyika kununua ardhi kwao.
Kwa ujumla kutakuwa na mtafaruku utakaosababisha watu kupoteza mali na hata muungano wenyewe kuvunjika.
Zanzibar watashindwa kuchangia serikali ya muungano (kipato chao kidogo), wafanyakazi waliopo bara kwa jina la serikali ya muungano watarudishwa kwao, wabunge wa kutoka Zanzibar watakosa fursa walizo nazo sasa na mengine mengi.
Raia wa Tanganyika waliopo Zanzibar watafukuzwa pia kwa sababu ya chuki ya kisiasa itakayojengeka.
 
Duh!, hakuna any provisions popote za kuuvunja muungano, huko kuuvunja kutaanzia wapi?.
Siku hizi tunahangaika sana na muungano huu.
Baada ya kukusoma juu ya hilo la kutokuwepo na 'provisions' za kuuvunja muungano; bila kujali niliyokwishajibu kuhusu jambo hilo, nimepata mfano sahihi wa kuunga hilo wazo la 'provisions'.

China ya Beijing (hivi hii ilitokatokaje kuwa Peking) na Hong Kong. Huo ndio mfano sahihi unaoendana na Tanganyika yetu na Zanzibar. Achana na habari za Zanzibar ilikuwa nchi huru kabla ya muungano.
Ile pwani iliyowahi kudaiwa na Sultan kuwa sehemu ya Zanzibar, ni sababu tosha ya Zanzibar kuwa 'an integral part of Tanganyika. Yeyote anayetafuta kuiondoa Zanzibar atakuwa anachezea usalama wa Tanganyika.
 
Mkuu, hatuhitaji kumtupia lawama mtu yeyote kwa sababu

Katiba hii hii mbovu, imetumika miaka mingi sasa na ilionekana ipo sawia kabisa kwa nyakati hizo ila kwa sasa haifai tena, naamini, hata ikiandikwa mpya leo, bado huko mbeleni haitaifaa tena kizazi kijacho kutokana na namna ya kizazi hiko

Na hata sasa, muungano wetu leo, unaonekana na matobo ni kutokana na majira na nyakati kupita, kwa kizazi tulichopo, ni vyema usukwe upya tena
 
Kwa kweli sijasoma ilikuwaje, wavunja miungano ni mabeberu, kama Japan na Taiwan, ni Mabeberu wa Marekani. China na Hong Kong ni mabeberu wa UK!.
Kwa vile zile Articles za Union, sio mkataba, ni agreement tuu, huko nyuma, niliwahi kuzifuatilia hadi UN, sikuziona!, Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu?!. (Ufuatiliaji Muungano Sehemu ya I) na Je, wajua kuwa kuna uwezekano Tanzania sio nchi halali Kisheria (De Jure) Bali ni De Factor?!
P.
 
Kama serikali tatu haifai basi serikali moja, kama tunaupenda muungano kweli

Hakuna workable formula. Muunganio hauwezekaniki. Milioni 62 kwa milioni 1 unusu, the math ain't mathing.

Serikali moja maana yake Zanzibar ni mkoa. Zanzibar ishasema toka 1964, haitaki kuwa mkoa.

Serikali mbili ndo hizi, Muungano umeshikiliwa kwa mtutu wa bunduki. Nyerere na Dr. Shein walidhani wakimfunga Maalim Seif na kum house arrest Aboud Jumbe na kuwa shuti Mashehe wa Uamsho na kutishia kuwafukuza chamani G55 basi tatizo limekwisha, Hola! Hoja ya ubovu wa muungano bado inaita!

Serikali tatu ni gharama za kinyonyaji na kijinga, Tanganyika hatuwezi kukubali. Tukishakuwa na serikali ya Tanganyika ya kuendesha mambo yetu hiyo ya Zanzibar tunaihitaji ya nini ???? Kwa nini tubebe mzigo, Zanzibar wana nini cha mno cha kuungana nao ????? Ma stress ya serikali tatu ya nini ?????????

HAKUNA jawabu la Muungano. Hasara tupu. Sio kila Muungano una faida. UK walijitoa EU. Tuvunje Muungano, for heavens sake!
 
Jinsi walivyowengi huku bara siku kikinuka sidhani kama watapata pa kukaa huko visiwani.

Wanazaliana kwa wingi mno halafu Ardhi ya kuwatosha hawana.

Ardhi wanayoitegemea ni ya Tanganyika na bado wanaleta kiburi.
 
Raisi wa Tanganyika katoka Zanzibar lakini mtanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar, mambo ya ajabu kabisa
 
Serikali 3 ni kurudi nyuma na madhara yatakuwa makubwa kwa raia. Bora kwenda mbele kwenye serikali moja.
Madhara ya erikali moja ni baadhi ya wanasiasa kukosa vyeo na madaraka.
Umeeleza kitu kidogo sana mkuu unamaanisha serikali moja itasababisha viongozi kukosa vyeo?? Kaa chini fikiria upya.
 
Umeeleza kitu kidogo sana mkuu unamaanisha serikali moja itasababisha viongozi kukosa vyeo?? Kaa chini fikiria upya.
Ndiyo,
Hawatakuwepo Rais wa Zanzibar, makamu wa kwanza na wa pili, mawaziri wa Zanzibar, baraza la mawaziri la Tanzania nafasi zitagawanywa pande zote za muungano, wakuu wa taasisi zisizo za muungano watapungua baada ya kuunganishwa, ......
 
Ndiyo,
Hawatakuwepo Rais wa Zanzibar, makamu wa kwanza na wa pili, mawaziri wa Zanzibar, baraza la mawaziri la Tanzania nafasi zitagawanywa pande zote za muungano, wakuu wa taasisi zisizo za muungano watapungua baada ya kuunganishwa, ......
Hivyo ni vitu vidogo sana. Kikubwa zaidi nadhani kipo kwa wananchi.
 
Ndiyo,
Hawatakuwepo Rais wa Zanzibar, makamu wa kwanza na wa pili, mawaziri wa Zanzibar, baraza la mawaziri la Tanzania nafasi zitagawanywa pande zote za muungano, wakuu wa taasisi zisizo za muungano watapungua baada ya kuunganishwa, ......
Na kwenye uchaguzi watu wa bara hawatawapigia kura watu waliotokea Zanzibar maana Ubaguzi unaonekana dhahir hivi sasa !!

Kwahiyo siioni Zanzibar ikikubali kupoteza Utaifa wake. !

Waswahili Wanasemaga Akumulikaye mchana Usiku atakuchoma !
 
Wabara tulikuwa kama tunapuuza fulani hivi ila wazenji wenyewe tangu Zamani wanapambanis upande wao na wana umoja bila kujali itikadi,sasa huku bara kuna kama kufumbuliwa macho hivi,sasa huku bara wakiendelea hivi, wazenji watalia sana.

NB: WAZENJI WABAGUZI SANA LAZIMA TWENDE NAO JINO KWA JINO
 
Ubaguzi huo !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…