.., naendelea kufuatilia siasa ya Kenya kwa ukaribu, siasa yao tamu sana.., ni mapambano kati ya wanasiasa na sio dola na wanasiasa..
.., naona UHURUTO 'wamepaniki'.., nimesikiliza hotuba ya Uhuru Kenyatta, William Rutto na Aden Duale wakiwa state house wakiongea na MCAs na governors.., wanapaswa sasa kutulia, wanaweza kuwa 'outshined'.., wanakuwa provoked na wameruhusu hasira ziendeshe kauli zao.., wanapaswa kutuliza munkari..
Mfano, Esther Passaris ( Nairobi woman representative) kutoka Kenya National Congress (KNC), anatumia nguvu kidogo kum'provoke Aden Bare Duale (Garissa town MP) na Duale anakasirika na kujibu kwa ghadabu.., fuatilia Twitter account ya Aden Bare Duale na Esther Passaris utaona moto ulivyowaka..
Mtifuano wa Aden Duale na Esther Passaris umeanza baada ya Raila Odinga (NASA chief principal) kusema IEBC hii haiwezi kuendesha tena uchaguzi mwingine baada ya awali kuwa nullified.. Duale akasema "kama kweli Raila ni mwanaume, aje awatoe IEBC".. hapo Esther Passaris akanunua ugomvi.., huyu Esther Passaris anatoka ODM..
Moto unazidi kuwaka.., NASA walikuwa Mathare pale Huruma stadium wanasema WAFULA CHEBUKAT (chairman wa IEBC) anapaswa kumfuta kazi CEO wa IEBC Ezra Chiloba.., wanamtuhumu kwa kuwahujumu kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifutwa na mahakama ya juu nchini humo.
Mbunge wa Embakasi-East (ODM), Paul Ongili Owino (Babu Owino) anasema kwamba wametoa siku 5 tu kwa Ezra Chiloba kuondoka ofisi za IEBC na asipofanya hivyo watakwenda kumuondoa ofisini kwa nguvu.., wallahi, vumbi itaruka.., Duale anasema hatoki mtu.., Owino anasema anatoka.. Kazi ipo!
Huyu Babu Owino ana balaa, wakati wa kuapisha wabunge alifanya balaa.. Alitakiwa kuapa zaidi ya mara 3., aliapa na kupachika jina la "Raila Amolo Odinga" kwenye kiapo na neno "Tibiim" kwenye hotuba yake, kila baada ya paragraph kulikuwa na neno "Mr Speaker, Tiaaaalala"..
.., ananifurahisha sana huyu kiumbe (Babu Owino) .., hii pia iliwahi kutokea mwaka 2007 aliyekuwa Mbunge wa Budalang'i, Ababu Namwamba aliwahi kufanya hivyo.. (kuapa kwa jina la RAO na sio official president of Kenya wakati huo, Mwai Kibaki)
NASA wana madai yao.., wanasema hawatakwenda kwenye uchaguzi kama madai yao hayatashughulikiwa.., wanataka mfumo wa kielektroniki wa kupokea matokeo upitiwe upya, wanataka wagombea wote wa awali wagombee, na wanataka baadhi ya watumishi wa IEBC waondoshwe kwenye tume huru ya uchaguzi na mipaka..
Utakumbuka kwamba, uchaguzi uliotajwa kufanyika oktoba 17, 2017 ulitakiwa kuhusisha wagombea wawili pekee wa NASA na JUBILEE, hatua ambayo inapingwa na NASA, na wanasema wote waliogombea awali waruhusiwe kugombea tena.., NASA wametishia kutoshiriki uchaguzi huo kama hawatasikilizwa..
Jubilee kwa upande wao wanasema uchaguzi chini ya IEBC hauna shida na wanasema wako tayari kwa uchaguzi.. NASA wa wao hawakushauriana na IEBC kuhusu kuafikiana tarehe ya uchaguzi.. Wanasema IEBC walishauriana na Jubilee tu.., NASA wao wanataka uchaguzi ufanyike kati ya 24 au 31 Oktoba..
Hivyo kwa jicho langu, kampeni hizi zitakuwa na balaa kubwa, timu ya NASA ambayo sasa inaweza kuwa 'threat' kubadili sana kwa Jubilee.., nimemsikia Gavana wa Mombasa, Ally Hassan Joho (ODM) akisema wanaunda timu ya Moto sana ya kampeni wakati huu kwa sababu wabunge, gavana na watu wote hawatakuwa na shughuli nyingine zaidi ya kampeni.., moto utawaka
Nimefuatilia nini maana ya "TIBIIM" na "TIALALA".., wataalam wanasema Tibiim kwenye siasa ni 'mapinduzi ya kisiasa' na kwenye maombi ukimaliza kwa neno hilo 'shetani popote alipo anatoka mbio' [emoji23]
Jubilee wana watu wa moto pia, 'mdosi' mwenyewe Uhuru Kenyatta, William Rutto, Johnson Sakaja, Peter Munya, Aden Duale, Justine Muturi, Joyce Laboso, Gideon Moi na wengine.. Moto utawaka.., sio kampeni za kukosa kufuatilia hizi..
Sent using
Jamii Forums mobile app