Uhuru ahimiza kiswahili kitumiwe kuunganisha afrika mashariki

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
RAIS Uhuru Kenyatta ametoa wito Kiswahili kitumiwe kuleta umoja baina ya wananchi wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akihotubia wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) waliokuwa katika Bunge la Kitaifa Nairobi Jumanne, rais alisema utumizi wa Kiswahili baina ya wananchi wa EAC ni njia mwafaka ya kudumisha utambulisho wa pamoja ulio wa kipekee.
“Mungu ametupatia sauti inayoweza kuleta umoja baina ya wananchi wote Afrika Mashariki, na tunafaa tuitumie ipasavyo kupitia vyombo tofauti vya habari ili kutimiza utangamano,” alisema.

Hata hivyo, kinaya iliyodhihirika ni kuwa alitoa hotuba yake yote kwa Kiingereza.

Rais Kenyatta alitoa hakikisho kuwa juhudi za kutimiza umoja kati ya mataifa ya EAC ziko sambamba, ingawa hakuna usawa kati ya mataifa katika utekelezaji wa mikakati ya kukamilisha juhudi hizo.

Alitoa wito kwa wabunge hao wajitahidi kupitisha sheria zitakazodumisha umoja wa EAC, hasa zinazohusu uendelezaji wa biashara kati ya mataifa husika.

Spika wa bunge la EALA Margaret Zziwa alimmiminia sifa Rais Kenyatta kwa kusema amedhihirisha kujitolea kwa Serikali anayoongoza katika kutimiza maazimio ya EAC.

Kulingana na Bi Zziwa, hatua ya Serikali kukabiliana na changamoto zilizokuwa zikiwakumba wafanyabiashara wanaopitisha mizigo katika maeneo ya mipaka na katika bandari ya Mombasa ni ishara ya kujitolea kwa Serikali kutimiza malengo ya EAC.

“Hatua hii imeboresha biashara na hakika, wafanyabiashara katika mataifa ya EAC tayari wanafaidika kwenye biashara zao,” alisema.

Mwenyekiti wa wabunge wa EALA kutoka Tanzania Adam Kimbisa, alimshauri Rais Kenyatta awe “mtumwa” kwa wananchi.

“Maisha yako sasa yamebadilika kutoka uhuru na kuwa utumwa. Ukiwa mtumwa kwa wananchi, hiyo ni taadhima na baraka kwako, na Mungu atakubariki sana,” alisema Bw Kimbisa.

Vijana

Alitumia muda aliopewa kumsifu Rais Kenyatta kwa kujitolea kwake kuleta umoja baina ya mataifa ya bara la Afrika.

Alizua kicheko bungeni alipomwambia Rais Kenyatta ashauri viongozi wenzake wa mataifa ya Afrika kuhusu jinsi ya kutawala kama vijana.

“Nadhani itakuwa msaada sana ukionana na marais wenzako na kuwaambia “waoneni hawa vijana”, nao waweze kuchangamka,” alisema.

Rais pia alisifiwa kwa mipango ya kipekee iliyoanzishwa na Serikali, kama vile mradi wa kupeana vipakatalishi kwa watoto wa shule za msingi.

“Kuna mataifa mengi Afrika ambayo yameshindwa kununulia wanafunzi kitabu na kalamu, ilhali wewe unafuata mkondo wa dijitali kwa elimu,” alisema Bw Kimbisa.

Alikariri msimamo wa EALA kuunga mkono Muungano wa Afrika (AU) kuhusiana na kesi zinazomkabili rais na naibu wake William Ruto katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Uhuru ahimiza Kiswahili kitumiwe kuunganisha Afrika Mashariki - HABARI ZA MIKOANI - swahilihub.com
 
Katika nchi zote za jumuiya ya Afrika mashariki. Tanzania ndio yenye makabila mengi kuliko zote lakini ndio inayoongoza kwa kuzungumza kiswahili.Tuna vyombo vingi vya, Habari yakiwemo magazeti,runinga na,radio lakini hakuna hata kimoja kinachotoa matangazo yake kwa Lugha ya kikabila zaidi ya Kiswahili, ila hao wengine mmmh kazi ipo
 
Kwet Kenya huwa tuna celebrate our diversity, uwezo wa kuongea lugha zetu za asilia pamoja na kuongea Kiswahili. Haimanishi kwa kupenda tamaduni zako na lugha yako ya asili kwamba huo ni ukabila.
 
