Mimi sioni kwanini Uhuru hapa anasifiwa, kama ni sifq ziende kwa wananchi wa Kenya ambao walipigana kwa muda mrefu kudai katiba yenye wigo mpana wa demokrasia, na msidhani ilipatikana kiurahisi, sio kweli, Raila huyo mnaemuona, alifungwa miaka 10 na mzee Moi kwa kudai uhuru wa kidemokrasia, na watu wengi walipoteza maisha chini ya utawala kandamizi wa Moi.
Wakenya walipochinjana mwaka 2007, Kenya ikawa njia panda, mtakumbuka Dunia nzima ilielekeza nguvu Kenya ili kuleta usuluhisha na maridhiano ya kudumu, moja ya makubaliano ni kuwa na katiba mpya, hii ambayo leo hii imemfunga rais wa Kenya asiwe na nguvu nyingi kisheria, hata ya kukemea rushwa, wala kusema lolote lile, kila kitu kimewekewa mipaka na katiba, kwa hiyo kushindwa kwa Uhuru kufanya lolote na kubaki kukubaliana na kila jambo, sio kwa mapenzi yake ni katiba yao inamlazimisha, na katiba hiyo sio kwamba viongozi wa Kenya waliipenda iwanyime uhuru wa madaraka, ni baada ya mkwamo uliotokea baada ya watu kuchinjwa 2007.
Huku Tanzania katiba iliyopo inampa madaraka makubwa rais, ndiyo mchakato huo wa kuipata katiba uekwama, watu huku Tanzania hawapo tayari kufungwa kama alivyofungwa Raila kudai demokrasia zaidi, au hata kumwaga damu kama walivyofanya wakenya, wanabaki kupiga kelele isiyoambatana na vitendo.
Anyway kwa kifupi, kilichofanyika Kenya, Uhuru hastaili pongezi kwa sababu amefuata katiba ya Kenya kama inavyotaka na sio kwamba yeye mwenyewe amelifanya kwa jitihada zake, na kiukweli yeye Uhuru ameonyesha kutopenda demokrasia hata kidogo kwa kutoa vitusho kwa jaji mkuu kinyume na katiba ya Kenya inayosema mahakama iachwe ifanye kazi yake bila vitisho vyovyote.
Kama nipongezi wanastahili wakenya kwa kupambana hadi kupata Katiba bora na kuilinda ili kuhakikisha haichezewi. Ila niwaombe wakenya wote kwa ujumla, kama katiba yenu inafanya vizuri katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kisiasa, kwa nini msiitumie kuwapatia ufumbuzi katika matatizo ya kiuchumi na kijamii, kama vile rushwa, ukabila, tofauti ya kipato kati ya matajiri na masikini, umilikaji wa ardhi na mauaji ya kiholela yanayofanywa na vyombo vya dola?
Sent using
Jamii Forums mobile app