Uhuru, haki na demokrasia katika Awamu ya Sita

Uhuru, haki na demokrasia katika Awamu ya Sita

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Awamu ya Tano ililaumiwa sana kuhusu kuminya Uhuru, Haki na Demokrasia. Katika kurejesha imani kuhusu "Haki", Rais wa Awamu ya Sita, Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akikemea watendaji wa Taasisi za kusimamia haki ili kuleta ufanisi. Matokeo yake kumekuwa na mabadiliko ya viongozi kwenye Taasisi hizo, km:

1) Mabadiliko katika Jeshi la Polisi ili wananchi watendewe haki inayostahili (kama kubambikiwa kesi na usumbufu barabarani).
Kumefanyika mabadiliko ya makamanda wa polisi wa mikoa, Usalama Barabarani, na Kurugenzi ya Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI).

2) Mabadaliko katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuharakisha kesi, kuondoa kesi zisizo na msingi na za kubambikiwa ili kuondokana na idadi kubwa ya kesi ambazo Serikali inashindwa.

3) Mabadiliko katika Ofisi ya Mashitaka (DPP) ili kupunguza/kuondoa ucheleweshaji, mlundikano wa mashauri Mahakamani na ubambikaji wa kesi.

4) Uteuzi wa Majaji ili kupunguza mlundikano wa mashauri Mahakamani.

Kwa kuwa Taasisi hizo za "Haki" zinategemeana, swali la kujiuliza Je, mabadiliko hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika utendaji wa Taasisi hizo?
 
Back
Top Bottom