[video=youtube_share;G0WfPq8okno]http://youtu.be/G0WfPq8okno[/video]
 
Kwet Kenya huwa tuna celebrate our diversity, uwezo wa kuongea lugha zetu za asilia pamoja na kuongea Kiswahili. Haimanishi kwa kupenda tamaduni zako na lugha yako ya asili kwamba huo ni ukabila.

Ni ujinga tu hebu fikiria mtu unaenda kwenye mkutano wa kampeni ya siasa mgombea anahutubia kilugha chake.Hivi hayo maeneo hamna watu wa makabila mengine kama wafanyakazi wa serikali n.k ambao sio kabila hiyo? Je hao sio wapiga kura ambao walitakiwa wasikie anachoongea mgombea?

Tanzania tulipiga marufuku lugha za makabila kutumika kwenye mikutano, vyombo vya habari tukijua umuhimu wa kila mtu kusikia kile kinachoongelewa.Kenya ni balaa hata makanisani nina mtoto nilizaa na mkristo alienda kusali akakuta watu wanasali lugha ya kikikuyu kanisani.Alirudi bila kusali.Hovyo kabisa.

Tabaduni kama hizo zimepitwa si tu na wakati bali hazijengi taifa zinakazia ukabila kwanza utaifa baadaye.
 
Hujanielewa sijasema lugha za asili zizadharauliwe mbona hata Tz tunaongea? Ila kuzipa kipaumbele katika media ni ujinga uliopitiliza wakati ipo lugha nyingine mama ambayo wanaweza kuzungumza watu wote tena bila kupitia darasani kama jinsi ilivyo kwa hayo makabila mnayojivunia kwenu hebu ngoja niishie hapa halafu kama kuna jambo jingine we uliza tu
 
Ni ujinga tu hebu fikiria mtu unaenda kwenye mkutano wa kampeni ya siasa mgombea anahutubia kilugha chake.Hivi hayo maeneo hamna watu wa makabila mengine kama wafanyakazi wa serikali n.k ambao sio kabila hiyo? Je hao sio wapiga kura ambao walitakiwa wasikie anachoongea mgombea?

Tanzania tulipiga marufuku lugha za makabila kutumika kwenye mikutano, vyombo vya habari tukijua umuhimu wa kila mtu kusikia kile kinachoongelewa.Kenya ni balaa hata makanisani nina mtoto nilizaa na mkristo alienda kusali akakuta watu wanasali lugha ya kikikuyu kanisani.Alirudi bila kusali.Hovyo kabisa.

Tabaduni kama hizo zimepitwa si tu na wakati bali hazijengi taifa zinakazia ukabila kwanza utaifa baadaye.
Unafaa uelewe kuna sehemu kule vijijini kabisa inabidi lazima utumie lugha inayoeleweka, kwani umuhimu wa lugha nini kama sio kueleweka. Ninacho jaribu kusema hapa ni kuwa kwa kujivunia tamaduni zako kama mfano Wamaasai huo sio ukabila, tatizo ni kuwabagua watu kwa misingi ya kikabila.
 
