Uhujumu NSSF

Uhujumu NSSF

Point hii..
Pole mtoa post inaonekana nawe ni wale wale ambao mirija ya ulaji imefungiwa sasa muna mu attack Erio. Mulizoea dezo dezo tu kufanya Shirika kama shamba la bibi munakula pesa za wanachama bila huruma shirika linatafunwa kila upande na wafanyakazi wasio waaminifu sasa Erio amekuja ameziba mirija yenu yote ndio mnamu attack poleni sana Hapa ni Kazi tu kashasema Baba vipi sauti inatosha huko nyuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI,

Wafanyakazi wa NSSF, tunaendelea kuwasilisha malalamiko yetu kwako kuhusu ufisadi na ubaguzi uliopo shirikani ili ufanye uchunguzi wako na uchukue hatua stahiki ili kuliokoa shirika letu.

1. Udanganyifu katika utendaji wa shirika.

Mkurugenzi Mkuu kwa makusudi kabisa aliopoingia shirikani alipunguza malengo yaliyokwisha wekwa na mtangulizi wake ili aonekane 'anaperfom" hivyo taarifa zikawa zinapelekwa wizarani zikionesha anavuka malengo kwa mwaka wa 2018/2019.

Mwaka 2019/2020 kwa ujanja kabisa hakukuwa na ongezeko lolote la malengo bali alichofanya ni kujumlisha michango na wanachama waiohamia NSSF kutoka mifuko mingine kwenye makusanyo ya mwaka uliopita, hivyo inaonekana ameongeza makusanyo kwa asilimia kubwa sana na amekuwa akipita na kujisifu kwa hilo.

2. Ubaguzi kwa wafanyakazi.

Mkurugenzi huyu amekuwa akifanya ubaguzi wa wazi baina ya staff aliotoka nao PPf na sisi wa NSSF, kwa mfano staff wote wa PPF wamewekwa makao makuu tu hawapelekwi mikoani.

Aidha kuna staff ambao PPF hawakuwa na cheo chochote lakini walilopokuja NSSF wamepewa umeneja.

3. Ubaguzi katika mishahara.

Inafahamika wazi kuwa mfanyakazi wa umma anapohamishiwa kwenye taasisi nyingine anahamia na mshahara wake iwapo ni mkubwa.

PPF mishahara yao ilikuwa ni mikubwa kuliko NSSF. Lakini kwa hila kabisa akatumia kipengele cha kodi ya nyumba na kuwqaongezea mishahara staff aloikuja nao kutoka PPF, kisha wakaingia mikataba na mabenk chap chap wakaikopea nyongeza ile yote hii mantiki yake ni kukwepa hoja za CAG iwapo wangekopeshana kupitia mikopo ya shirika na vile vile kujilipa in advance in case of anything. Jamaa ni mjanja sana yeye na watu wake.

4. Dhuluma kwenye makato ya wafanyakazi.

Ndani ya NSSF kuna mpango wa uchangiaji wa wanachama wa NSSF-Hiari kwa wafanyakazi ambapo mwajiri anachangia 10% na mfanyakazi anakatwa 10%.

Mpango huu haupo NSSF peke yake bali mashirika mengi yana mpango kama huu kwa namna tofauti hata PPF walikuwa nao na walilipana mafao mifuko ilipounganishwa.

Mwezi Desemba 2018 mkurugenzi mkuu alisitisha kuchangia 10% yake bila taarifa yoyote huku akiendelea kuwakata wafanyakazi mpaka hivi leo licha ya wafanyakazi wengi kuandika barua kuomba makato hayo yasitishwe.

Mwezi Desemba 2019 mkuu huyu aliitisha baraza la majadiliano na kuwafahamisha kuwa alisitisha makato kutokana na agizo lako ulilotoa ulipokutana na viongozi wa mifuko mwezi Desemba, 2018 hivyo amekuja na mpango mpya ambao itabidi michango yote iliyokokwisha changiwa NSSF kiasi cha bilioni 23 kitolewe na uanzishwe mfuko binafsi wa wafanyakazi utakao kuwa na bodi yake na uongozi wake utakaojumuisha na wafanyakazi waliohamia.

Wawakilishi wa wafanyakazi walijua huu ni mchezo mchafu aina ya DESI, hivyo wakaugomea mpango huo na ikakubaliwa kuwa makato kwa wafanyakazi yasitishwe kuanzia mwezi Desemba, 2019.

