UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Kwa wakulima wa mazao ya chakula katika wilaya ya Geita, mkoani Geita kuvuna si mwisho wa safari ya kupata kipato. Baada ya miezi kadhaa ya maandalizi, kupanda na kusubiri mavuno, hatua inayofuata ya kuhifadhi mazao ndiyo huamua kama jasho lao litageuka kuwa fedha au kupotea bila faida.
Baadhi yao changamoto huanza baada ya mazao kutoka shambani. Ukosefu wa maeneo maalumu ya kuhifadhi, matumizi ya mifuko isiyofaa na uelewa mdogo kuhusu teknolojia bora za uhifadhi husababisha sehemu ya mazao kuharibika kabla hayajafika sokoni au kutumika kama chakula cha familia.
Fortunatusi Zakayo, mkulima wa mahindi, mpunga, maharage na pamba kutoka kijiji cha Rwamugasa, anasema changamoto hiyo ya uhifadhi wa mazao imekuwa sehemu ya maisha ya wakulima wengi wa Geita, hasa maeneo ya vijijini.
“Huwa tunakumbana na changamoto, hasa upande wa mahindi, mahindi namna ya utunzaji unakuwa na shida sana kwa sababu uvunaji wake unakuwa ni kazi, namna ya kutunza,” anaeleza Fortunatusi.
Kauli yake inaakisi hali inayowakabili maelfu ya wakulima wadogo nchini Tanzania, ambapo jasho la miezi kadhaa mashambani hupotea katika kipindi kifupi tu baada ya mavuno.
Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), takribani asilimia 30 ya mazao ya chakula katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara hupotea baada ya mavuno kutokana na uhifadhi duni, huku hapa nchini Tanzania, Wizara ya Kilimo inaeleza kuwa upotevu wa mazao ya nafaka baada ya mavuno unafikia kati ya asilimia 30 hadi 40, hali inayopunguza kipato cha wakulima na kuathiri usalama wa chakula.
Katika wilaya ya Geita, ambako kilimo ndicho uti wa mgongo wa uchumi wa kaya nyingi, athari za upotevu huo zinaonekana moja kwa moja, licha ya kifungu cha 3.12 cha Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 kinachozungumzia usalama wa chakula na lishe, kikisisitiza wazi jukumu la serikali kuimarisha na kupanua miundombinu ya uhifadhi wa chakula, ili kuongeza uthabiti wa upatikanaji wa chakula, bado wakulima wanahifadhi mazao yao katika maghala yasiyo na viwango, mifuko ya kawaida au vyumba vya nyumba, jambo linaloongeza uwezekano wa mazao kushambuliwa na wadudu waharibifu, unyevu pamoja na panya.
Kwa Fortunatusi, hasara sio kupungua kwa chakula pekee yake, bali pia kushuka kwa thamani ya mazao sokoni.
“Upotevu, kwa mfano unapovuna namna ya kuyaweka yanaharibika, unajikuta ungevuna mahindi ambayo yana ubora, lakini sasa unakuja kukuta bei ndogo kwa sababu yanakuwa yameharibika, yamebunguliwa, yameoza wakati wa mvua, kama ulikuwa unategemea gunia ungeliuza kwa shilingi 90,000 unaliza kwa shilingi 60,000 kutokana na kupungua ubora,” masikitiko ya Fortunatusi kushuka ubora na bei ya mazao iliyochangiwa na uhifadhi mbovu.
Tofauti ya shilingi 30,000 kwa gunia moja inaweza kuonekana ndogo kwa mtu ambaye hajawahi kujishughulisha na kilimo, lakini kwa mkulima anayevuna magunia kadhaa kwa msimu, hasara hiyo hujikusanya na kuathiri uwezo wa kulipia ada za watoto, kununua pembejeo za msimu unaofuata au hata kukidhi mahitaji ya msingi ya familia.
Katika baadhi ya maeneo ya Geita, wakulima wameanza kuachana na mbinu za zamani za kuhifadhi mazao na kuhamia matumizi ya mifuko maalumu ya kinga njaa. Hata hivyo, si wote waliofanikiwa kufanya mabadiliko hayo.
Kajina Kaisanga, mkulima wa mahindi kutoka Nyambugu, Manispaa ya Geita, ni miongoni mwa waliobadili mfumo wa uhifadhi wa mazao yao baada ya kupata elimu ya uhifadhi bora wa mazao ya chakula.
“Mimi mazao yangu ninapoweka, huwa nayatoa shambani, nikiyavuna, nayaanika, natunza, naweka kwenye mifuko ya kinga njaa,” anasema Kajina.
