Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Kwani huu muungano ukifa shida ipo wapi? Kwanini tulazimishane kuungana wakati muungano umegeuka KERO badala ya neema? Sijawahi kuona muungano wa kiquma kama huu tangu nizaliwe.
 
kwan kati ya mmasai wa tz na mmasai wa kenya vs mmakonde yupi ndugu zaid ? ccmu inajaa wajinga siku hz

hoja za Lissu zipo wazi kwann mtanganyika hanaonekana raia daraj la pili kule zenji ?

ukute wewe ni mtanganyika ila ccmu wamekujaza ujinga
 
kwa anayofanya Sa100 , tuvunje tu muungano
 
sorry umeandika pumba mkuu

kwahiyo unauza nchi ya Tz ili kuizuia Zenj isipige hatua ? je mapato yao huwa mnaletewa huku bara ?

fanya research achana na hizo story za vijiweni
 
ila Lumumba imejaza watu wajinga sana , mbona uliyoyaandika hayajibu maswali ya Lissu , siku tukiungana EAC kila raia atakuwa huru kwenda nchi jiran kumiliki lolote pia uhuru wa kuabudu kitu ambacho watanganyika wanakidai kwa Zanzibar

kwann mzenji anamiliki ardhi huku ila sisi hatuwez kwenda kumiliki ardhi kule kwao ?

kwann mzenji anaeza kuwa kiongoz huku bara hata uenyekiti wa kijiji ila si mtanganyika kuwa kiongoz kule zenji ?

kwann wao wana uhuru wa kuabudu huku bara ila sisi wakristo hatuna uhuru wa kufungua sehem za kuabudu kule zenj ?

Zenji ni eneo la kuongeza kura kwa ccmu kipind cha uchaguz

UKIWA MJINGA UNAKUWA MTAJI WA CCMU
 
ni bora tuvunje muungano kuliko kuendelea kuwapa ccmu pa kujazia kura za uchaguz kwa kodi zetu zinazoenda wapet peti wazenji
 
Ubaguzi huo !
kunizuia mimi mtz mwenzio kumiliki ardhi huko kwenu huo sio ubaguz ila mimi kukutaka urudi kwenu nami nimiliki ardhi yangu huu ndo ubaguz si ndio ?

JINO KWA JINO MPK AKILI ZIWAKAE
 
Bro Umezungumza kama dikteta hujatoa suluhisho nini kifanyike kutatua KERO ambazo ndio msingi wa hoja za muungano na mara nyini wanasiasa zaidi ni maslahi sio ufumbuzi wa kudumu kwa nini iwe chako chetu na chetu chetu?
kweny huu muungano kipele ni Zanzibar , maana hawapo kwenye muungano ila ccmu ya Tanganyika inalazimisha huu muungano sababu ni kichaka chao cha kura kipindi cha uchaguzi
 
Hivi kwanini huu muungano usizamwishwe baharini na hawa wala UROJO warudi kwao na vibwengwe vyao!
Halafu tumewachoka Saaaaaaaaaaaaana!
 
Watu wa bara ndio watu gani!? Sema waTanganyika na waZanzibar
 
Pascal acha kuhadaa watu kwa mifano isiyo na ulinganifu. Hayo ya kuchanganya udongo ni mbwembwe za fikra kiimani ktk siasa kama zilivyo kauli mbinu ktk kuendea jambo fulani kisiasa.

Wapo watu waliounganisha undugu wa hiari kwa kuchanja damu na kuzichanganya ktk miili yao lakini bado undugu ulivunjika na maisha yaliendelea kama ilivyo ktk ndoa wanavyoapa kuwa kitu kimoja lakini bado inavunjika.

pascal acha kupotosha ukweli usemwe na kujadiliwa ili maauzi sahihi yafanyike kwa kuwa na tija ya kitaifa lakini pia kuepusha uhasama utakaokuja kutokea.
 
Watanzania tuko 61 Million na ardhi yetu ina 945,000 Sqaure kilometres za ukubwa.

Zanzibar wako 1.2 Million na ukubwa wa 2,460 Square kilometres.

Ni aibu leo watu 61 Million kuanza kugombea ki-ardhi kidogo namna hiyo wakati huku kumejaa mapori makubwa ya kutisha.

Hizo fursa za kazi unazozitaka ZNZ ziko wapi? Kama elimu yako na uwezo wako hauwezi kukupatia ajira hapa Bara penye uchumi wa GDP ya USD 85 Billion ndiyo ukabamane na GDP ya ZNZ ambayo USD 3.75??

Tunahitaji kubadilisha mtazamo tu. Tatizo letu kubwa ni umaskini. Zanzibar ingekuwa tajiri kama Qatar, mengi ya yanayosemwa wala isingekuwa issue. Kama sikosei, Area Commissioners from Zanzibar au positions nyingine zimepewa Watu wa upande mwingine wa Mwungano toka enzi za Mwalimu.

