Maisha[hariri | hariri chanzo]
Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]
Alizaliwa kama
mwana wa kwanza wa
Jomo Kenyatta aliyekuwa rais wa kwanza wa Kenya na
mke wake Ngina Muhoho aliyeitwa Mama Ngina.
Baada ya kumaliza masomo, alishughulikia hasa
biashara za
familia alizorithi kutoka kwa baba yake.
Kuingia katika siasa[hariri | hariri chanzo]
Mwaka 1997 alijaribu kuingia mara ya kwanza katika
siasa lakini alishindwa katika
uchaguzi wa
bunge.
Mwaka
1999 rais
Daniel arap Moi alimpa
cheo cha
mwenyekiti wa
bodi ya
utalii. Moi aliendelea kumpandisha ngazi kwa kumpa nafasi ya
mbunge wa kitaifa na
waziri msaidizi.
Mwaka
2002 akawa makamu wa mwenyekiti wa
KANU.
Mgombea wa urais 2002[hariri | hariri chanzo]
Tangu Julai 2002 ilionekana wazi ya kwamba Moi alimtaka kama mgombea wa urais upande wa KANU atakayemfuata katika
ikulu.
Mkutano mkuu wa KANU katika mwezi Oktoba 2002 uliitikia mapenzi ya rais ukamtangaza Uhuru kama mgombea wa urais.
Tendo hili lilisikitisha wanasiasa wengi wasiokuwa
Wakikuyu na waliotegemea nafasi hiyo kwa ajili yao wenyewe. Waliondoka katika KANU na kuendelea katika ushirikiano wa
upinzani wa
NARC.
Uhuru ulishindwa katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 alipopata
asilimia 31 tu za
kura.
Kiongozi wa upinzani na wa chama[hariri | hariri chanzo]
Katika bunge jipya alikuwa
kiongozi wa upinzani, lakini aliona pia upinzani ndani ya
chama hasa kutoka kwa
Nicholas Biwott pamoja na wanasiasa kutoka
Bonde la Ufa. Kwenye mkutano wa chama cha Januari
2005 Uhuru alithibitishwa kwa kura nyingi na Biwott aliunda chama cha
New Kanu.
Pingamizi dhidi yake ndani ya KANU[hariri | hariri chanzo]
Katika kura maalumu ya wananchi kuhusu
katiba Uhuru alishikamana na viongozi wa
LDP katika kambi ya
Chungwa. Mipango yake ya kushiriki katika
Orange Democratic Movement (
ODM) yalipingwa vikali ndani ya chama kwa sababu wanaKANU pamoja na rais mstaafu Moi waliogopa kupotea kwa chama cha kwanza katika
historia ya Kenya.
Katika Novemba
2006 Biwott alirudia jaribio la kumpindua Uhuru kwa kuita mkutano wa Kanu
mjini Mombasa bila idhini ya mwenyekiti wala
kamati ya chama. Hapo alichaguliwa kuwa mweyekiti mpya. Kwa msaada wa serikali Biwott alifaulu kuandikisha kamati yake kama
uongozi rasmi, na hivyo kumwondoa Uhuru katika nafasi ya kiongozi wa upinzani bungeni.
Uhuru alipinga uamuzi huo, na hatimaye
mahakama kuu ikabatilisha kura ya Mombasa tarehe
29 Desemba 2006 ikathibitisha azimio hili mnamo Juni
2007.
Kuhamia upande wa Kibaki 2007[hariri | hariri chanzo]
Juni 2007 Uhuru alionyesha wazi ya kwamba alitaka kuacha ushirikiano na ODM kwa kutopeleka
jina lake kati ya wagombea wa urais upande wa ODM. Badala yake alieleza ya kuwa atampigania rais Kibaki achaguliwe tena.
Katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 Uhuru alichaguliwa tena kama mbunge w