Inamuondolea sifa ukiwa na mtazamo chanya, lakini Afrika watu wenye sifa za ufisadi ndio hupendwa sana. Ilmradi jina lako linatajwa tajwa na kuanikwa kwenye vyombo vya habari, hiyo imetosha.
Japo pia hamna kiongozi msafi hapa Kenya, wote mafisadi lakini wana wafuasi ambao huwambii kitu, hebu leo rais Uhuru adiriki kumfuta huyo Ruto ndio utajua kisa kilichomfanya chui awe na madoadoa, kwanza huko kuthubutu ndiko kulimharibia Raila maana alipogombana na Ruto akaishia maisha ya kwenye gizani na baridi.
Leo hii huyo Ruto ndiye ngao ya rais Uhuru, kwa kweli nakiri kwamba isingekua Ruto, Raila angeingia ikulu tena asubuhi saa nne. Lakini Raila akiwa waziri mkuu kwa unafiki akajifanya kupigana na Ruto kisa ufisadi (ilhali Raila mwenyewe mfisadi mkuu na amezungukwa na mafisadi wakubwa), sasa alimfuta kazi na kumuondolea nje nje, Ruto akacheza high voltage politricks na leo yupo anakunywa chai ikulu kama naibu wa rais.
Ruto amekua anatumia raslimali za serikali kujiandalia mazingira ya kuingia ikulu kama rais kwenye uchaguzi ujao, amekusanya viongozi wake, hata gavana wa Nairobi bwana Mike Sonko ni kibaraka wake, aliwafadhili viongozi wengi sana hata mkoa wa kati ambao huko ni mfupa uliomshinda fisi. Nilishangaa sana juzi bibi yangu kijijini anasema bora afe kwenye foleni lakini lazima ampigie Ruto kura.
Jamaa ni mjanja sana kisiasa na hili nalisema bila kutetereka yeye ndiye atakua rais baada ya Uhuru, labda Mwenyezi Mungu amchukue, lakini kama bado yupo hapa, hatuna jinsi, bora tujiandae tu kwa urais wake. Japo ni mzuri kiutendaji lakini mfisadi vibaya sana, yeye hunyakua bila kujali chochote, yeyote, au lolote.