Uhayawani wa binadamu: haya mauaji ni wivu, visasi au malipizi? Je, inaweza kuwa ushirikina?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Huyu ndiye Dada Jonais (Mzaliwa wa Mwika Kilimanjaro) aliyekutwa ameuwawa msituni huko Korogwe, na pembeni ni mtoto wake ambaye pia alichomwa moto kwenye tukio hilo hilo. Kwenye kadhia hiyo pia binti wake wa kazi nae aliuwawa, naarifiwa anazikwa Tanga leo pia.

Huku Kilimanjaro pia walikuwa na msiba wa baba yao mdogo alikuwa azikwe jana ila baada ya taarifa za kifo cha huyo dada wamesitisha zoezi hili. Tetesi zinasema (Huenda walichukuliwa kinguvu nyumbani kwao na kupelekwa kwenye msitu na kufanyiwa unyama huo) Kiufupi maumivu ya familia hii hayaelezeki. Mungu awatie nguvu.

 
Sababu hasa ya haya ni nini? Maana naona tunapewa yaliyojili, na hatujui kwanini yamekuwa hivyo.
 
Okay.

Kuna maswali mengi Sana kuhusu suala hili.
1. Alikuwa anajishughulisha na kazi gani hasa?
2. Aliolewa? 3. Baba wa mtoto wake yuko wapi? 4. Hali yake ya mahusiano yake ipoje?
5. Je, ni kweli kwamba baba wa mtoto wake anayejulikana na jamii ndiye baba mzazi halisi wa mtoto wake aliyekuwa naye? Or there was a problem/conflict of paternity fraud between them???????
Suala hili la Paternity Fraudulent activity linapaswa kuangaziwa kwa kina zaidi kwenye Mikasa ya mauaji kama hii kwa sababu wanawake wengi Sana siku hizi wanapenda kuwabambikizia wanaume watoto wasiokuwa wao kiuhalisia.
 
😓😭inaumiza kuamini wasioaminika...I wish kama tungepata ujasiri kama wananchi tukafanya mapinduzi ya kweli...so sad to see these young souls perishing in vain and no backups or non tó fight to their back for their innocence...Yani ningeitukana serikali kuwa ni ya "kijinga na kipumbavu" lakini huo uwezo Sina, binafsi Sina Imani na serikali yangu.
 
Je waliyofanya hili tukio watapatikana?
Hapa ni polisi wenyewe kufanya uchunguzi tu lakini kama watafanya uchunguzi

Ova
 

Ulichoongea ni kweli kabisa
 
Mume aulizwe sana
Kabla ya maiti za huyo mama na mwanae hazijazikwa, ni vyema Sana Jeshi la Polisi wakatoa AMRI kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwenda kuchukua sampuli za vinasaba vya kupima DNA kutoka kwa hizi maiti Mbili. Maiti zisizikwe kabla ya kuchukuliwa kwa sampuli za kupima DNA, sambamba na kuchukua sampuli za vinasaba vya DNA kutoka kwa huyo Mwanaume ambaye anahusika na ubaba (partenity) wa huyo mtoto aliyeuawa pamoja na mama yake.
Hili ni suala muhimu sana la kuzingatiwa ili kuondoa mashaka yote kwamba vifo vya Watu hawa vimetokana na Mgogoro wa masuala ya Partenity Fraud, pia itasaidia kumfanya huyo mwanaume aishi maisha yake kwa Uhuru baada ya msiba huu kupita.
 
Picha ya mfanyakazi haipo!, Wao hawajafiwa??



Spiritually, Kuna la kusemwa ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…