Wazanzibari walipodai Zanzibar yao, hakuna madhara makuwa yaliyojitokeza labda tu kule kuchafuka kwa hali ya kisiasa; leo waTanganyika wakidai Tanganyika yao eti kutatokea madhara makubwa!
Ninachoona ni kuwa Watanganyika walikuwa wamelala sasa wanaamshwa kudai Tanganyika yao, wapewe kama Wazanzibari walivyopewa Zanzibar yao.
Utasikia Mzanzobari anasema 'tunajitambua' na Katiba yao inawatambua kuwa wao ni Wazanzibari lakini Watanganyika hawajajitambua na Katiba haimyambui Mtanganyika bali inamchanganya na Mzanzibari kuwa wote ni Watanzania- Shida iko hapo.
Sasa Wazanzibari wanasema wamemezwa na Tanganyika, na Watanganyika wanasema wamemezwa na Tanzania maana yaye wote hawaridhiki na hali ilivyo - wote wasikilizwe ili muafaka mpya upatikane.