BIG OKIngekuwa muungano tuliutaka sisi ndiyo ungesema yote hayo. Huu muungano ni wa Uingereza na Mmarekani. Kama wao hawautaki utavunjika siku moja tu.
Tumewachiwa dudu la "divide and rule" sisi kwa ujinga wetu tunaona tuna muungano.
Ukomunisti/ujamaa na uwazi ni vitu ambavyo ni maadui wakubwa.Na hatuelezwi ni kero zipi zimetatuliwa na zimetatuliwaje - isije kuwa zimetatuliwa kwa gharama ya Tanganyika! Uwazi ni muhimu sana
Muungano uvunjwe harakaWazanzibari walipodai Zanzibar yao, hakuna madhara makuwa yaliyojitokeza labda tu kule kuchafuka kwa hali ya kisiasa; leo waTanganyika wakidai Tanganyika yao eti kutatokea madhara makubwa!
Ninachoona ni kuwa Watanganyika walikuwa wamelala sasa wanaamshwa kudai Tanganyika yao, wapewe kama Wazanzibari walivyopewa Zanzibar yao.
Utasikia Mzanzobari anasema 'tunajitambua' na Katiba yao inawatambua kuwa wao ni Wazanzibari lakini Watanganyika hawajajitambua na Katiba haimyambui Mtanganyika bali inamchanganya na Mzanzibari kuwa wote ni Watanzania- Shida iko hapo.
Sasa Wazanzibari wanasema wamemezwa na Tanganyika, na Watanganyika wanasema wamemezwa na Tanzania maana yaye wote hawaridhiki na hali ilivyo - wote wasikilizwe ili muafaka mpya upatikane.
Muungano uvunjweHizi hisia ni za zamani sana kwamba Zanzibar ikiachwa itaangukia kwa alshababi. Tukubali kuwa Dunia imesonga mbele na siyo kama zamani. Umetoa mfano mzuri kuwa vipo visiwa vya usheli na comoro ambvyo vipo jirani na vipo salama kwamba havina hao maadui je woga huo kwetu unatoka wapi. Lakini pia ujue hauwezi endelea kukaa na mtu asiyekutaka ukadhani utamtawala milele siku ya kutoka ni vita kama Urusi na ukraine je ndivyo unataka itokee
Ama kuleta hii mifano ya mikoa yenye uchumi kujitenga bado unatembelea kivuli cha Nyerere ambacho kwa wakati ule ilikuwa sahihi lakini pia uelewe Zanzibar tayari ni nchi iliyo na Rais, tamaduni, na mambo mengi ya ki mamlaka kama nchi, hivyo mfano huo hauwezi kuwa halisi kwa mikoa ya bara kujitenga.
Mapinduzi ya kijeshi kwa Tanzania ni ngumu kidogo ila ntaungana na wewe kwenye mabaadiliko ya kimazingira, utashi na uelewa wa wananchi.Kwa hapa tulipofikia ccm lazima wajue kizazi kimebadilika, na yenyewe sio sehemu ya kizazi hiki. Ni vyema wakaruhusu rasimu ya Warioba itengeneze katiba yenye maoni halisi ya wananchi, na sio katiba ya kuifanya ccm isalie madarakani. Kinyume na hapo machafuko ama mapinduzi ya kijeshi lazima yatatokea hapa nchini Ili kupata mabadiliko ya kweli.
Hatuko mbali sana na huko.Mapinduzi ya kijeshi kwa Tanzania ni ngumu kidogo ila ntaungana na wewe kwenye mabaadiliko ya kimazingira, utashi na uelewa wa wananchi.
Kuhusu machafuko HAPANA bado kwa aina ya jamii ya kitanzania hatujafikia huko.
Kupinga ni haki yako ya uhuru wa maoni, na sio kukubali tuu kila kitu kitutusa!, ila msingi wa mijadala humu ni kwa hoja, jibu hoja kwa hoja au pangua hoja kwa hoja mbadala.Hapana kwa mara ya kwanza nakupinga
Kunahitaka sana elimu ya uraia kuhusu huu Muungano wetu, ni muungano adimu na adhimu.Hujui au umejisahaulisha kuwa katika Muungano wetu kimekufa kimoja tu, kingine kikabaki; katika hali hiyo hoja yako ya chemical reaction to form a compound si sahihi. Kwa mantiki hayo hayo basi hii ni mixture.
Naamini unajua Nyerere alifanya nini kuhusu hoja ya G55!.G55 Nyerere hakuwepo?
Kwa hiyo unataka tuendelee kuwa chini ya fikra za marehemu hata kama tutachinjana?Naamini unajua Nyerere alifanya nini kuhusu hoja ya G55!.
P