Uhuru Kenyatta hana mfano Afrika kwa demokrasia

interconsult

Senior Member
Joined
Dec 8, 2017
Posts
112
Reaction score
154
Wakati waliowengi walitegemea machafuko makubwa Jana Kenya kwa kitendo cha UHAINI kwa RAILA ODINGA kujiapisha,ukweli ukawa tofauti. Jana mpk saa 5 asbh vikosi vya dola vilijiweka kivita na kishali kuakikisha UHURU PARK hakai wala hafiki mtu.

Mh. Uhuru Kenyata, kaka mpenda demokrasia, aliamulu vikosi vyote vya dola kuondoka na kuacha UWANJA huo huru ili wapenzi na wafuasi wa ODINGA wakae wafanye watakayo ili wapunguze hasira zao. Mpk hivi hakuna hata aliyejikwaa kidole. JE INGEKUWA HAPA hali ingekuwaje.

JE TUNAJIFUNZA NINI. Na madikteta wetu wa afrika mashariki wanajifunza nini kutoka kwa RAIS KIJANA KABISA NA HANDSOME KULIKO WOTE AFRIKA MASHARIKI.
 
Kwa kilichotokea Kenya Uhuru Kenyata anastahiri pongezi kwa ukomavu aliouonesha,ni mwanasiasa wa mfano Africa.Hapa kwetu ilitangazwa oparesheni "UKUTA" tukashuhudia barabara za nchi nzima zikigeuzwa viwanja vya mazoezi ya kivita kwa askari kufurika barabarani wakiwa na siraha za kivita wakifanya mazoezi ya kujiandaa kuua raia wasio na hatia!

Hongera Uhuru Kenyatta.

https://www.jamiiforums.com/attachments/1472313226634-jpg.388760/
 
Jambo umeongeza na mahaba niuwe, ila binafsi nimeona kenya inazidi kuwa mfano wa kuigwa duniani ,

Kitendo alichokifanya Mh Raila Odinga jana kama angefanya kwa nchi nyingine hasa nchi Fulani hivi basi hiyo tafrani mitaani isingekuwa ya kawaida, ila hii imeonyesha kuwa demokrasiaimeeleweka vyakutosha nchini kenya,

Hongera kwa kenyatta kuimarisha usalama wa wakenya na taifa kwa ujumla,
 
Nafkiri mtoa mda umesahau kitu kikubwa sana:

Uhuru Kenyata, aliponea chupuchupu kufungwa na ICC miaka michache iliyopita kwa sababu hiohio ya ukatili ma mauaji ya kisiasa na kikabila.

Kwa sasa amefungwa mikono, akitumia nguvu tena arudishwa ICC this time for good.

Nadhani sasa umeelewa kwanini anaogopa kufanya kilichotarawajiwa na wengi...
 
yaani angethubutu kuleta ubabe sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine!!ye mwenyewe alishaona umati ule unautawanyisha vp??ndo maana jamaa akawa mpole tu!
mtihani mwingine kwa Uhuru akijaribu kumkamata bwana odinga kwa kosa la uhaini!!atakuwa kafanya kosa kubwa sana kwa maana wale wafuasi wa odinga nilivyowaona si watu wazuri wale hata kidogo!!
 
Tumejifunza sometimes turuhusu uhaini.
 
Kwa upande mwingine africa ilivyo pia ni kosa kumuacha mtu ajenge hisia kwenye mioyo ya watu likija kuibuka baya ni vigumu kubadirisha kile mtu aliaminishwa.
 
Demokrasia ni uwanja mpana sana mbona TV stations zilzimwa zote ili sisionyeshe hilo tukio?
 
Kwa kweli anastahili kupongezwa....kwa average african country jana ilikuwa ni siku ua mauaji in the name public order/disorder.....ukweli ni kwamba tukio la jana halimpungizii Kenyetta Urais wake kwa namna yeyote big up.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…