Na michango iliyopo iendelee kubaki NSSF, Cha kushangaza makato yanaendelea mpaka sasa na hatujui kimsingi mkuu anahitaji nini hasa.

Mheshiwa Rais, tunaomba uingilie kati, kwani tunakufahamu na wewe ni msema kweli na mtetezi wa wanyonge.

Mungu akubariki!

Mkurugenzi William Erio ni mtu mchapakazi asiyetaka watu wazembe kama wewe mtoa post.Ni mwendawazimu tu asiyejua ni jinsi gani PPF ilivyokuwa akichapa kazi ukilinganisha na NSSF.

Wafanyakazi wengi tu wa NSSF mlishazoea rushwa na wizi sasa kaletwa kiongozi mchapa kazi mmeanza majungu! Hapo makao makuu ni lazima awe na watu wachapa kazi, waaminifu na wazalendo ili shirika lisiyumbe kama lilivyokuwa mwanzoni. Mnaacha kuongelea ni jinsi gani viongozi wezi kwa kushirikiana na wafanyakazi wezi na wala rushwa kama wewe mtoa post mlivyosababisha kutowalipa wanachama michango yao kwa muda stahili kwa kutumia michango hiyo katika ujenzi wa majengo kama yale ya DEGE ECO VILLAGE Kigamboni ambayo sasa ujenzi wake haujaisha na kugeuka kuwa magofu na miradi mingine kwa manufaa ya matumbo ya viongozi wezi! Watu hawa wanafahamika, watafutwe na kukamatwa na kisha wafunguliwe mashitaka.

Matumizi haya ya hovyo ya pesa za wafanyakazi ni dhambi kubwa sana! Kuna watu wameishakufa bila kulipwa mafao yao na wengine mpaka leo hawajalipwa kutokana na shirika la NSSF kutokuwa na pesa za kutosha kulipa mafao ya wanachama kutokana na utendaji wa hovyo kabisa uliofanywa na viongozi wa shirika na viongozi wa serikali waliopita! Mheshimiwa Rais Magufuli anajaribu kulifufua shirika hili tayari mashetani mmeanza kuleta majungu!

Toka Mheshimiwa Rais alipomteua mkurugenzi William Erio kumekuwa na mabadiliko ya kuridhisha kiutendaji ndani ya NSSF ikiwa ni pamoja ma mafao kuanza kulipwa kwa kutochukua muda mrefu kama zamani japo bado kuna wafanyakazi wachache kama wewe mtoa post mambo yenu bado hayajabadilika bado mnaendelea na tabia zenu za kuzungusha watu kwa kuchelewesha kutoa huduma haraka na kupeleka siku au miezi mbele zaidi ili ionekane kuna ugumu katika kupata mafao wakati kumbe nyie mnatengeneza mazingira ya rushwa! Ole wenu, zama hizi siyo zile za mjomba.

Pale NSSF UBUNGO kuna baadhi ya wafanyakazi (kwa mfano dada anayetoa huduma dirisha namba 5 ana kauli mbaya kwa wanachama, anachelewa kuanza kazi mpaka afuatwe na askari wa SUMA JKT waliopo pale ndani na wakati mwingine anakuwa busy akiongea au akichati kwenye simu) ambao nao hawataki kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais kwa kumteua mkurugenzi William Erio katika kuwatumikia wananchi. Hapo hapo NSSF UBUNGO kuna baadhi ya wafanyakazi wachache kama Oisso huyu yupo ghorofa ya 9 ni mtu anayejituma sana katika kuwatumikia wanachama wenye shida mbalimbali tena bila hata kujali kama hiyo shida inamhusu yeye kiutendaji!
 
Ngoja niendelee kusoma comment

Huyo kiongozi wenu yuko vizuri, hatukuwahi kusikia kelele wakati yuko PPF, tatizo mlizoeshwa vibaya huko NSSF sasa hamtaki kubadilika, pambaneni na hali zenu. Muheshimiwa Raisi, achana na hawa maboya, jenga taifa.
Palikuwa na udini sana pale, Ameingia Farao asiye mjua Yusuph, wameanza lalamika, fanya adaptation, wewe hujui kila shetani na Mbuyu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom