Uhujumu wa Bandari yetu

Uhujumu wa Bandari yetu

Marathon day

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2020
Posts
643
Reaction score
1,016
Kuna hujuma ya kupunguza mapato ya nchi dhidi ya sheria tata za pollice wetu, baada ya hizi ajali za mara kwa mara police wameweka sheria hizi gari za IT kutokubeba mtu zaidi ya dereva tu.

Sasa unakuta mtu anakuja kuchukua gari yake, hapohapo afanye shopping, aje na mkewe au mtoto wake, atakua amechangia kodi kubwa tu, Mtu amepitishia truck au bus, inabidi akodi dereva amuendeahe na yeye asimamie gari yake anunue na mizigo yake Kariakoo, hapo amechangia pato la taifa.

Police wetu wamegeuza hiyo ni mradi, gari awepo dereva tu. Usiweke hata box moja ndani ya gari nishida njia nzima. Sasa hivi wa congoman na wazambia wameanza kupitishia mizigo yao Duban SA na Maputo msumbiji.

Wahusika tutizame shwalla hili.
 
Polisi wamekua chanzo cha kukimbiza tena wateja wa bandari yetu, ilifanyika nguvu kubwa kujaribu kuwarudisha, baada ya wateja wengi kukimbilia bandari za nchi jirani.
 
Hakuma hujuma. Madereva wa gari za IT ni watu wapumbavu, nilikua nashangaa Sana kuona wanapakark pale mbezi na Kibamba ili kubeba abiria wa mikoanj. Huu ni upumbavu kabisa
 
Hapo tatizo ni njaa tu, hao polisi sio kwamba hawataki upakia mtu mwingine na mizigo, bali wanataka upakie ili wakukamte uwape rushwa..., tena wanafurahi sana ukipakia
 
Hakuma hujuma. Madereva wa gari za IT ni watu wapumbavu, nilikua nashangaa Sana kuona wanapakark pale mbezi na Kibamba ili kubeba abiria wa mikoanj. Huu ni upumbavu kabisa
Wapakie tu, we unaona raha gari kutembea tupu? Wawekewe kanuni na taratibu ili lifanyike rasmi
 
Kunahujuma ya kupunguza mapato ya nchi dhidi ya sheria tata za pollice wetu, baada ya hizi ajali za mara kwa mara police wameweka sheria hizi gari za IT kutokubeba mtu zaidi ya dereva tu.

Sasa unakuta mtu anakuja kuchukua gari yake, hapohapo afanye shopping, aje na mkewe au mtoto wake, atakua amechangia kodi kubwa tu, Mtu amepitishia truck au bus, inabidi akodi dereva amuendeahe na yeye asimamie gari yake anunue na mizigo yake Kariakoo, hapo amechangia pato la taifa.

Police wetu wamegeuza hiyo ni mradi, gari awepo dereva tu. Usiweke hata box moja ndani ya gari nishida njia nzima. Sasa hivi wa congoman na wazambia wameanza kupitishia mizigo yao Duban SA na Maputo msumbiji.

Wahusika tutizame shwalla hili.
Nikiwaambia kuwa mkataba baina ya shetani na CCM ndo unaoleta maumivu haya ndo mnielewe.

Hapo wanazalisha tatizo kisha kesho anasimama makamu wa chama taifa anakemea polisi waache kuwasumbua watu wa IT atapigiwa makofi well done.

Nchi inahitaji maombi ya kujitoa haswaaa
 
Ninavyofahamu mimi mmiliki kwa hurumua tu hakatazwi kupanda hilo Gari lake ongawaje kisheria na kiitaratibu haitakiwi cha msingi aonyeshe nyaraka zitakazomtambulisha kama ndiye mmiliki na hata familia aonyeshe nyaraka kuthibitisha ni familia yake .
Na mizigo pia aonyeshe nyaraka .
Tatizo ninaloliona Mimi ni risk yake tu kwani hizo Gari za transit bima yake ni ndogo Kwa ajili ya transit tu mtu mwingine zaidi ya dreva hawi covered pindi ikitokea ajali.
Acheni kulaumu vitu vingine ambavyo huvielewi
 
Je kinachosababisha ajali ni wale abiria waliobebwa ndani ya hayo magari? Je mabasi yasibebe abiria kisa ajali? Magari ya maiti yasibebe waombolezaji kisa ajali? Hii nchi ni hovyo sana Akili ndogo kuwa kwenye maamuzi ni tatizo sana.
 
Back
Top Bottom