'Uhuni' unaofanywa na Mawakala wa Kampuni za Bia unashangaza

'Uhuni' unaofanywa na Mawakala wa Kampuni za Bia unashangaza

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
317
Reaction score
520
Wadau, salaam Kuna Mawakala wa kutangaza (promotion) bia za kampuni za bia nchini kama Tanzania Breweries Ltd na Serengeti Breweries.

Yaani iko hivi, hawa Mawakala wao kazi yao ni kutafuta wasichana warembo na kwenda nao kwenye baa kubwa ambapo huwapa bia ili wazitembeze kwa wateja wa baa husika kwa bei ya ofa.

Shughuli hii (mara nyingi) huanza saa kumi jioni siku za wikiendi na kumalizika saa 6 usiku huku warembo hao wakiwa wamevaa sketi fupi, raba na blauzi ya sare (kuvutia wateja).

Malipo yao yako hivi; kila wanapofunga promotion usiku hupewa shilingi elfu tano nauli ya kumrejesha mrembo nyumbani. Lakini Jumatano ya kila wiki hutakiwa kilipwa Tsh. 30,000. Kwa hiyo kwa mwezi ni sawa na kulipwa Tsh. 120,000 (endapo watalipwa kweli).

Tafsiri ya uwakala huu ni kwamba, kampuni za bia wao huwalipa mawakala ambao nao huwalipa watu wao kwa ujumla wake.

Sasa, kuna kitu cha kushangaza, ni kwamba, kuna Meneja wa Mawakala mmoja, amekuwa akihaha kutafuta warembo ili wakatangaze bia husika kwenye baa. Lakini warembo siku hizi wamekuwa wagumu kukubali tofauti na zamani.

Kumbe bwana, wakala wa meneja huyo hawawalipi warembo ndiyo maana kila wakati wanatafuta warembo wapya kwa sababu wale wa kwanza wanakataa wakisema mpaka walipwe stahiki zao.

Mfano sahihi; kuna msichana mmoja, mkazi wa Gongo la Mboto, Desemba mwaka jana, alishiriki kutangaza bia za Guinness kwenye baa za Gongo la Mboto. Lakini Mawakala hawakuwahi kumlipa Jumatano yoyote achilia mbali ile waliyomuahidi.

Januari, 2022, meneja akadai uongozi ulikwenda likizo ya X-Mass, umerejea pesa italipwa. Haikulipwa.

Katikati ya Januari, 2022, mdada mmoja kutoka ofisini kwa Wakala husika akampigia simu msichana 'mhanga' akamwambia avumilie pesa yake italipwa wiki inayofuatia, hawakulipa!

Februari ilipoanza, hawakulipa. Katikati ya Februari, mdada (huenda ni mwingine au yuleyule) akampigia tena simu 'mhanga', akamuuliza akitumiwa pesa yake jina gani litasoma, akajibiwa. Hakuna kilichoendelea mpaka leo tarehe 1/3/2022 ni kimya!

Wasiwasi uliyopo, huenda kampuni ya bia yenyewe haijui. Au yenyewe ndiyo inazembea kuwalipa Mawakala ili nao wawalipe warembo wao.
 
FB_IMG_16446785616937164.jpg
 
Haya makampuni kwanini yanaruhusu unyonyaji kwa kuweka wapigaji kati kati kwanini wasiwalipe direct na kuhakikisha wanapata kile wanachostahili ?
 
Haya makampuni kwanini yanaruhusu unyonyaji kwa kuweka wapigaji kati kati kwanini wasiwalipe direct na kuhakikisha wanapata kile wanachostahili ?
Ktk biashara kubwa kubwa hizo mtu wa kati(wakala)huwezi kumkwepa, yaani TBL/SBL kila kazi wafanye wao wataweza?hata kama hilo lingewezekana bado kuna shida, kazi ngapi za serikali zinafanywa na watumishi wenyewe lakini bado watu wanadhurumika?!!
 
Sadly true. Kuna sista anahangaishwa malipo toka mwaka jana. Wakilipa wanalipa kiduchu. Wanazingua sana
 
Ktk biashara kubwa kubwa hizo mtu wa kati(wakala)huwezi kumkwepa, yaani TBL/SBL kila kazi wafanye wao wataweza?hata kama hilo lingewezekana bado kuna shida, kazi ngapi za serikali zinafanywa na watumishi wenyewe lakini bado watu wanadhurumika?!!
Basi waweke mfumo mzuri na transparency including auditing ya ao outsourced middle firms.
 
Umenikumbusha Mrembo wangu wa Budwiser sikuhizi sionani nae sijui naye amekutwa na madhila haya
 
Back
Top Bottom