Vita dhidi ya ufisadi ni vichafu na lazima rais Uhuru awe tayari kwa jina lake kutumika kama kinga kwa baadhi ya hawa, wataliburuza na kulitia tope, sasa yeye atumie busara na kufanya yake kimya kimya, akianza kuwajibu atakua anatimiza wanachokitaka.
DCI endelea vivyo hivyo, kaza mkanda, pambana na usiachie, mbele kuna mawimbi na misukosuko ya kila aina, lakini upo upande ufaao kihistoria, wajukuu wetu watasoma kukuhusu.