Uhuru Kenyatta: Serikali nyingi Afrika zinajiendesha kwa kukomoa matajiri

hayo ni majungu. na wewe si ukafanye hivyo kama unaona ukifanya hivo unakuwa tajiri. Acheni vivu wa kike. Huwezi kufanya maisha ya maskini kuwa nafuu kwa kuwashusha chini waliokuwa juu.
Hakuna anaeshusha matajiri chini Isipokuwa Wao Wanafundishwa tu kufata sheria ndio unaona kama wanashuka, Utajiri wao hauna Faida kama wanakwepa Kodi na kutoa Rushwa
 
Hao ndio wakwepaji kodi wakubwa hapa nchini nimefanya kazi hapo kwa mda mfupi ilikua field... Sema wanauma na kupuliza... Kwa m
Sasa huko unajua wewe, ila kwasababu hajakamatwa na kuthibitika, hatuwezi kuishi kwa kunyoosheana vidole vya husda, akikamatwa kama Lugumi na Majembe Auction, pia atashughulikiwa.
 
Sasa ulitegemea Bilionea asemeje? Of course hataki kulipa kodi ili andelee kuwa Bilionea na wewe ubakie kapuku na kumpigia makofi ikifika siku ya uchaguzi unaamka saa kumi alfajiri kujipanga foleni kumpigia kura, kama unavyofanya, too stupid!
Hahahahahahaaa, safi sana, mtu familia yake inamiliki mashamba yote ya wakoloni, unategemea aseme nini kuhusu matajiri..
 
Unajua story ya utajiri wa familia ya Kenya, isome kwanza uielewe walivyonyonya ndo ujibu hivyo...anzia na umiliki wao wa mashamba ya waxungu...
 
Safi sana mkuu...asiyejua utajiri wa hii familia ndo anaweza kutetea aliyoyasema
 
Tunaanza na wale waliothibitika kwanza, nchi haziendeshwi kwa mawazo ya kishirikina, huko tulishapita zamani sana, hawa waliothibitika kutwaa ardhi ya wananchi kwanini mnapepesa macho?
 
Ipo siku atakuja rais mwingine na kubadilisha sheria ya ardhi ns kuwataka waeleze waliipataje, muda utaongea tu. Haya majivuno na huu utajiri wa kunyakua ardhi una mwisho wake
 
Tunaanza na wale waliothibitika kwanza, nchi haziendeshwi kwa mawazo ya kishirikina, huko tulishapita zamani sana, hawa waliothibitika kutwaa ardhi ya wananchi kwanini mnapepesa macho?
Mimi pia siamini ktk ushirikina ila chukulia alibino amekufaa, Mkuu
 
Ndo tatizo la kuchagua rais masikini, lazima tu atake waliokuwa wakimzidi wawe masikini
Tatizo la kuchagua rais tajiri ni , njaa, watu kulaka kwenye slums, walio wengi kukosa ajira na pengo la masikini na tajiri kuongezeka
 
Mimi pia siamini ktk ushirikina ila chukulia alibino amekufaa, Mkuu
Albino waliuliwa na watu katili, wengi walikamatwa na kuukumiwa kifo, sababu ya mauaji ya albino inajulikana, ila serikali ilijitahidi kulimalizo hilo tatizo kama ilivyokuwa Kibiti, kwanini wakenya wanashindwa kumshughulikia Kenyatta na majambazi wengine waliotwaa ardhi yao kwa nguvu?
 
....Tanzania tuna mapori ya kumwaga,hata ukitaka ekari moja kwa laki mbili unapata, mbona watu hawatajiriki? Tukubali tuu kwamba kuwa tajiri si lelemama...hujaona humu ndani mtu anakwambia nina milioni kumi mifanye biashara gani? Wakati kuna mtu anakopa benki milioni moja na anaanza biashara
 
Tatizo lako unadhani kukaa porini ndio kuwa tajiri. Issue ni kunyakua ardhi za watu walizoziendeleza na zipo katika mazingira mazuri.

Kufyeka pori pekee yako siyo jambo rahisi. Kitu walichokifanya ni kunyang'anya mashamba ya watu waliokuwa nayo na kuhodhi.
 
Unasema tunamapori ya kumwaga kwasababu Nyerere hakuruhusu wazungu na yeye mwenyewe kujimilikisha, angefanya kama Jommo Kenyatta alivyofanya, usingeikuta hiyo ardhi, kumbuka biggest factor of production ni land, sisi watanzania kama unataka kuzalisha mali, husumbuki kupata land, mamilioni ya watanzania leo huu wanaendesha maisha yao vizuri sana kwa shughuli za kilimo, ufugaji, uchimbaji madini na biashara nyingi tu, popote pale nchini bila kujali kwamba ni mwenyeji wa eneo hilo au hapana, sio lazima watu wawe matajiri, hata nchi zilizoendelea matajiri ni wachache lakini karibu watu wote wanaishi maisha mazuri, sasa kama mtu anayopesa kama hiyo uliyosema, na ardhi ipo, na bado anauliza afanye biashara gani, basi huyo upungufu wake ni elimu ya ujasiriamali, usilaumu nchi.
 
....Hoja yangu ni kwamba issue siyo tuu kuwa na ardhi kama ulivyotanabahisha, na pia utajiri haupatikani kama kutungua maembe...wewe unaweza pewa milioni mia but kama huna creativity zitaisha tuu na ubaki kulia lia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…