Uhuru Kenyatta achagua baraza jipya la mawaziri

Huyu akiwa rais kuna watu wataumia sana. Maana anawechekea hao watu usoni tu kwa sababu kuna kitu anakitaka.

Jamaa amejijenga sana na anaendelea kukua kadiri anavyopigwa, ni mara nyingi sana ametabiriwa kuanguka lakini leo hii ndiye hukaimu urais na kuwa amiri jeshi mkuu kila wakati Uhuru akiondoka nje ya nchi.

Kumbuka sasa dola iko mikononi mwake ili afanye maandalizi ya kuandaa mazingira yake mwenyewe.
 
Jina la Ruto kila mahali ni ishara yake kuwa Rais wa KENYA come 2022.
Mount Kenya hawataki kusikia jina la Ruto this time Raila Odinga ataungana na Gideon Moi kuhakikisha Ruto hapasui
 
Wakenya endapo watamchagua Ruto itakuwa siyo poa, kwa muda Ruto aliohudumu unatosha, ni muda wa mtu mwingine fresh kuonyesha yale anayoweza kufanya, Kenya ina watu wengi wanaoweza kuongoza vizuri.
 
Wakenya endapo watamchagua Ruto itakuwa siyo poa, kwa muda Ruto aliohudumu unatosha, ni muda wa mtu mwingine fresh kuonyesha yale anayoweza kufanya, Kenya ina watu wengi wanaoweza kuongoza vizuri.

Ruto hajatawala ila amekua naibu, katiba haijamzuia.
Ni vigumu sana kumzuia huyo jamaa kuwa rais, mwenyewe amejijenga kisiasa hadi hapo, amejiandaa na kujijengea mazingira.
Viongozi wengi waliochaguliwa leo hii yeye ndiye kawafadhili halafu ni presidential material maana kwa kweli ukimskliza kwenye mahojiano, jamaa hudhihirishaa uelewa wa hali ya juu na udhabiti kisiasa, tatizo lake moja tu, ni mfisadi mpaka basi.
 
Hahaha. If this is true then it is very interesting
 

Sawa ila kuna watu watalia maana huyu ana roho ya kimaskini sana si kama Uhuru.
 
Mount Kenya hawataki kusikia jina la Ruto this time Raila Odinga ataungana na Gideon Moi kuhakikisha Ruto hapasui
Mimi ni Mtu wa Mt. Kenya na slogan ni "Gûcokia guoko" yani to return the favour come 2022 to WSR hizo porojo zingine sijui umeokota wapi.
 

Hapo kwenye red ndio inamwondolea sifa ya kuwa Rais wenu. Ufisadi umegharimu sana maisha ya watu katika nchi za Afrika.
 
Hapo kwenye red ndio inamwondolea sifa ya kuwa Rais wenu. Ufisadi umegharimu sana maisha ya watu katika nchi za Afrika.

Inamuondolea sifa ukiwa na mtazamo chanya, lakini Afrika watu wenye sifa za ufisadi ndio hupendwa sana. Ilmradi jina lako linatajwa tajwa na kuanikwa kwenye vyombo vya habari, hiyo imetosha.
Japo pia hamna kiongozi msafi hapa Kenya, wote mafisadi lakini wana wafuasi ambao huwambii kitu, hebu leo rais Uhuru adiriki kumfuta huyo Ruto ndio utajua kisa kilichomfanya chui awe na madoadoa, kwanza huko kuthubutu ndiko kulimharibia Raila maana alipogombana na Ruto akaishia maisha ya kwenye gizani na baridi.

Leo hii huyo Ruto ndiye ngao ya rais Uhuru, kwa kweli nakiri kwamba isingekua Ruto, Raila angeingia ikulu tena asubuhi saa nne. Lakini Raila akiwa waziri mkuu kwa unafiki akajifanya kupigana na Ruto kisa ufisadi (ilhali Raila mwenyewe mfisadi mkuu na amezungukwa na mafisadi wakubwa), sasa alimfuta kazi na kumuondolea nje nje, Ruto akacheza high voltage politricks na leo yupo anakunywa chai ikulu kama naibu wa rais.

Ruto amekua anatumia raslimali za serikali kujiandalia mazingira ya kuingia ikulu kama rais kwenye uchaguzi ujao, amekusanya viongozi wake, hata gavana wa Nairobi bwana Mike Sonko ni kibaraka wake, aliwafadhili viongozi wengi sana hata mkoa wa kati ambao huko ni mfupa uliomshinda fisi. Nilishangaa sana juzi bibi yangu kijijini anasema bora afe kwenye foleni lakini lazima ampigie Ruto kura.

Jamaa ni mjanja sana kisiasa na hili nalisema bila kutetereka yeye ndiye atakua rais baada ya Uhuru, labda Mwenyezi Mungu amchukue, lakini kama bado yupo hapa, hatuna jinsi, bora tujiandae tu kwa urais wake. Japo ni mzuri kiutendaji lakini mfisadi vibaya sana, yeye hunyakua bila kujali chochote, yeyote, au lolote.
 
What happened to Prof. alipotaka kugombea urais?
 


Mkuu MK254 maelezo yako ni ya kina sana na yamejitosheleza. Sikujua kama Ruto ana nguvu iliyojichimbia chini namna hii. Kwa jinsi ulivyoweka maelezo yako naona hakuna wa kumzuia, mjiandae tu kisaikolojia kuwa yeye ni Rais wenu hapo 2022.
 
What happened to Prof. alipotaka kugombea urais?

Hivi huwa sielewi kwanini Watanzania hudai Prof. Saitoti aliuawa kwa ajili ya kugombea urais, yule hakua na ushawishi wowote kiasi cha kufuatwa.
 
Kenyatta hawezi hilo, Kenya huwa pagumu sana kutawala kimabavu, leo hata urais wa Kenyatta haujatulia maana Odinga anamchokonoa sana.
Mimi napenda sana siasa ya Kenya 2022 kuna possibility kubwa NASA na KANU wakaungana kama Jubilee watamsimamisha Ruto. Kura za Rift valley itagawanyika mara 2 hapo ndipo uwezekano wa Ruto kuwa Rais utakufa
 
Hivi huwa sielewi kwanini Watanzania hudai Prof. Saitoti aliuawa kwa ajili ya kugombea urais, yule hakua na ushawishi wowote kiasi cha kufuatwa.
Saitoti alikuwa anataka kugombea urais ama kumuunga mkono Raila na kwasababu alikuwa very powerful than Uhuru Kenyatta ilikuwa hakuna njia nyingine lazima afanyiwe mambo yaleeee.
 
Huyu akiwa rais kuna watu wataumia sana. Maana anawechekea hao watu usoni tu kwa sababu kuna kitu anakitaka.
For last 20 years kutoka kuwa muuza kuku mpaka kuwa one of the richest person in Kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…