Inafaa ifahamike Wakenya sio wa kwanza kutumia lugha zao za asilia, hata Afrika Kusini hadi Nigeria na hata mataifa ya mbali. Kwa kujivunia lugha na tamaduni zetu kunatufanya kufurahia maisha na kujiamini na sote tunajivunia utaifa kwa jumla. Huwa napenda sana kuwasikliza Wakenya wenzangu wakiongea Kiswahili na Kingereza kwa lafudhi tofauti, yaani Mjaluo na Mkikuyu wanapo wasiliana kwa lafudhi tofauti inapendeza maana hiyo ni taswira ya diversity na ndio maana watalii huja kwetu hata wakati Alshabaab wanarusha mabomu.
Ubaguzi wa kikabila ndio saratani inayotumaliza, ila kuna mipango mingi sasa ambayo inaelekea kupunguza huu ugonjwa. Mfano, sasa kuna serikali za mikoa (counties), hivi kuna ushindani wa mikoa katika kuwakaribisha wawekezaji tokea mikoa mingine.
 
Unachotaka kusema ni kuwa utaifa kenya bado haujafika vijijini.Hivyo inabidi utumie lugha yao.Na ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya wakenya wanakaa vijijini basi hilo ni janga la umoja wa kitaifa.

Pia kubagua mtu kikabila si tu kumnyima kazi na fursa ni pamoja na kuongea kilugha cha kikabila chako mbele yake iwe kwenye mikutano ya hadhara au vyombo vya habari.Huo ni ubaguzi tena mbaya wa kikabila kuliko ubaguzi mwingine wowwote.

Unaona gazeti uko katikati ya Nairobi lina vichwa na picha nzuri unatizama unalipenda taabu unaona limeandiandikwa kilugha cha kikabila unafungua radio unasikia watu wanatangaza kilugha chao.hovyo kabisa.

Hivi kuuza magazeti yaliyoandikwa kilugha nairobi na miji mikuu lengo ni nini kama sio kukuza ukabila? Mtu kama anajua kusoma na kuandika je kweli hajui lugha ya taifa? Kenya kukuza ukabila mmekubuhu.
 
Unachotaka kusema ni kuwa utaifa kenya bado haujafika vijijini.Hivyo inabidi utumie lugha yao.Na ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya wakenya wanakaa vijijini basi hilo ni janga la umoja wa kitaifa.

Pia kubagua mtu kikabila si tu kumnyima kazi na fursa ni pamoja na kuongea kilugha cha kikabila chako mbele yake iwe kwenye mikutano ya hadhara au vyombo vya habari.Huo ni ubaguzi tena mbaya wa kikabila kuliko ubaguzi mwingine wowwoteUnaona gazeti uko katikati ya Nairobi lina vichwa na picha nzuri unatizama unalipenda taabu unaona limeandiandikwa kilugha cha kikabila unafungua radio unasikia watu wanatangaza kilugha hovyo kabisa.

Kutokujua lugha ya taifa haimaniishi huna utaifa, kawaida nchi zote dunia vijijini watu huongea lugha za asilia.
Ubaguzi ni wakati unaongea lugha ya asilia kuhusu jambo linalomhusu mtu mwengine asiyeelewa unachokisema, lakini kama hayamhusu basi huo sio ubaguzi. Ingalikua huo ni ubaguzi, basi labda Bongo mungewafukuza Wahindi, Wachina, Wazungu wote maana wao hutumia lugha zao wanapowasiliana wao kwa wao.
 
Tuje mifano halisi uko mombasa unakutana na magazeti yaliyoandikwa kwa lugha ya kikikuyu yanauzwa pale posta mombasa kule hakuna kijiji cha wakikuyu kama sio ubaguzi wa kikabila ni nini?

Mikutano ya hadhara usiseme mimi mwenyewe nilikuwepo baadhi ya maeneo ujaluoni,ukambani na ukikuyuni hali inatisha hata waandishi wa habari mtu inabidi azunguke na waandishi wa kabila yake inatisha jamani.Sikubaliani na matumizi ya lugha za asili kwenye political campains.Watazamaji na wasikilizaji si watu wa kabila zenu tu please.
 
