Uhuru Park, Kenya: Raila Odinga aapa kama Rais wa Watu bila kuwepo kwa makamu wake Kalonzo

Bavicha wamejipanga kusifia kila linalotokea Kenya hasa kuhusu Kenyata.Hujikuta wakielezea mapungufu yyt ya Kenyatta.Naweza sema Chadema kimekuwa chombo cha propaganda cha Kenyatta kwa upande wa Tanzania na EA.
 

Vurugu Arusha: Mke wa Dk. Slaa akiwa amejeruhiwa baada ya kudaiwa kupigwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU).
Mkuu hawa NYUMBU ni burudani sana.Huwa nafikiria wananini kwenye ubongo wao.
 
!
!
Aisee. Huku tangazo tu la hiyo event kwenye social media ingekuwa ni kosa la mtandao na uchochezi. Achilia mbali tukio lenyewe
[HASHTAG]#nguvuguniaakilikijiko[/HASHTAG]
 
Dah, Kasie, naona jirani leo umetutembelea. Huyo sibling yako ndo dadako mdogo au? Sisteh, nipe directions za kufika kwenye makao yake basi na contacts zake pia. Ntarudi na mrejesho, kuhusu hali yake na usalama wake pia. 😀😀😀

Yeah nimewatembelea ila naona washauvuruga uzi wa best yangu Mshana Jr.
Aahahahahaa ngoja nikija kutembelea kipindi cha passes nitakutafuta tupate wote stafutahi.
 
Msiwe watu wa kuzungumza bila utafiti....
Uliza historia ya Raila,uliza habari za watoto wake. ...mke wake...Halafu itimisha na tukio la leo....
Sasa si utupatie hiyo historia ya Raila ili tujifunze pia.
 
Faru John akiona tu hata kivuli cha Chadema barabarani amani hana, sinawahi ona watu wasiojiamini kama yeye.
 
Na GJ Malisa

Kuna mambo mawili ya kujifunza Kenya.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; ni kuhusu Raila. Amekuwa jasiri, na mwenye msimamo thabiti wa kusimamia kile anachoamini hadi dakika ya mwisho. Ameongoza maelfu ya watu wake katika kuhitimisha safari ya "Kaanani". Kwenye kampeni aliwaambia wananchi wake atashinda, matokeo yalipotangazwa hakukubaliana nayo. Akawaaongoza watu wake kuyakataa. Na leo ameungana nao kujiapisha.

Bila kujali vitisho kutoka vyombo vya dola, bila kujali kuwa anaweza kushtakiwa kwa "uhaini" lakini amejivika ujasiri. Hili ni funzo kwa viongozi wengi wa vyama vya siasa barani Afrika. Sio unawaambia watu "pigeni kura matokeo niachieni mimi" lakini siku ya matokeo unajifungia ndani, halafu baada ya miaka miwili unaenda kupongeza juhudi. If people grant their trust on u, please learn to fight your battle to the last.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; ni kuhusu Uhuru. Huyu ni kielelezo cha kiongozi wa mfano bora kabisa wa demokrasia duniani. Ameonesha "political maturity" ya hali ya juu sana. Kama ni soka huyu ndiye "man of the match" kwa leo.

Mwanzoni vyombo vya usalama vilitishia kusambaratisha kusanyiko hilo la Raila. Ni wazi wangefanya hivyo yangetokea machafuko makubwa sana nchini humo na huenda sasa hivi tungekua tunasambaza picha za majeruhi na marehemu na hashtag isemayo "Pray 4Kenya"

Lakini Uhuru ametumia hekima ambayo viongozi wengi wa Afrika wamekosa. Ameamua kuwaacha wafuasi wa Raila waridhishe mioyo yao. Wakati wafuasi wa Raila wanafika uwanjani tayari Askari walikua wametanda viwanjani hapo na silaha nzito. Uhuru alijua kwamba pamoja na kuzuia askari wasishambulie raia, lakini wafuasi hao wangeweza kuwachokoza askari na hatimaye kuzusha taharuki. Kwahiyo akaamua kuwaondoa askari wote uwanjani.

Hii ni busara ya hali ya juu sana. Sio viongozi wengine wamejaa mihemko wakiona tu watu wamekusanyika na tishert za "Pray4Somebody" wanaagiza wapigwe. Huku ni kuyatumia vibaya majeshi. Ukiona hata katuni unakasirika. Ebo.!! Kiongozi ni lazima ujifunze kuzuia mihemko yako. Mtu amepigwa risasi, watu wamekusanyika kwa amani ili wamuombee, unaagiza Polisi kuwasambaratisha kwa mabomu. Kama kusanyiko la kumuombea tu mtu linakupa mihemko, vp ukisikia kuna kiongozi anataka kujiapisha kama Raila?

Kuna wakati viongozi husababisha maafa bila sababu yoyote kwa kuvitumia vibaya vyombo vya ulinzi na usalama. Ni muhimu viongozi wa Afrika wajifunze busara ya Uhuru kwamba si lazima matumizi ya nguvu kila mahali. Uhuru anajua hamna Ikulu mbili, hakuna cabinet mbili, hakuna mabunge mawili. Anajua Raila amejiapisha kujifurahisha tu na kukata kiu ya wafuasi wake. Lakini at last atarudi nyumbani akale "gideri" na mke wake. Sasa kwanini ajihangaishe kupiga mabomu na kuua watu bure? This is the true meaning of democracy.

Salaam kwa Faru John.!
 
-Hili ni funzo kwa viongozi wengi wa vyama vya siasa barani Afrika. Sio unawaambia watu "pigeni kura matokeo niachieni mimi" lakini siku ya matokeo unajifungia ndani, halafu baada ya miaka miwili unaenda kupongeza juhudi. If people grant their trust on u, please learn to fight your battle to the last.
 
Msiwe watu wa kuzungumza bila utafiti....
Uliza historia ya Raila,uliza habari za watoto wake. ...mke wake...Halafu itimisha na tukio la leo....
Malisa kasema anayoyajua, hayo ya historia na watoto wake yalete tu Mkuu kwani umekatazwa? Halafu connect hiyo historia na yale ya jana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…