Uhuru Kenyatta anza maandalizi ya uchaguzi wa duru la pili

Uhuru Kenyatta anza maandalizi ya uchaguzi wa duru la pili

KOMBAJR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
5,827
Reaction score
1,271
katika kile kinachooneka kuanza kukimbia kivuli chake na kutokuwa na uhakika wa ushindi wake baada ya muungano wa coard kuwasilisha ushahidi mzito kuhusu uchakachuaji wa uchaguzi wa kenya ambao ulipelekea tume ya uchaguzi kumtangaza uhuru kuwa rais.umeingia katika sura nyingine baada ya muungano wa jubilee kuungana na muungano wa amani ukiongozwa na mudavadi pamoja na wagombea wengine kutoka katika vyama vingine hii ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa duru ya pili.
Mytake.
Kama uhuru na muungano wa jubilee wanajiamini kuwa ushindi wa 50 + 1 ulikuwa halali kwanini wanaanya bumps?
1. Kama mahakama itabatilisha matokeo je uhuru bado atakuwa na sifa za kuwa mgombea?na vipi tume iliyoshiriki katika uchakachuaji bado itakuwa na sifa ya kuitwa tume?
2. Vipi wale waliotuma salaam chap chap watawithdraw salam zao?
Hili liwe somo pia kwetu katika uchaguzi ujao.
Jpili njema wanajf
 
Hiyo mytake imefanya nigundue na wewe ni mmoja wa vilaza wazuri tu
 
Kama watamuita kinana tena atashinda tena zaidi ya asilimia 80
 
Siasa bana! Raila n musokya wamekuwa wapinzani sasa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mi nimeipenda, kama hakukua na haki...basi uchaguzi urudiwe demokrasia na haki sawa lazima vizingatiwe - na hapa ndio nauona upinzani wenye manufaa
 
mi nimeipenda, kama hakukua na haki...basi uchaguzi urudiwe demokrasia na haki sawa lazima vizingatiwe - na hapa ndio nauona upinzani wenye manufaa

100 mama d hilo kwetu ni somo kuwa haitoshi tu kuwa na katiba mpya na tume ya uchaguzi bali kuwa na mahaka huru ambayo itatoa haki na usawa bila kuyumbishwa kwa faida ya watu wachache
 
Kwa taarifa yako, Uhuru aliwakaribisha vyama vyote kuunda Serikali, hivyo sio kama anajiandaa kwa uchaguzi mingine bari hakua na uchu wa madaraka. Kwa kesi iliyowakilishwa Mahakamani kwa CORD kushinda itakua ni vigumu sana kwa Maana wao wanataka matokeo yangekua Tallied kwa Computa kama Sheria ya uchaguzi ilivyotaka, lakini wamesahau kua ni lazima uanze kwa mkono ndipo ufanye electronic, mengine ni madogo madogo sana.
 
Tutumie lugha ya heshima na busara. Kumuita mtu kilaza kwasababu tu kaandika yasiyokufurahisha au mnatofautiana mtizamo si vizuri na si sahihi. Hoja ipingwe kwa hoja si matuzi. Kama Raila anavyopinga ushindi wa Uhuru kwa kufuata sheria nasi tuwapinge tunaotofautiana nao kwa hoja. Ustaarabu wa mtu hupimwa kwa hoja zake si kwa matusi yake. Wakati mwingine nashangaa kuona vijana tuliowafundisha vyuo vikuundo hawatoi hoja za kuwapambanua na wale wenye elimu ndogo badala yake ndo wanakuwa wajuvi wa matusi. Kwa kweli sipendezwi na hii tabia ya kutukana watu eti kwasababu chama chetu si chao, mtizamo wao so wetu etc.
 
Uhuruto wamemzidi RAO kura zaidi ya laki 6 na huyu mudavadi amepata kura laki 4 sasa hata kama angemwacha RAO aungane na RAO bado wamgemshinda tu, UHURU anaunda serikali yenye nguvu ndo maana anatafuta watu wenye uwezi maana sio siri Mudavadi ni kiongozi mzuri sana ndo maana hata yeye Uhuru alishashawishika Mudavadi achukue urais yeye awe msaidizi...ila tungonje Supleme court watasemaje!! Jpili njema
 
Nakuunga mkono mabaghee kuna watu hapa wana tabia za kijinga sana.
 
Uhuruto wamemzidi RAO kura zaidi ya laki 6 na huyu mudavadi amepata kura laki 4 sasa hata kama angemwacha RAO aungane na RAO bado wamgemshinda tu, UHURU anaunda serikali yenye nguvu ndo maana anatafuta watu wenye uwezi maana sio siri Mudavadi ni kiongozi mzuri sana ndo maana hata yeye Uhuru alishashawishika Mudavadi achukue urais yeye awe msaidizi...ila tungonje Supleme court watasemaje!! Jpili njema

Supreme
 
mi nimeipenda, kama hakukua na haki...basi uchaguzi urudiwe demokrasia na haki sawa lazima vizingatiwe - na hapa ndio nauona upinzani wenye manufaa

uchaguzi ukirudiwa lazima wahusika wa tume walioharibu huo uchaguzi wafikishwe mahakamani, sababu wanaingiza nchi kwenye garama kubwa za kurudia uchaguzi na kupotezea watu muda wao.

itakuwa fundisho kwa chaguzi zijazo, ila tukifunika kombe ili mwanaharamu apite kodi za wananchi zitazidi kupotea sababu ya watu wachache
 
Mkuu Likwanda
Kama ukiendelea kusoma submission za RAO Kuna kitu cha msingi hapo,mismatch ya waliojiandikisha ni ziada 85,000. na idadi hiyo imetokea ndani ya siku 30 kabla ya kupiga kura ktk. Kipindi hicho daftari halitakiwi kufanyiwa marekebisho yoyote,daftari la upigaji kura ndio rejeo la mwisho lenye mamlaka, sasa limechezewa credibility haipo.
 
Back
Top Bottom