Uhuru Kenyata ni mwanademokrasia kama Obama

Uhuru Kenyata ni mwanademokrasia kama Obama

Uhuru ametoa povu balaa.
Anamtishia jaji [emoji23][emoji23][emoji23]
Urais mtamu aisee

Amini usiamini, ukihitimu shule ndio utaanza masomo.
kweli Uraisi mtamu bratha...
sio kwa povu lile
😀
 
Hayo ni maneno ya baadhi ya watu humu.

Kuwa eti kwa yeye kuacha watu waandamane bila kubugudhiwa basi ndo anakuwa mwanademokrasia kama rais Obama.

Bullshit.

Mwanademokrasia gani baada ya kesi dhidi ya ushindi wake kutokwenda vile ambavyo angependa yeye anaanza kumtolea vitisho jaji mkuu wa mahakama ya nchi?

Kama anajiamini na 'ushindi' aloupata kwa nini atoe vitisho kwa mahakama iliyoamua kuwa uchaguzi urudiwe?

Huyo Uhuru anachohofia ni nini hadi aanze kutoa vitisho kwa jaji mkuu?

Hivyo vitisho vyake vya kitoto vinachangia watu kuamini kuwa yule bwana Msando si ajabu aliuliwa na watu wa huyo Uhuru na pia kwamba Uhuru hakushinda kihalali bali alibebwa na figisu za tume ya uchaguzi ambayo ilikuwa inatumika kuhakikisha Uhuru 'anashinda'.

Mwanademokrasia wa kweli na anayejiamini hawezi kutoa vitisho juu ya mhimili mwingine wa serikali pamoja na kiongozi wake.

Huyo Uhuru si lolote na si chochote. Mnamwona ni mwanademokrasia tu pale ambapo labda maslahi yake hayapo hatarini. Yakiwa hatarini hana tofauti yoyote ile na akina Kagame na Museveni.

Hata siku moja sikuwahi kumsikia Obama akimtishia Chief Justice John Roberts.

Mimi naamini kabisa kuwa kama kweli uchaguzi wa Kenya utakuwa wa huru, haki, na wazi basi Raila atashinda.

Miaka yote hii wamekuwa wakimfanyia figisu. Mwaka 2007 ndo alishinda dhahiri kabisa na wakampora ushindi wake mchana kweupe bila hata aibu.

We umeona wapi jitu linaapishwa uani tena jioni karibu giza kuingia?

Hata 2013 naamini Odinga alifanyiwa figisu. Mwaka huu hata mahakama yao kuu imeliona hilo.

Sasa huyo Uhuru anaanza kuweweseka kwa sababu the jig might be up.

Vitisho vya nini kama ulishinda kihalali?

Vitisho vya nini kama unajiamini kuwa utashinda tena uchaguzi ukirudiwa?

So, no. He ain't no Barack Obama. He ain't no like Barack Obama.

Maybe more like Donald Trump who also has a penchant for railing against judges who don't rule in his favor.
Mkuu, bado Kenyatta ni mdemokrasi sana. Kwa viwango vya Afrika.

Tatizo unalinganisha na USA. USA hata wakati wa Bush kulikua na mapungufu. Hata wakati Trump vilevile. But wale wapo mbele yetu sana.

Hayana matupu impact kwenye utawala unaofuata sheria.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuwe wakweli tu siyo jambo jepesi hata tu kukubali uchaguzi urudiwe ni hatua.
Nakupa mifano miwili ambayo siyo toka Africa, Herode aliposikia kuna mtoto amezaliwa na wakatoa sifa kadhaa wale Wataalamu wa nyota(Mamajusi) nawalipo mpiga chenga akaona isiwe tabu akafyeka vitoto vyote vya umri kuanzia miaka 2 hadi 0 ktk eneo husika ingawa hakufanikiwa.
Watu wakaimba Sauli kaua maelfu na Daudi kaua makumi elfu, kauli hii ilitosha kuugeuza moyo wa mfalme Sauli nakutaka kufutilia mbali Daudi atoke kabisa kwenye uso wa dunia.
Hata ungekuwa wewe ndiyo Uhuru sidhani kama furaha yako baada ya ruling ya mahakama ingekuwa kama ya Odinga kikubwa kakubali kurudi ulingoni mambo mengine na risk nyingine kwenye siasa sidhani kama zinaepukika kirahisi hivyo.
Hata kwenye nchi kama USA kina Snowden wanaishi uhamishoni kwa kusema ukweli.
Haya yalikuwako na yatakuwako tu hata Uhuru akinyamaza ila chini ya Carpet jamaa lazima awe makini sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom