Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Zanzibar chao ni chao chetu ni chao pia
Naumbea muungano uvunjike hata leo leo
 
huu ubaguzi mbona unaongelewa humu tu JF,huko znz hakuna tatizo kabisa, wazanzibar,wamasai na wasukuma wanaishi vizuri tu bila shida yeyote. tena wote wanakula urojo. Hizi habari za ubaguzi wamebaki nazo watanganyika tu. sijui nu ukosefu wa kazi, mapenzi ya kulalamika au ni husda. Au siasa iliyo pitiliza?
 
Subiri muanze kuchinjana sasa😁 ndio mtajua kuwa ni compound au mixture
 
siku hizi hawaitwi wanyamwezi, wanaitwa wasukuma.
Wasukuma wamehamia miaka ya karibuni, na kwa upande mmoja wao wenyewe wanajitambilisha hivyo na wanapenda watambuliwe hivyo. Ila kiuhalisia watu kutoka Bara hutambuliwa kama ni Wanyamwezi...
 
Binafsi naamini kuwa muungano hautafika 2050
 
Na Lissu nae?
 
Msikie huyu.
 
Hebu hili andiko lako litoe hapa liwe mada inayojitegemea. Lipe kichwa cha "Muungano wa Tanzania ni Strategic, ni mwendawazimu tu ndiye amaweza kuuvunja"

Hongera Synthesizer, huko nyuma nimekurupuka "kukudogosha", I am sorry
 
Bora iwe hivyo mkuu, ili kusudi kila mtu afe na chake. Pengine tutapata maendeleo kama nchi zingine zilizosimama zenyewe. Zanzibar wana kiburi cha kitoto sana ni kama mtoto anaebebwa na wazazi kupewa kila kitu ili atulie ila haridhiki. Anatafta mabalaa tu.
 
Ukiona shamba linauzwa kaombe kununua ndipo urudi kutuambia hakuna ubaguzi. Au omba kazi serikalini au private sector huko Zanzibar. Na ukisikia mtu anaitwa jina kama chogo huko Zanzibar uliza nini maana ya chogo, na kwa nini chogo.
 
1. Raia wa Tanganyika walioko zanzibar watafukuzwa: ni wachache sana ndugu, ukiwaona jua wanafanya kazi kwenye mashirika ya kimataira/NGO, mahoteli na biashara kubwa, na wanachukiwa sana, hawapendwi, hivyo madhara hayatakuwa makubwa kwanza watarudi nyumbani kwao.

2. kwa wazanzibar, watatakiwa kurudisha ardhi ama la wapitie TIC wamiliki kama wawekezaji. itafaa kama wakinyang'anywa ili tuwe sawa, haiwezekani wao wamiliki kwetu ila sisi marufuku kumiliki kwao. wataamua wauze au wagawe watajua wenyewe.

3. wabunge kutoka zanzibar watakosa fursa walizo nazo bara za kupata perdiem na mamishahara rundo, wanajulikana mbona wamejenga majumba mengi tu DSM na Dodoma, watatapika zote hizo. ili warudi kwao wakaendelee kutuita chogo.

4. wafanyakazi wazanzibar waliopo bara itabidi warudi kwao wakajenge nchi yao, ajira zao wanapaswa waajiriwe watanganyika. haiwezekani wao waajiriwe hapa ila sisi marufuku kuajiriwa kwao.

5. kwenye changu ni changu na chako ni chako, ipo hadi sasa, wanzanzibar wanasema chochote walicho nacho ni chao, ila cha kwetu sisi ni chetu. ni kama mwanamke vile, anavyovitafuta ni vya kwake ila unachokitafuta wewe mwanaume ni cha wote.

wengi wanafikiri tunaandika hivi kwasababu ya chuki, no, hii ni kero mojawapo ya muungano ambayo watanganyika watatamani itatuliwe, na wazanzibar waeleweshwe kwamba kubaki kwenye muungano kama udungu inawafaidisha zaidi wao, na watanganyika wanafaidika tu kuwa tunaungana nao kama ndugu zetu ila sio kama watu tunaofaidika nao. wanatakiwa waruhusu aidha, cha kwao kiwe cha kwetu and vise versa, au la kila mtu achukue hamsini zake na tujuane kama mataifa mawili huru.

Pia, onyo kwao, siku zote mwanamke huwa anapiga sana yowe kuomba talaka kama wao walivyotuchukia na kutuona hatuna maana, sisi machogo, ila akitoka huwa anatamani kurudi ila ndio mwengine keshabadili. siku wakitoka kwenye muungano watakapokosa fursa zote hizi ndio watajua kumbe Watanganyika walikuwa na roho nzuri tu na waliwapenda tu.
 
Bro Umezungumza kama dikteta hujatoa suluhisho nini kifanyike kutatua KERO ambazo ndio msingi wa hoja za muungano na mara nyini wanasiasa zaidi ni maslahi sio ufumbuzi wa kudumu kwa nini iwe chako chetu na chetu chetu?
 
hata ukiachiwa ununue utaweza bei ya ardhi huko? au unafikiri bei ni kama za mkuranga?
Mfano mmoja ulio hai ni kwamba bei ya nyumba moja iliyopo pale msimbazi K.koo ni sawa na kununua mtaa mzima Mkuranga. πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Haya ndiyo tunatakiwa kutatua kwa akili ili raia wasipate shida kwa sababu ya siasa.
Changamoto zote husababishwa na maamuzi ya wanasiasa.
 
Muungano una CHANGAMOTO kubwaaa...Katiba Mpya ILIYO BORA ndio SULUHU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…