Uchaguzi 2020 Uhuru, Haki na Maendeleo: Sera bora kabisa kuwahi kutokea

Uchaguzi 2020 Uhuru, Haki na Maendeleo: Sera bora kabisa kuwahi kutokea

Usisahau kuweka link ya Arusha kamanda [emoji16]
Tunataka tuone mabakuli yanavyotembezwa
Hata nchi hii ilitafuta Uhuru kwa kutembeza mabakuli, hata historia ya jinsi tulivyo pata Uhuru hujui, Bora ukae kimya kwa sababu tayari tusha fahamu upeo wako wa kufikiria jinsi ilivyo chini unahitaji kubustiwa.
 
Hata nchi hii ilitafuta Uhuru kwa kutembeza mabakuli, hata historia ya jinsi tulivyo pata Uhuru hujui, Bora ukae kimya kwa sababu tayari tusha fahamu upeo wako wa kufikiria jinsi ilivyo chini unahitaji kubustiwa.
Poaaa, basi msione aibu kurusha picha za mabakuli 😁 😁 ...
Zile 6bn michango ya wabunge yote amekula Mbowe 🙄
 
Hela waliopata maafa kagera ulipewa mgao .
Hapana kamanda, sikupata mgao kwa kuwa mimi sikuathirika na maafa 😁...
Wewe ulipata mgao wa 6bn kutoka kwa Mbowe ?
Usisahau link na picha za mabakuli kamanda😁😁😁
 
Uhuru wa kupora mali za nchi na kutolipa kodi. Ni aibu kukosa sera yaani hospital kibao zimejengwa, elimu bure

Bila miundo mbinu hizo bidhaa za kilimo zitafikaje sokoni.

Hebu tumieni akili
Ukiwa na fikra za kishetani unawaza kishetani shetani
 
Uhuru wa kupora mali za nchi na kutolipa kodi. Ni aibu kukosa sera yaani hospital kibao zimejengwa, elimu bure

Bila miundo mbinu hizo bidhaa za kilimo zitafikaje sokoni.

Hebu tumieni akili
Hospital bila dawa ni bure.
Tunauziwa hadi maji ya kutundikiwa. sijui wenyewe mnaita drip water
 
Lijuakali alielezea chama gani kinaiba kura
Kuna haja gani ya kuongoza chama kisichokubalika na wananchi?
Chama ambacho hakishindi bila kuiba kura.
Chama ambacho viongozi wake wanakiri hadharani kuwa ushindi wait unatokana na kuwatumia polisi na TISS.
Chama ambacho kinaitumia NEC kuwaengua wapinzani wake.
Hiki chama hakika Ni CHAMA CHA MASHETANI
 
Sela Bora kabisa hizi.

Jaman uku chama tawala kinatudanganya totally hasa uyu anae jiita rais wa wanyonge hafu ananunua mandege .
Wanyonge hatuna hela za kupanda ndege, wanyonge tunahitaji chakula Bora na mlo kamili , Wanyonge tunahitaji vitu gharama nafuu ili tuweze kuishi nyumba Bora.

Tuendelee kuelimishana ili kila mtu ajue kwamba Lissu atotua katika hayo kwa kuleta Sela Bora.
 
haki na uhuru unavovitaka hata hao walounda hiyo mifumo hawazifuati, marekani ndo wanajisifia kwa demokrasia bt angalia mambo ya hovyo wanayoyafanya, yaani police anaua mtu asie hatia bt kufunguliwa mashtaka mpaka watu waandamane na kushinikiza.

unataka serikali iangalie maendeleo ya mtu mmoja mmoja, je nani atakua tayari kupangiwa ratiba ya shughuli zake binafsi na serikali? huu mfumo ndo utaharibu haki maana serikali hawawezi deal na matamanio ya kila kitu bt watafanya kwa ujumla kitu ambacho wengine hawatakubaliana nacho.

hebu tuacheni ujinga wa kufuata mkumbo madam eti ni wapinzani, huo uhuru na haki unaoutaka jaribu kuuweka kwenye ngazi ya familia uone kama familia haitakushinda.

uhuru na haki lazima viendane na mazingira husika pia viwe na mipaka, hao mabeberu wanaotuhubiri huo uhuru na haki ndo wanaongoza kwa kuvikiuka na kufanya ukatili wa kila aina ajili ya maslahi yao, tuvishughulisheni sana vichwa vyetu kuwaza ili tuiepuke vita ya fikra ambayo tunapambana nayo bila kujua tena tukidhania ni haki
 
Hizi propaganda kadanganye wavivu wakufikiri.Kila mtu anaona nakujua mbivu na mbichi.
 
