Uhuru ndiye rais pekee Afrika aliyealikwa kuhutubia mataifa makubwa ya G7

Uhuru ndiye rais pekee Afrika aliyealikwa kuhutubia mataifa makubwa ya G7

Hili kongomano la G7 huwa linahusisha mataifa saba yenye usemi mkubwa dunia hii, kualikwa pale uwahutubie huwa wamekuchunguza kwa makini na kubaini wewe sio mtu wa kuwapotezea muda, unalo la kusema ambalo utalisema bila kumumunya maneno na lazima uteme yai ipasavyo bila kuwa kigugumizi.

Hongera sana rais wangu, nenda pale useme nao, waonyeshe wale kuwa Afrika tunakuja na tumejiandaa na tunayo agenda, tuna malengo, tuna nia, tuna nguvu na tuna uwezo.
Hongereni sana Wakenya kwakua na Rais makini, mwenye uwezo mzuri wa kujieleza, Mzarendo wa kweli wa nchi yake na asiye na roho ya Kimasikini, kuna baadhi ya nchi Rais wao akitaka kuhutubia wanashika vichwa maana hawajui ataropoka utumbo gani.
 
Kauli ya kitoto sana na kama ni mtu mzima ni kauli ya mtu aliyekata tamaa
Kwani uongo?
Labda nirudie hili, Kenya ni Puppets tangu harakati za Uhuru!
Halafu yako mengi ya Kujivunia, hili nalo la kuitwa ni Lakujivunia? Hata kuanzishia uzi?
 
Kwani uongo acha azipende tu!
Mwingine kila siku akisima amasema sitawaangusha mara niliomba kura peke yangu!
Sasa g7 ataongea nini
Mimi nafikiri angeitwa mchagga mmoja au Mtei au Mbowe akaenda
 
"It will focus on the global economy, foreign policy, security of citizens and environmental sustainability".

Al-Shabab ndio wanampeleka huko.
 
Hili la Uhuru mimi sina shida nalo, tatizo langu ni hii inayojiita G7, kwamba ni mataifa yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, unaziachaje nchi Kama China na Russia na kuwaweka Italy na Japan halafu wanaenda kujadili masuala ya uchumi na usalama wa dunia, hii haipo sawa kabisa kwani kwenye masuala ya uchumi sasa hivi China ndie anayemfuatia America na Russia yupo imara mno kwenye masuala ya usalama wa dunia hii, halafu wanawekwa kando.
Hii dunia haiwezi fanikiwa kwa mtindo huu. Ukanda wa Korea haupo salama kwa sababu ya bwana mdogo Kim Jong Un, na siku zote Marekani anaomba support ya Mchina ili kumuwajibisha huyu Kim, halafu leo Mchina hayupo kwenye hiyo G7 yenu, Mrusi yupo Syria anamsupport Assad dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Marekani, halafu mnakaa kujadili usalama wa dunia hii bila Russia na China, uko ni kupoteza muda bure, kama mimi ningekuwa Uhuru Kenyatta nisingekweda.
 
"It will focus on the global economy, foreign policy, security of citizens and environmental sustainability".

Al-Shabab ndio wanampeleka huko.
Ndio, ameenda huko kama representative wa bara la Africa, kuzungumzia matatizo zinazokumba bara hili on the behalf of the continent. Na susla la ughaidi au utovu wa usalama in general sio matatizo inayoaffect Kenya pekee.

Hako huko kuzungumzia matatizo ya Kenya pekee, mbali bara nzima ya Africa, na jinsi haya mataifa ya G7 can help the continent.
 
Hiyo kweli, ndio maana nikasema wanakua makini katika kuchagua nani wa kualikwa awakilishe Afrika maana wale hawapendi kupoteza wakati, lazima uwe umejijengea mazingira ya kueleweka ili ukaribishwe pale.
Hivi hii ni mara ya ngapi wa kwenu kualikwa?
 
Back
Top Bottom