Kajina amebainisha kuwa hatua hiyo ya kutumia mifuko ya kinga njaa imewasaidia kupunguza uharibifu wa mazao ukilinganisha na mbinu walizokuwa wakitumia zamani.
“Hizo njia za zamani ambazo tulikuwa tunatumia dawa, kwa sasa hivi huwa tunawatembelea wakulima, tunawashauri wanaweka kwenye kinga njaa,” anaeleza Kajina.
Boniface Kaswahili, Diwani wa Kata ya Shiloleli katika Manispaa ya Geita, anaonya kuwa upotevu wa mazao unaweza kuchangia kuendelea kwa changamoto ya njaa.
“Kwa hiyo wanaathirika vibaya, ndiyo maana unaweza ukakuta kwamba njaa haziishi,” anasema Boniface.
Marcel Magayane, ambaye ni mkulima mwezeshaji kutoka kijiji cha Nyambogo anaunga mkono hoja ya kwamba baadhi ya wakulima, hasa maeneo ya vijijini wapo kwenye hati hati ya kukabiliwa na njaa kutokana na uhifadhi mbovu.
“Athari moja ni upatikanaji wa mazao machache shambani na utunzaji wa mazao nyumbani… Maana yake kama mkulima amelima ekari moja, akapata gunia tatu, hiyo ni njaa tayari, ametunza mazao yake, yanabunguliwa, mahindi yaliyo mazuri ni kidogo, yaliyo mengi yatakuwa yamebunguliwa na wadudu, kwa hiyo ni njaa ya kutosha kabisa.”
Marcel anaeleza kuwa hapo awali katika kijiji anachoishi, wakulima walikuwa wakihifadhi mazao katika mifuko ya kawaida, hali iliyowaweka katika hatari ya kupoteza sehemu kubwa ya mavuno yao.
“Zamani tulikuwa tuna changamoto ya kubunguliwa mazao yetu, yaani namna ya uhifadhi ilikuwa sio nzuri, tulikuwa tunahifadhi katika mifuko ya kawaida," anaeleza Marcel.
Akisema changamoto hiyo katika kijiji cha Nyambogo imepungua baada ya wakulima kupata mafunzo kuhusu matumizi ya mifuko ya kinga njaa, ambayo husaidia kulinda mazao dhidi ya wadudu na kupunguza utegemezi wa kemikali katika uhifadhi.
Gharos Riwa, ambaye ni mdau katika sekta ya kilimo kutoka Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Geita anazungumzia athari za uhifadhi mbovu wa mazao ya chakula katika jicho la kibiashara.
“Tumekuwa tukiona athari kubwa inayotokea, hasa katika mazao haya ya kibiashara, yamekuwa yakileta madhara yakileta milipuko ya moto, lakini vilevile pia mazao kama mahindi kupunguza ubora kuwa na sumu kuvu. Na yote haya yanasabisha pengine hata sokoni ubora sokoni kutokuwa na ushindani wa kutosha,” anasema Gharos.
Gharos anaeleza kuwa mkulima asiyehifadhi vizuri ghalani hupata hasara kutokana na kupungua kwa ujazo unaosababishwa na mashambulizi ya wadudu waharibifu na changamoto nyingine.
Kwa upande wake mkulima Fortunatusi anasema kabla ya kupata mafunzo kuhusu mbinu bora za uhifadhi, alikuwa akitumia dawa za kuhifadhia mahindi kama ilivyozoeleka kwa wakulima wengi, baadaye alibadili mfumo huo baada ya kupata elimu.
“Zamani nilikuwa nahifadhi kwa kutumia sumu hizi mahindi, lakini baadae tulipofundisha na kampuni ya kilimo hifadhi, ndipo tukaona kwamba utunzaji wa kuweka sumu ni hatari, baadae nikawa naweka kwenye mifuko ya kinga njaa,” anazungumza Fortunatusi.
Matekere Mafuru, Afisa Kilimo wa Kata ya Shiloleli katika Manispaa ya Geita, mkoani Geita, anataja mahindi, maharage, kunde, udaga pamoja na mtama kuwa miongoni mwa mazao yanayohitaji uhifadhi makini.
“Mazao ambayo kwa kweli yasipohifadhiwa vizuri yanaweza yakaharibika, ni pamoja na mahindi, kwa sababu wadudu wanaanzia shambani moja kwa moja, mazao mengine ni maharage, kunde, udaga na mtama, sasa hayo mazao yasipowekwa vizuri, unakuta ni unga tu,” anabainisha Matekere.
Kifungu cha 5 cha Sheria Ndogo za (Kilimo Kwanza na Usalama wa Chakula) Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), kinataka serikali ya kijiji kuhakikisha kwamba kila mkazi wa kijiji anakua na ghala bora la kuhifadhia chakula na pembejeo.
