GE2025 Uhuni unaoendelea kushuhudiwa katika kura za maoni ndani ya CCM ni dalili ya kuporomoka kwa maadili ya kisiasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

ILAN RAMON

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
10,292
Reaction score
4,976
Uhuni unaoendelea kushuhudiwa katika kipindi hiki cha kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni dalili ya kuporomoka kwa maadili ya kisiasa na ukosefu wa utawala wa sheria ndani ya mfumo wa chama hicho. Matukio ya kukodi vijana wahuni ili kuwadhuru wapinzani wa kisiasa ndani ya chama, uporaji wa mali na fedha, ujazaji wa kura feki, pamoja na vitisho, vinaonyesha jinsi mchakato wa kidemokrasia unavyogeuzwa kuwa uwanja wa mapambano yasiyo ya kisiasa bali ya kimabavu.

Swali muhimu la kujiuliza ni hili: kama wanachama wa CCM wenyewe wanatendewa haya madhila makubwa na wenzao kwa sababu tu ya kugombea nafasi za uongozi, ni madhila ya aina gani wapinzani wa kisiasa watafanyiwa pale ambapo vyombo vya dola kama polisi, mahakama, na taasisi za usalama zipo upande wa chama tawala? Ikiwa ndani ya chama chenyewe hakuna heshima kwa haki, taratibu, na sheria, ni wazi kuwa katika medani ya ushindani wa vyama vingi, wapinzani wataendelea kuwa waathirika wakubwa wa mifumo ya kidhalimu.

Matukio haya yanadhihirisha kuendelea kwa siasa za mabavu na kukosekana kwa uadilifu wa kisiasa nchini. Ujenzi wa demokrasia ya kweli hauwezi kufikiwa iwapo chama tawala hakitaonyesha mfano wa kuzingatia haki, uwazi, na amani katika mchakato wake wa ndani. Aidha, hali hii inazidi kuwakatisha tamaa vijana na wananchi kwa ujumla, na kuendeleza imani kuwa siasa ni eneo la giza na hatari.

Ni wakati muafaka kwa viongozi wa CCM na taasisi huru za kikatiba kuchukua hatua madhubuti kusafisha mfumo huu kabla haujaleta athari kubwa kwa ustawi wa taifa.
 
Hii ni kawaida kwa kiongozi au chama kinapokaa madarakani muda mrefu, mara nyingi upatikanaji wa madaraka hutumika njia za kihalifu, rushwa, udanganyifu na uchafu kama huo. Na mara nyingi vyama hivi hutoka madarakani baada ya umwagaji mkubwa wa damu.
 
Mwenyekiti muhuni na anashirikiana na wahuni. Unategemea nini kwa wanachama wa kawaida.
Ni uhuni uhuni
 
Kuiba kura
Rushwa
kutekena na
kupigana makonde
Ndio tafsiri rasmi kabisa ya namna ccm ilivyo kwa sasa!
 
Back
Top Bottom