Juni 6, 2022, Shi Weixia, mfanyakazi wa makavazi ya wilaya ya Wenxian katika mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan, China ananakili vitabu vya kale na kubadilisha kurasa za vitabu vya kale kuwa mafaili ya picha.
Kuanzia mwaka jana, Makavazi ya Wenxian imekumbatia teknolojia za kisasa katika kupanga, kuhifadhi na kukarabati vitabu vya kale na kumbukumbu katika mkusanyiko wake, na imetumia nukishi ya mionzi na upigaji picha wa karibu kunakili vitabu vya kale kwa njia ya kidijitali, na kusukuma mbele uhifadhi na matumizi ya vitabu vya kale na kumbukumbu zake, ili vitabu hivyo, kumbukumbu na nyaraka "viendelee kuwepo" na kuweza kutumiwa ipasavyo.