Hapana kamanda, sikupata mgao kwa kuwa mimi sikuathirika na maafa [emoji16]...
Wewe ulipata mgao wa 6bn kutoka kwa Mbowe ?
Usisahau link na picha za mabakuli kamanda[emoji16][emoji16][emoji16]
Uwezo wako wa kujenga hoja ndio huo.
 
Uhuru wa kupora mali za nchi na kutolipa kodi. Ni aibu kukosa sera yaani hospital kibao zimejengwa, elimu bure

Bila miundo mbinu hizo bidhaa za kilimo zitafikaje sokoni.

Hebu tumieni akili
*CCM WANAORODHESHA VITU BADALA YA KUTUPA MIPANGO* .

Mwenyekiti wa CCM ambae pia ndie mgombea urais wa Chama hicho pamoja na timu yake wameanza kampeni zao pale Dodoma na kwenye vyombo vya habari vya ndani. Kuanzia siku ya kwanza ambayo kiuhalisia ilikuwa ni Tamasha la Burudani wao wakalipa jina uzinduzi wa kampeni. Wameshindwa kutubainishia nini watafanya, kwa mipango na mikakati ipi.

Mwenyekiti na Timu yake ya kampeni hawatuelezi mipango ya ukusanyaji wa kodi watakayoitumia. Je, kodi zinazoenda kutozwa ni zilezile za kutufanya tuishi kama shetani? Sekta ya hifadhi ya jamii wameipangia mipango ipi? Je, bado tutaendelea kusubiri miaka 60 ili tupatiwe *FAO* letu la kujitoa? Anajenga majengo na kuyaita hospitali. Kama *"central"* tunaingia bure kutoka ni pesa. Huko kwenye hospitali kuna mipango ipi ya kutusaidia ili *MAITI* zetu zisikamatwe na kuzuiliwa?

Yapo mengi ya kujiuliza. Hizo barabara, madaraja, reli na vivuko tunajenga kwa kutumia wakandarasi wa nje au wa ndani? Je, "Value for money" imekaaje? Uwekezaji kutoka nje (foreign Direct Investment) umeshuka kwa 50% na TBL ambae ni mlipa kodi namba moja nae amepunguza kutoa kodi kwa 30%. Pesa zinatoka wapi za kugharamia hivyo VITU wanavyoorozesha. Je, mbona CCM haisemi kwa nini Deni la Taifa limeongezeka maradufu kwenye miaka 5 ya hapa kazi tu?

Rais ambae unapotaja maendeleo akilini kwake huja flyovers, madaraja, reli, na vipasua anga huyu hatufai. Rais ambae ukisema tunaboresha huduma ya afya kwake huja majengo na si huduma zitolewazo kupitia kwa wataalamu, vifaa tiba na madawa. Huyu hatufai.

RAIA wa China kila uchwao ndoto yao ni kwenda kuishi Ulaya na Marekani. Wanazamia kwa maelfu Ulaya na Marekani.Ukiwauliza kwa nini, wanakwambia wanahitaji maisha bora yenye kujali Utu, Haki na Uhuru. Hivi kwa ulimwengu wa sasa kuna nchi ina miundomsingi imara na ya kisasa kama uchina.

Tunamuhitaji Mh Tundu Antipas Lissu. *#NIYEYE* *2020*. Huyu anajibainisha kutupa SERA, mipango na mikakati iliyo maridhawa. Kipaumbele ni Haki, Uhuru na Maendeleo. Huyu ndie mbeba maono wa nyakati hizi. Tunahitaji maridhiano ya kutuleta pamoja chini ya Katiba Mpya ambayo itaridhiwa na wengi.