Na hizi feelings zikipewa nafasi, zinaweza hata kuleta issues kati ya movements za watu mikoani. Kuna watu, suddenly, watadai wakuu wa mikoa, wilaya, watoke katika mkoa huo huo.

Mikoa kama ya Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha ina mchango mkubwa kiuchumi kuliko mikoa mingine kama Tabora, Singida, Kigoma, Mtwara. What if hao wenye uchumi mkubwa wakaona wanannyonywa au kutawaliwa na watu wa mikoa maskini?
 
Ndugu nahisi kama hoja za changamoto za Muungano huu haujazopitia vizuri na kung'amua chanzo chake.

Hoja za kudai ardhi, nafasi za uongozi na fursa kadhaa zinazungumzwa na watu wa bara kwa kuwa wananchi wa wanzanzibar na viongozi wao tena wakiwemo wa ccm wanapaza sauti ya kudai wawe na mamlaka kamili, lakini pia wakidai kuwa Tanzania bara inainyonya zanzibar, rejea hata jinsi Rais wa Zanzibar alivyowahi kuivimbia serikali ya Muungano juu ya deni la umeme. Kwa ufupi wanzanzibar wamechoka na Muungano huu na tunavyoendelea kulazimisha ndivyo wanavyotaka na makubwa zaidi. Ndiyo maana sasa ifike kikomo kuwe mjadala huru juu ya namna bora ya kuwa na Muungano huu ama turejed ktk kuchakata katiba mpya au mazungumzo makhushu na ya kina juu ya Muungano yafanyike
 
Bado hivyo vitu ni peanut sana kuliko strategic position tuliyonayo. Kuwaacha ZNZ wawe available kwa mshirika mwingine kama Alshabab ni risk kwa nchi yetu.

Hizo gharama za umeme sijui na mgawo wa fedha inazopewa ZNZ ndizo opportunity cost ya Muungano.

Duniani kote hakuna watu wanaopenda Muungano iwe Russia, USA au Sudan.

Leo ZNZ ikijitoa na tukaiacha, itakuja mikoa yenye uchumi mkubwa kama Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro na Arusha. Watadai wananyonywa na mikoa ya Singida, Lindi na Mtwara hivyo wanadai kujitenga.

Watakuja Kagera watakuambia wao ni watu wa Uganda wanataka warudi kule kwa kuwa Nyerere aliwaleta kwa lazima.

Hizi hoja hazina mashiko zaidi ya kuwapa umaarufu wanasiasa.

Nimezaliwa miaka 4 kabla ya Muungano na sasa ni mstaafu, sioni faida yeyote tutakayoipata tukiwa bila ZNZ.

Na hao ZNZ wasijifanganye kuwa watapiga hatua kuwa kama DUBAI eti kwa sababu ni kisiwa. Mbona Comoros, Seychelles na Mauritius bado haziko kama Dubai au Qatar.

Kwenye geopolitics sehemu ambayo iko strategic kupata biashara ni Eritrea na Djibouti.

Ni nani apeleke meli zake Zanzibar Port na aache kuleta Dar Port ambako kuna ndiko kuna mizigo inapaswa kufika nankutawanyika kwenda nchi 8 zinazotuzunguka?
 
N
 
Hizi hisia ni za zamani sana kwamba Zanzibar ikiachwa itaangukia kwa alshababi. Tukubali kuwa Dunia imesonga mbele na siyo kama zamani. Umetoa mfano mzuri kuwa vipo visiwa vya usheli na comoro ambvyo vipo jirani na vipo salama kwamba havina hao maadui je woga huo kwetu unatoka wapi. Lakini pia ujue hauwezi endelea kukaa na mtu asiyekutaka ukadhani utamtawala milele siku ya kutoka ni vita kama Urusi na ukraine je ndivyo unataka itokee

Ama kuleta hii mifano ya mikoa yenye uchumi kujitenga bado unatembelea kivuli cha Nyerere ambacho kwa wakati ule ilikuwa sahihi lakini pia uelewe Zanzibar tayari ni nchi iliyo na Rais, tamaduni, na mambo mengi ya ki mamlaka kama nchi, hivyo mfano huo hauwezi kuwa halisi kwa mikoa ya bara kujitenga.
 
kunizuia mimi mtz mwenzio kumiliki ardhi huko kwenu huo sio ubaguz ila mimi kukutaka urudi kwenu nami nimiliki ardhi yangu huu ndo ubaguz si ndio ?

JINO KWA JINO MPK AKILI ZIWAKAE
Duh 🙄 !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…