Uhujumu NSSF

Point hii..
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkurugenzi William Erio ni mtu mchapakazi asiyetaka watu wazembe kama wewe mtoa post.Ni mwendawazimu tu asiyejua ni jinsi gani PPF ilivyokuwa akichapa kazi ukilinganisha na NSSF.

Wafanyakazi wengi tu wa NSSF mlishazoea rushwa na wizi sasa kaletwa kiongozi mchapa kazi mmeanza majungu! Hapo makao makuu ni lazima awe na watu wachapa kazi, waaminifu na wazalendo ili shirika lisiyumbe kama lilivyokuwa mwanzoni. Mnaacha kuongelea ni jinsi gani viongozi wezi kwa kushirikiana na wafanyakazi wezi na wala rushwa kama wewe mtoa post mlivyosababisha kutowalipa wanachama michango yao kwa muda stahili kwa kutumia michango hiyo katika ujenzi wa majengo kama yale ya DEGE ECO VILLAGE Kigamboni ambayo sasa ujenzi wake haujaisha na kugeuka kuwa magofu na miradi mingine kwa manufaa ya matumbo ya viongozi wezi! Watu hawa wanafahamika, watafutwe na kukamatwa na kisha wafunguliwe mashitaka.

Matumizi haya ya hovyo ya pesa za wafanyakazi ni dhambi kubwa sana! Kuna watu wameishakufa bila kulipwa mafao yao na wengine mpaka leo hawajalipwa kutokana na shirika la NSSF kutokuwa na pesa za kutosha kulipa mafao ya wanachama kutokana na utendaji wa hovyo kabisa uliofanywa na viongozi wa shirika na viongozi wa serikali waliopita! Mheshimiwa Rais Magufuli anajaribu kulifufua shirika hili tayari mashetani mmeanza kuleta majungu!

Toka Mheshimiwa Rais alipomteua mkurugenzi William Erio kumekuwa na mabadiliko ya kuridhisha kiutendaji ndani ya NSSF ikiwa ni pamoja ma mafao kuanza kulipwa kwa kutochukua muda mrefu kama zamani japo bado kuna wafanyakazi wachache kama wewe mtoa post mambo yenu bado hayajabadilika bado mnaendelea na tabia zenu za kuzungusha watu kwa kuchelewesha kutoa huduma haraka na kupeleka siku au miezi mbele zaidi ili ionekane kuna ugumu katika kupata mafao wakati kumbe nyie mnatengeneza mazingira ya rushwa! Ole wenu, zama hizi siyo zile za mjomba.

Pale NSSF UBUNGO kuna baadhi ya wafanyakazi (kwa mfano dada anayetoa huduma dirisha namba 5 ana kauli mbaya kwa wanachama, anachelewa kuanza kazi mpaka afuatwe na askari wa SUMA JKT waliopo pale ndani na wakati mwingine anakuwa busy akiongea au akichati kwenye simu) ambao nao hawataki kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais kwa kumteua mkurugenzi William Erio katika kuwatumikia wananchi. Hapo hapo NSSF UBUNGO kuna baadhi ya wafanyakazi wachache kama Oisso huyu yupo ghorofa ya 9 ni mtu anayejituma sana katika kuwatumikia wanachama wenye shida mbalimbali tena bila hata kujali kama hiyo shida inamhusu yeye kiutendaji!
 
Ngoja niendelee kusoma comment
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kiongozi wenu yuko vizuri, hatukuwahi kusikia kelele wakati yuko PPF, tatizo mlizoeshwa vibaya huko NSSF sasa hamtaki kubadilika, pambaneni na hali zenu. Muheshimiwa Raisi, achana na hawa maboya, jenga taifa.
Palikuwa na udini sana pale, Ameingia Farao asiye mjua Yusuph, wameanza lalamika, fanya adaptation, wewe hujui kila shetani na Mbuyu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…