Uhuru Kenyatta wewe ndiye mshindi

Mahakama ilisema wazi 3rd respondent(Uhuru) hana hatia yoyote na ni wazi alishinda ila iebc haikuandaa uchaguzi kwa kuzingatia katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
That's the polite way to say you are a criminal, tried and proven the process was rigged and fraud which favored Uhuru that's why they did what they did.

We are defer in interpretation
 
Hii ni kwa wale wanaomuelewa Uhuru Kenyatta vizuri na wale wasio na chuki za kipuuzi! Wala msiwe na shaka, tarehe 17 Oktoba, usubuhi usubuhi tunampa Uhuru Kenyatta zake tano tena kama tulivofanya tu chee ya Agosti 8! Hiyo siku itafika tu, Inshaalah!
 

Kwa uhakika Uhuru anachukuwa Urais kwa sababu hajaua binadamu yeyote lakini upande wa upinzani baada ya matokeo ya urais kutangazwa waliandamana katika ngome zao Mathare na Nyanza wakafa wengi lakini koti ilipofuta matokeo Uhuru kasema peace peace peace, amani hakuna tone la damu mpaka leo kwa hiyo Uhuru ni mteule wa Mungu kwa sababu Vox Populi Vox Dei!!!! Kwanini majaji hawakusema kura ziesabiwe katika kila kituo kwa kufungua masanduku yaliyofungwa kwa lakiri!! badala ya kupoteza pesa ya Wakenya kwa kurudia kura over 12 billion shilings za Kenya, kwa hesabu ya Tz ni 240 billion shs.
 
Mimi sioni kwanini Uhuru hapa anasifiwa, kama ni sifq ziende kwa wananchi wa Kenya ambao walipigana kwa muda mrefu kudai katiba yenye wigo mpana wa demokrasia, na msidhani ilipatikana kiurahisi, sio kweli, Raila huyo mnaemuona, alifungwa miaka 10 na mzee Moi kwa kudai uhuru wa kidemokrasia, na watu wengi walipoteza maisha chini ya utawala kandamizi wa Moi.

Wakenya walipochinjana mwaka 2007, Kenya ikawa njia panda, mtakumbuka Dunia nzima ilielekeza nguvu Kenya ili kuleta usuluhisha na maridhiano ya kudumu, moja ya makubaliano ni kuwa na katiba mpya, hii ambayo leo hii imemfunga rais wa Kenya asiwe na nguvu nyingi kisheria, hata ya kukemea rushwa, wala kusema lolote lile, kila kitu kimewekewa mipaka na katiba, kwa hiyo kushindwa kwa Uhuru kufanya lolote na kubaki kukubaliana na kila jambo, sio kwa mapenzi yake ni katiba yao inamlazimisha, na katiba hiyo sio kwamba viongozi wa Kenya waliipenda iwanyime uhuru wa madaraka, ni baada ya mkwamo uliotokea baada ya watu kuchinjwa 2007.

Huku Tanzania katiba iliyopo inampa madaraka makubwa rais, ndiyo mchakato huo wa kuipata katiba uekwama, watu huku Tanzania hawapo tayari kufungwa kama alivyofungwa Raila kudai demokrasia zaidi, au hata kumwaga damu kama walivyofanya wakenya, wanabaki kupiga kelele isiyoambatana na vitendo.

Anyway kwa kifupi, kilichofanyika Kenya, Uhuru hastaili pongezi kwa sababu amefuata katiba ya Kenya kama inavyotaka na sio kwamba yeye mwenyewe amelifanya kwa jitihada zake, na kiukweli yeye Uhuru ameonyesha kutopenda demokrasia hata kidogo kwa kutoa vitusho kwa jaji mkuu kinyume na katiba ya Kenya inayosema mahakama iachwe ifanye kazi yake bila vitisho vyovyote.