*Peter Ng'wandu*
*Furahini katika* *#YEYE2020*
*0717025818*
 
Wapo wajinga wanaodhani kuwa ubelgiji hakuna sheria za ukwepaji kodi,wanadhani ubelgiji hakuna magereza,mataifa yote duniani yanasheri na wapo wanaozilalamikia kwa sababu tu sheria zimeundwa ili zifuatwe sema ukishakuwa mwanasheria tena mwanaharakati na wakili wewe utasimamma kumtetea muuaji,jambazi,muhujumu bila kujali amefanya au hajafanya na anafanya hayo kwa malipo leo hii lissu awe mtetetzi wenu kweli watu wana akili.
Kipi kinazidi kingine,anayenyima haki zilizoainishwa katika Sheria ama anayetetea utekelezaji wa Sheria ilikupata haki
 
Kipi kinazidi kingine,anayenyima haki zilizoainishwa katika Sheria ama anayetetea utekelezaji wa Sheria ilikupata haki
Kwiyo unataka kuniambia sheria ya mazingira ya dunia iliyokuwa inatukataza kujenga bwawa la umeme rufiji ilikuwa inafaa ifuatwe,au sheria ya marekani iliyowapa nguvu polisi kuua mtu mweusi ni sahihi ifuatwe ni hivi sheria hutungwa kwa lengo zuri lakini si msaafu kwamba zikishindwa kutekelezeka kwamba zisifutwe lahasha zipo sheria ambazo kutokana na mazingira zimepitwa na wakati lakini zipo na hazisimamiwi ipasavyo kutokana na madhara yake kwa wakati uliopo.mfano:leo hii sheria ya usalama barabarani inataka kupigwa faini tsh 20000 baiskeli mbovu,je sheria hii inafanya kazi mtaani kwenu si inapuuzwa tu,ni kwa sababu imepitwa na wakati,huyu lisu anajua sheria lakini hata yeye anapotaka sheria isimamiwe sehemu nyingine kama za uchaguzi,dhamana na nyingine nyingi kwanini alalamikie sheria ya vyombo vya habari,au zile za uhujumu uchumi ni kwasababu kwake anaziona zinamtesa,we we na mimi tumeguswa?hivyo ili sheria iwe mbaya lazima ikuguse na hakuna sheria yoyote rafiki duniani bali kuna sheria nafuu tu,marekani wanasema wao wako huru vipi kuhusu mauaji ya weusi kila kukicha.
 
Sera bora ambayo haijawahi kutokea.

Mwanadamu yeyote yule anahitajika kuwa huru katika maamuzi, na hii ndio maana kamili ya utashi. Hongereni CHADEMA.
Haki kila mwanadamu yeyote yule anazo haki zake za msingi , ikiwa ni pamoja na tiba, elimu, kuishi, nk

Maendeleo, kila mwanadamu anahitaji maendeleo yake binafsi iwe ni katika kilimo, kazi, biashara, nk. Ukishawawezesha watu wako mmoja mmoja kupata maendeleo ndipo unakuja na maendeleo ya ujumla.

Watanzania ebu tuangalie tulikotoka na hali tuliyonayo tusirudie makosa. Kwa kauli mbiu ya hii ya CHADEMA, nawapa hongera.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

"Ukhanithi sasa basi". Maalim Seif.
 
Sera bora ambayo haijawahi kutokea.

Mwanadamu yeyote yule anahitajika kuwa huru katika maamuzi, na hii ndio maana kamili ya utashi. Hongereni CHADEMA.
Haki kila mwanadamu yeyote yule anazo haki zake za msingi , ikiwa ni pamoja na tiba, elimu, kuishi, nk

Maendeleo, kila mwanadamu anahitaji maendeleo yake binafsi iwe ni katika kilimo, kazi, biashara, nk. Ukishawawezesha watu wako mmoja mmoja kupata maendeleo ndipo unakuja na maendeleo ya ujumla.

Watanzania ebu tuangalie tulikotoka na hali tuliyonayo tusirudie makosa. Kwa kauli mbiu ya hii ya CHADEMA, nawapa hongera.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Maendeleo hayana chama. Tuwaunge mkono CDM.

Haupo muda sahihi wa kuleta mabadiliko kwa amani kuliko huu.
 
Back
Top Bottom