Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uhuru alikwenda Shule kusoma sio kuvunja madirisha.Mahakama ya Juu nchini Kenya imetoa hukumu kwamba Uhuru Kenyatta wa Jubilee hakushinda kihalali na hivyo kukubaliana na madai ya Raila Odinga kwamba uchaguzi mkuu nchini humo haukuendeshwa ipasavyo.
Lengo langu hapa sio kuongelea mwenendo na maamuzi ya mahakama hiyo, ila ni kuongelea namna Uhuru Kenyatta alivyopokea maamuzi hayo; kuheshimu uhuru wa mahakama na utawala wa sheria; na wito wake kwa wakenya kwamba wadumishe amani, wao ni wakenya.
Huyu kiongozi ameonesha ni kwa jinsi gani anavyochukia utengano, ubaguzi, chuki, na uhasama miongoni mwa raia wa nchi yake. Hotuba yake imewakumbusha na kuwasisisitiza wakenya kwamba wao ni wa moja hata kama wanatofautiana kisiasa, kikabila na rangi. Wao wanabaki kuwa wakenya.
Kiongozi huyu hata kama hajaomba tumwombee, wapenda haki kote Afrika ya Mashariki na Afrika kwa jumla, tumwombee. Mungu wa mbinguni, aliyeumba mbingu na nchi azidi kumjalia hekima na busara, upendo na umoja.
Tufunge hata siku tatu pasipo kula wala kunywa tumlilie Mungu wa mbinguni ampe hekima. Huyu ni aina ya viongozi ambao wakiomba taifa liwaombee wanastahili kuombewa. Sio hawa wengine wa Angalo wanafiki wanaomba waombewe huku wakijenga chuki na kuchukiana; ubaguzi wa kidini na kikabila; kikanda na kisiasa ndani ya nchi zao. Wanaojijengea himaya ya kutoguswa. Huku wakibana ajira na kuongeza umasikini katika mataifa yao.
Uhuru Kenyatta aombewe na Mungu aipatie Afruika kina Uhuru Kenyatta wengine watawale Afrika Mashariki kote.
Mungu Ibariki Kenya, wakenya na viongozi wao.
Mungu ibariki Afrika
Ha ha ha. Wewe kijana acha utani. Haya faidi ugali wako kwa shemeji.