Hata hivyo, licha ya takwa hilo la kisheria, bado wakulima wanalalamikia suala la ukosefu wa maeneo salama ya kuhifadhi mazao yao mara baada ya kuvuna, hasa mahindi.
Patrice Undole, mtaalamu wa kilimo kutoka mradi wa Kilimo Hifadhi unaosimamiwa na Kanisa la AICT mkoani Geita, anasema changamoto ya upotevu wa mazao bado ni kubwa licha ya jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali.
“Bado kuna upungufu wa elimu kwa hawa wakulima, wengi hawajapa elimu nzuri ambayo inaweza kuwasadia kuweza kupunguza huu uharibifu wa mazao, namna ya kuhifadhi,” anaeleza Patrice.
Patrice anaeleza kuwa hata pale ambapo teknolojia za kisasa za kuhifadhi zinapatikana, bado wakulima wengi hushindwa kuzipata kwa urahisi kutokana na umbali na gharama za kuzifuata.
“Upatikanaji wa hivi vifaa vya kufungia…Mifuko ya kinga njaa inapatikana, lakini haipatikani kwa urahisi na wakati. Tuchukilie mfano inapatikana hapa Geita, mkulima yupo kijijini labda kilomita 30, anaona ule ugumu kutafuta nauli, kuja mpaka hapa mjini kuchukua hiyo mifuko. Anaona kwamba anatumia gharama kubwa,” maelezo ya Patrice.
Maelezo hayo yanaonyesha kuwa kupunguza upotevu wa mazao si suala la kumwelekeza mkulima pekee. Ni suala linalohusisha upatikanaji wa teknolojia, miundombinu na huduma zinazomwezesha mkulima kuhifadhi mazao yake kwa usalama.
Ingawa baadhi ya wakulima wameanza kutumia mbinu zinazosaidia kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, wengi bado wanaendelea kukabiliana na changamoto zinazowafanya wapoteze sehemu ya mavuno yao kila msimu. Hali hiyo inaendelea kuibua maswali kuhusu kwa nini tatizo hili linaendelea kujirudia licha ya umuhimu wa mazao hayo kwa maisha na uchumi wa wakulima.
Katika sehemu ya pili ya makala hii, tutafuatilia kwa kina kinachochochea tatizo la uhifadhi duni wa mazao ya chakula na kwa nini linaendelea kuwa changamoto kwa wakulima wengi wa Geita.
Pia soma:
~ Jasho shambani, hasara ghalani: Chanzo cha upotevu wa mazao Geita
~ Jasho lisipotee ghalani: Njia za kuokoa mazao ya wakulima wa Geita
Andiko la: Dominic Allen
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.

Mkulima Mathayo Kanyelema akiwa anakausha mahindi kwa kuyaanika juani, hatua inayolenga kupunguza unyevu na kusaidia kuhifadhi mazao baada ya mavuno katika eneo la Geita. Hata hivyo, wakulima wengi bado wanakabiliwa na changamoto za uhifadhi unaoweza kusababisha upotevu wa sehemu ya mavuno yao.
Katika baadhi ya maeneo ya Geita, wakulima wameanza kuachana na mbinu za zamani za kuhifadhi mazao na kuhamia matumizi ya mifuko maalumu ya kinga njaa. Hata hivyo, si wote waliofanikiwa kufanya mabadiliko hayo.
Kajina Kaisanga, mkulima wa mahindi kutoka Nyambugu, Manispaa ya Geita, ni miongoni mwa waliobadili mfumo wa uhifadhi wa mazao yao baada ya kupata elimu ya uhifadhi bora wa mazao ya chakula.
“Mimi mazao yangu ninapoweka, huwa nayatoa shambani, nikiyavuna, nayaanika, natunza, naweka kwenye mifuko ya kinga njaa,” anasema Kajina.
Kajina amebainisha kuwa hatua hiyo ya kutumia mifuko ya kinga njaa imewasaidia kupunguza uharibifu wa mazao ukilinganisha na mbinu walizokuwa wakitumia zamani.
“Hizo njia za zamani ambazo tulikuwa tunatumia dawa, kwa sasa hivi huwa tunawatembelea wakulima, tunawashauri wanaweka kwenye kinga njaa,” anaeleza Kajina.
Wakulima wakikusanya na kufungasha mazao kwenye mifuko ya kinga njaa kwa ajili ya kuhifadhi ghalani, hatua muhimu katika kulinda mavuno dhidi ya upotevu baada ya kuvuna.
