Uhuru asema CJ Maraga atamtambua yeye ni nani, asema yeye ni rais

Uhuru asema CJ Maraga atamtambua yeye ni nani, asema yeye ni rais

Alichozungumza Uhuru kimechanganyika siasa na ukweli. Supreme court, hata kwa tusiojua sheria, imekwenda kwenye uamuzi wa mbele sana bila sababu. Kama tatizo lilikuwa kwenye ujumlishaji na utangazaji kwa nini haikutoa order ya recounting. Hiyo imewahi kufanyika pia USA. Mifumo ya kielektroniki iliwekwa pembeni na uhesabuji wa kura ulifanyika manually.

Naona hata baadhi ya wachumbuzi wa masuala ya mataifa haya makubwa wameelezea kushangazwa na kuitisha uchaguzi upya badala ya kuitisha uhesabuji wa kura upya. Mahakama yenyewe haijaeleza kama kulikuwa na tatizo katika upigaji kura. Imeeleza kulikuwa na tatizo kwenye mitatizo kwenye mitambo ya IT. Je, ikitokea tena ikaonekana IT systems zimefail au kuchezewa, wataitisha uchaguzi tena?

Kuitisha uchaguzi upya ni gharama kubwa, na inapowezekana kuepusha, inastahili kuepuka.
 
Kwa Tundu Lisu nani bora kati ya Pombe na Kenyata, Rais ambaye anatishia taasisi ambayo wewe ni mtaalamu halafu uko upande wake? shame on him....

Nadhani umesikia lakini hukuelewa.

Uhuru ameongea kuwa kuna tatizo kwenye mfumo wa sheria zao ambao unahitaji kufanyiwa marekebisho. Ni mfumo ambao unaruhusu mahakama kubadilisha maamuzi ya watu wengi kiurahisi. Na inaonekana hilo siyo tu kwenye suala la uchaguzi pekee lakini pia kwenye mambo mengine.

Sioni kama hicho ni kitisho. Ukizingatia hata kauli yenyewe imetolewa kisiasa.
 
Ukimsikiliza Rais uhuru unaona hata kuruhusu hiyo wenda aliogopa tu kupelekwa alikopelekwa kipindi iliyopita. Uhuru kaachia yake ya moyoni.

Hawa ndio viongozi wa Afrika ,wamelewa madaraka,nadhani sasa akina Lowassa na Chadema wameona hiyo demokrasia wanayoidai kwa kumuunga mkono Uhuru watakuwa wamezabwa kibao cha kerubu na huyo Uhuru,anahutubia utadhani katoka kulewa Uwanja wa Fisi Manzese,kama hakuiba na anajua atashinda mapovu yote ya nini,hawa jamaa wao ndio wakora
 
Hiyo ni edited speech,
watu wa NASA wame edit speech ya jamaa wakati ule akiwa kwenye kampeni
Na lengo lao ni kumuharibia na wanaweza wakamfanya chochote huyo jaji ili ionekane tu serikali imemuua na wapate huruma ya wananchi.
wanasiasa si wa kuwaamini sana.
Acha uongo wewe sote tumeona live kwenye TV ,uongo upi wewe ?2013 mahakama iliamua upande wa Uhuru hatukusikia hizo kelele,leo imeamua upande wa Raila tunasikia ujinga kutoka eti kwa raisi Uhuru,raisi gani anakuwa hafikiri kabla ya kutamka
 
WATU WENGINE HUMU MNAMPA UHURU MISIFA YA KIJINGA...UHURU NI CHUI ALIYEVALIA NGOZI YA KONDOO....
Teh teh teh, mkulu wenu ni fisi aliyevalia ngozi ya fisi! 😀 Afu anaendesha lorry kwa mwendo kama wa chui na kwa fujo mithili ya kifaru huku akitoa mipasho zaidi ya nyimbo za taarab! Mtajiju wenyewe! Yetu jicho tu! 😉
 
Kiukweli haya aliyoyasema Uhuru yanasikitisha, yanaogopesha na kutukumbusha mauaji mengi yaliyotokea na yanayoendelea nchini Kenya chini ya kivuli cha siasa ambayo hadi leo polisi hawajatoa majibu yoyote yale, kama vile ya wale mashahidi wa ICC ambao wengi waliuliwa, Jacob Juma aliyekuwa anaishambulia serikali, Msando aliyetaka kudhibiti kura zisivurugwe, viongozi wa dini kule Monbasa; Rogo, Makaburi, na Mmiliki wa Coast Modern bus ambaye serikali ilimtuhumu kufadhili ugaidi, na zaidi ya vijana 200 kule pwani waliokamatwa na polisi na kupotea chini ya uangalizi wa polisi.

Kenya inaongoza Afrika katika kipengele cha extra judicial killings kulingana na ripoti ya mwaka 2017 ya Transparency international, kwa kauli hizi za Uhuru na Rutta kwamba tukichaguliwa tena Jaji Muraga atakiona, au nasisi ipo siku yetu tutafanya tunachokijua, kweli ni jambo la kuogopesha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichozungumza Uhuru kimechanganyika siasa na ukweli. Supreme court, hata kwa tusiojua sheria, imekwenda kwenye uamuzi wa mbele sana bila sababu. Kama tatizo lilikuwa kwenye ujumlishaji na utangazaji kwa nini haikutoa order ya recounting. Hiyo imewahi kufanyika pia USA. Mifumo ya kielektroniki iliwekwa pembeni na uhesabuji wa kura ulifanyika manually.

Naona hata baadhi ya wachumbuzi wa masuala ya mataifa haya makubwa wameelezea kushangazwa na kuitisha uchaguzi upya badala ya kuitisha uhesabuji wa kura upya. Mahakama yenyewe haijaeleza kama kulikuwa na tatizo katika upigaji kura. Imeeleza kulikuwa na tatizo kwenye mitatizo kwenye mitambo ya IT. Je, ikitokea tena ikaonekana IT systems zimefail au kuchezewa, wataitisha uchaguzi tena?

Kuitisha uchaguzi upya ni gharama kubwa, na inapowezekana kuepusha, inastahili kuepuka.

Uko sahihi, lakini najaribu kujiuliza kama baadhi ya sababu za mapungufu ni fomu ambazo hazikusainiwa na pande zozote na pia nyingine kutoka kwenye vituo ambavyo havikuwepo (ghost stations?), sasa watakuwa wanahesabu nini kutokea humo au fomu za hivyo zitawekwa tu pembeni?

Gharama ya demokrasia ni kubwa...hali kadhalika kurudia uchaguzi....sijui pesa zinachotwa wapi tena kusapoti uchaguzi mpya..
 
Nadhani umesikia lakini hukuelewa.

Uhuru ameongea kuwa kuna tatizo kwenye mfumo wa sheria zao ambao unahitaji kufanyiwa marekebisho. Ni mfumo ambao unaruhusu mahakama kubadilisha maamuzi ya watu wengi kiurahisi. Na inaonekana hilo siyo tu kwenye suala la uchaguzi pekee lakini pia kwenye mambo mengine.

Sioni kama hicho ni kitisho. Ukizingatia hata kauli yenyewe imetolewa kisiasa.

Sharia zote zinamapungufu na kumbuka hawa wanakatiba brand new inayoendena vizuri sana na wakati, lakini kwa kukuwa imepiga kile Kenyata alivyotaka inamapungufu how is that?
kwa sababu zetu za kishabiki tumebaki na tafasri tunazotaka kusikia na kuona, tunaishi kwa kuongozwa na hisia zetu bila kureasons kwa kina.
 
Back
Top Bottom