Kama nipongezi wanastahili wakenya kwa kupambana hadi kupata Katiba bora na kuilinda ili kuhakikisha haichezewi. Ila niwaombe wakenya wote kwa ujumla, kama katiba yenu inafanya vizuri katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kisiasa, kwa nini msiitumie kuwapatia ufumbuzi katika matatizo ya kiuchumi na kijamii, kama vile rushwa, ukabila, tofauti ya kipato kati ya matajiri na masikini, umilikaji wa ardhi na mauaji ya kiholela yanayofanywa na vyombo vya dola?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa Raila unayemsifu ati alileta uhuru wa demokrasia ndiye pia anataka maafisa wa IEBC watolewe kiholela bila kufuata katiba,ndiye huyo pia hataki taasisi ziwachwe kufanya kazi bila kuingliwa kisiasa.Odinga ndiye huyo pia akiitwa kutoa ushahidi kwa kashfa ya Eurobond anasema "siendi na siendi ,these guys are too junior to me"

Sasa jiulixe vipi utapigania demokrasia lakini huheshimu katiba,huheshimu utawala wa kisheria ,hutaki taasisi zifanye kazi vilivyo na siasa ndio unazingatia zaidi katika kila mwelekeo wako.Kwa kifupi don't trust Raila he's not fighting for democracy ,he's fighting for his own selfish "politics of the stomach".
 
Acheni kuwa kama mataahira nyie mazezeta unamsifiaje Uhuru wakati mahakamani imemtia hatiani kupitia tume ya uchaguzi?

Kuweni na akili mnaongea mambo ya kipumbavu kabisa mtu mwenye akili za kuvukia barabara tu hawezi kuongea hivi
Hawa si ni nyumbu mkuu
 
Ninakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa sana, ndiyo sababu sikusema asifiwe Raila, nimesema wananchi wote wa Kenya, nimetoa mfano wa Raila kwa sababu alifungwa muda mrefu, lakini wote hao akina Uhuru na Rutto walikuwa kambi moja kudai katiba mpya, lakini hulka ya binadamu ilivyo ni nafsi ya ubinafsi, kama katiba haikidhi matakwa yako unaanza kuigeuka, watu wengi wanapopigia kelele demkrasia, lengo ili iwe kwa maslahi yao si vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kuwa kama mataahira nyie mazezeta unamsifiaje Uhuru wakati mahakamani imemtia hatiani kupitia tume ya uchaguzi?

Kuweni na akili mnaongea mambo ya kipumbavu kabisa mtu mwenye akili za kuvukia barabara tu hawezi kuongea hivi
Utamfananisha na Sizonje ? Hata kukosolewa tu hataki km vile yeye ni malaika sembuse kuruhusu uchaguzi urudiwe ?
 
Kuwa na katiba nzuri ni jambo moja na kuifuata na kuilinda ni jambo lingine,,anachosifiwa uhuru ni kuilinda na kuifuata katiba,hebu jiulize kwetu tunaweza?iliyopo ni mbovu lkn hata yale mazuri tumeshindwa kuyafuata sembuse hiyo ktb mpya!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo pale nikakuambia sio kwamba Uhuru anapenda kuifuata hiyo katiba, ni kwasababu hiyo katiba imeweka misingi bora ya kuhakikisha inafuatwa haivunjwi ovyo ovyo, ndiyo sababu ikaitwa ni katiba nzuri, imeweka check and balances nyingi sana, ukijaribu tu kuivunja inakumaliza, kwa sababu imetoa mwanya wa mtu yeyote yule kumfungulia mashitaka rais na mwisho mahakama inaweza kumtoa madarakani, rais anaogopa kuchukua maamuzi kiurahisi, japo bado anavunja katiba lakini sio sana

Huku kwetu katiba inamruhusu rais kufanya mambo mengi sana, lakini tatizo lingine kubwa huku kwetu lipo kwa upinzani ambao ndiyo hasa wenye jukumu la check and balance kwa rais, pamoja nanmapungufu yake katiba ya sasa lakini imetoa uhuru wa kufanya siasa na kukusanyika kufanya mikutano ya siasa bila kusumbuliwa, hiyo ni haki ya kikatiba, ina maana yeyote atakayekiuka haki hiyo ashitakiwe mahakakani, rais Magufuli amezuia hiyo haki ya msingi, badala ya upinzani kwenda mahakamani, wanabaki kupiga kelele zisizo na faida yoyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naona jaji mkuu kateuliwa ili kuwasahaulisha ibada Kwa shujaa lissu

Don't mind me
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…