Kila kampuni ina mikakati ya kuwalenga walaji wa bidhaa zake. Magazeti hayo ya lugha yanawalenga watu wanao uwezo wa kuongea lugha hizo, kuna watu wanachangamoto katika matumizi ya lugha ya taifa ya Kiswahili na wakisoma kwa lugha zao za asilia wanauwezo wakuelewa kwa undani. Umuhimu wa lugha ni kuelewana, nina uhakika hata Tanzania lazima kuna magazeti yameandikwa kwa lugha ya kingereza na hayawalengi Watanzania wote.
 
Tuje mifano halisi uko mombasa unakutana na magazeti yaliyoandikwa kwa lugha ya kikikuyu yanauzwa pale posta mombasa kule hakuna kijiji cha wakikuyu kama sio ubaguzi wa kikabila ni nini?

Mikutano ya hadhara usiseme mimi mwenyewe nilikuwepo baadhi ya maeneo ujaluoni,ukambani na ukikuyuni hali inatisha hata waandishi wa habari mtu inabidi azunguke na waandishi wa kabila yake inatisha jamani.Sikubaliani na matumizi ya lugha za asili kwenye political campains.Watazamaji na wasikilizaji si watu wa kabila zenu tu please.

Kenya hakuna ukabila
 
Inafaa ifahamike Wakenya sio wa kwanza kutumia lugha zao za asilia, hata Afrika Kusini hadi Nigeria na hata mataifa ya mbali. Kwa kujivunia lugha na tamaduni zetu kunatufanya kufurahia maisha na kujiamini na sote tunajivunia utaifa kwa jumla. Huwa napenda sana kuwasikliza Wakenya wenzangu wakiongea Kiswahili na Kingereza kwa lafudhi tofauti, yaani Mjaluo na Mkikuyu wanapo wasiliana kwa lafudhi tofauti inapendeza maana hiyo ni taswira ya diversity na ndio maana watalii huja kwetu hata wakati Alshabaab wanarusha mabomu.
Ubaguzi wa kikabila ndio saratani inayotumaliza, ila kuna mipango mingi sasa ambayo inaelekea kupunguza huu ugonjwa. Mfano, sasa kuna serikali za mikoa (counties), hivi kuna ushindani wa mikoa katika kuwakaribisha wawekezaji tokea mikoa mingine.

sikia wewe mkenya, afrika ya kusini na nigeria ukiacha kugha ya malkia, hawana lugha nyingine zaidi ya lugha zao za makabila. Ila nyinyi wakenya mnaweka mbele kiingereza na lugha zenu za makabila huku mkifanya kiswahili kuwa lugha ya tatu, so, msijilinganishe na wanigeria au S.A.nyinyi ukabila unawateketeza.
 
Wanahifadhi lugha zao za asili na sio vibaya mwanasiasa akihutubia kwa lugha ya kikuyu
 
Mimi nasema UK ameona mbali kwamba kiswahili ndio silaha pekee ya kutuunganisha watu wa Afrika Mashariki, hasa Wakenya na Watanzania.
 
sikia wewe mkenya, afrika ya kusini na nigeria ukiacha kugha ya malkia, hawana lugha nyingine zaidi ya lugha zao za makabila. Ila nyinyi wakenya mnaweka mbele kiingereza na lugha zenu za makabila huku mkifanya kiswahili kuwa lugha ya tatu, so, msijilinganishe na wanigeria au S.A.nyinyi ukabila unawateketeza.[/QU English is a global language and I bet you've learnt it, hamna shida mtu kuzungumza kabila lake, shida ni ubaguzi kwa misingi ya kikabila, now, is that hard to understand?
 
very hard, kwanini mnatangaza kuwa kiswahili ni lugha ya taifa lenu wakati mnatumia english kama national language, huo ni unafiki na utumwa. Pili unapotumia lugha ya kabila lako kwenye public automatically huo ni ubaguzi wa kikabila, kumbuka lugha ndio inayounganisha watu kama sisi kiswahili kilivyotuunganisha.
 
Back
Top Bottom