Boniface Kaswahili, Diwani wa Kata ya Shiloleli katika Manispaa ya Geita, anaonya kuwa upotevu wa mazao unaweza kuchangia kuendelea kwa changamoto ya njaa.
“Kwa hiyo wanaathirika vibaya, ndiyo maana unaweza ukakuta kwamba njaa haziishi,” anasema Boniface.
Marcel Magayane, ambaye ni mkulima mwezeshaji kutoka kijiji cha Nyambogo anaunga mkono hoja ya kwamba baadhi ya wakulima, hasa maeneo ya vijijini wapo kwenye hati hati ya kukabiliwa na njaa kutokana na uhifadhi mbovu.
“Athari moja ni upatikanaji wa mazao machache shambani na utunzaji wa mazao nyumbani… Maana yake kama mkulima amelima ekari moja, akapata gunia tatu, hiyo ni njaa tayari, ametunza mazao yake, yanabunguliwa, mahindi yaliyo mazuri ni kidogo, yaliyo mengi yatakuwa yamebunguliwa na wadudu, kwa hiyo ni njaa ya kutosha kabisa.”
Marcel anaeleza kuwa hapo awali katika kijiji anachoishi, wakulima walikuwa wakihifadhi mazao katika mifuko ya kawaida, hali iliyowaweka katika hatari ya kupoteza sehemu kubwa ya mavuno yao.
“Zamani tulikuwa tuna changamoto ya kubunguliwa mazao yetu, yaani namna ya uhifadhi ilikuwa sio nzuri, tulikuwa tunahifadhi katika mifuko ya kawaida," anaeleza Marcel.
Akisema changamoto hiyo katika kijiji cha Nyambogo imepungua baada ya wakulima kupata mafunzo kuhusu matumizi ya mifuko ya kinga njaa, ambayo husaidia kulinda mazao dhidi ya wadudu na kupunguza utegemezi wa kemikali katika uhifadhi.
Gharos Riwa, ambaye ni mdau katika sekta ya kilimo kutoka Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Geita anazungumzia athari za uhifadhi mbovu wa mazao ya chakula katika jicho la kibiashara.
“Tumekuwa tukiona athari kubwa inayotokea, hasa katika mazao haya ya kibiashara, yamekuwa yakileta madhara yakileta milipuko ya moto, lakini vilevile pia mazao kama mahindi kupunguza ubora kuwa na sumu kuvu. Na yote haya yanasabisha pengine hata sokoni ubora sokoni kutokuwa na ushindani wa kutosha,” anasema Gharos.
Gharos anaeleza kuwa mkulima asiyehifadhi vizuri ghalani hupata hasara kutokana na kupungua kwa ujazo unaosababishwa na mashambulizi ya wadudu waharibifu na changamoto nyingine.
Kwa upande wake mkulima Fortunatusi anasema kabla ya kupata mafunzo kuhusu mbinu bora za uhifadhi, alikuwa akitumia dawa za kuhifadhia mahindi kama ilivyozoeleka kwa wakulima wengi, baadaye alibadili mfumo huo baada ya kupata elimu.
“Zamani nilikuwa nahifadhi kwa kutumia sumu hizi mahindi, lakini baadae tulipofundisha na kampuni ya kilimo hifadhi, ndipo tukaona kwamba utunzaji wa kuweka sumu ni hatari, baadae nikawa naweka kwenye mifuko ya kinga njaa,” anazungumza Fortunatusi.
Matekere Mafuru, Afisa Kilimo wa Kata ya Shiloleli katika Manispaa ya Geita, mkoani Geita, anataja mahindi, maharage, kunde, udaga pamoja na mtama kuwa miongoni mwa mazao yanayohitaji uhifadhi makini.
“Mazao ambayo kwa kweli yasipohifadhiwa vizuri yanaweza yakaharibika, ni pamoja na mahindi, kwa sababu wadudu wanaanzia shambani moja kwa moja, mazao mengine ni maharage, kunde, udaga na mtama, sasa hayo mazao yasipowekwa vizuri, unakuta ni unga tu,” anabainisha Matekere.
Kifungu cha 5 cha Sheria Ndogo za (Kilimo Kwanza na Usalama wa Chakula) Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), kinataka serikali ya kijiji kuhakikisha kwamba kila mkazi wa kijiji anakua na ghala bora la kuhifadhia chakula na pembejeo.
Hata hivyo, licha ya takwa hilo la kisheria, bado wakulima wanalalamikia suala la ukosefu wa maeneo salama ya kuhifadhi mazao yao mara baada ya kuvuna, hasa mahindi.
Wakulima wakikagua mahindi, hatua muhimu kabla ya kuanika na kuhifadhi, ili kupunguza hatari ya uharibifu baada ya mavuno.