Uhuru Park, Kenya: Raila Odinga aapa kama Rais wa Watu bila kuwepo kwa makamu wake Kalonzo

Wasanii tu nyie naona mnajifariji...kichekesho ni pale unapompongeza uhuru kwa pamoja na raila!
Ninyi si mlikuwa mnafungamana na uhuru, kulikoni tena raila leo?!
Kweli wewe ni shithole, kwani ukifungamana na A huwezi kumpongeza B? Yaani kama mtu akikosea ukampinga kwa makosa yake kwahiyo ndiyo kusema unampinga milele? Hizi shule mlizoenda mlisoma ujinga tu
 
Mkuu watu waelewa huwa hawana jealous huwa hawana kinyongo wanampongeza mtu kwa matendo yake sio kwa upande wake.
 
Eti eeh, na mbona majuzi mamvi alipoenda ikulu kumpongeza JPM makamanda wote mlishikwa na taharuki hasa hapa jf?!
Tatizo lenu kumbukumbu hamna alafu ni wanafki balaa!!!.
 
Kuna mambo mawili ya kujifunza Kenya.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; ni kuhusu Raila Odinga. Amekuwa jasiri, na mwenye msimamo thabiti wa kusimamia kile anachoamini hadi dakika ya mwisho. Ameongoza maelfu ya watu wake katika kuhitimisha safari ya "Kaanani". Kwenye kampeni aliwaambia wananchi wake atashinda, matokeo yalipotangazwa hakukubaliana nayo. Akawaaongoza watu wake kuyakataa. Na leo ameungana nao kujiapisha.

Bila kujali vitisho kutoka vyombo vya dola, bila kujali kuwa anaweza kushtakiwa kwa "uhaini" lakini amejivika ujasiri. Hili ni funzo kwa viongozi wengi wa vyama vya siasa barani Afrika. Sio unawaambia watu "pigeni kura matokeo niachieni mimi" lakini siku ya matokeo unajifungia ndani, halafu baada ya miaka miwili unaenda kupongeza juhudi. If people grant their trust on u, please learn to fight your battle to the last.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; ni kuhusu Rais Uhuru Kenyatta. Huyu ni kielelezo cha kiongozi wa mfano bora kabisa wa demokrasia duniani. Ameonesha "political maturity" ya hali ya juu sana. Kama ni soka huyu ndiye "man of the match" kwa leo.

Mwanzoni vyombo vya usalama vilitishia kusambaratisha kusanyiko hilo la Raila. Ni wazi wangefanya hivyo yangetokea machafuko makubwa sana nchini humo na huenda sasa hivi tungekua tunasambaza picha za majeruhi na marehemu na hashtag isemayo "Pray 4Kenya"

Lakini Uhuru ametumia hekima ambayo viongozi wengi wa Afrika wamekosa. Ameamua kuwaacha wafuasi wa Raila waridhishe mioyo yao. Wakati wafuasi wa Raila wanafika uwanjani tayari Askari walikua wametanda viwanjani hapo na silaha nzito. Uhuru alijua kwamba pamoja na kuzuia askari wasishambulie raia, lakini wafuasi hao wangeweza kuwachokoza askari na hatimaye kuzusha taharuki. Kwahiyo akaamua kuwaondoa askari wote uwanjani.

Hii ni busara ya hali ya juu sana. Sio viongozi wengine wamejaa mihemko wakiona tu watu wamekusanyika na tishert za "Pray4Somebody" wanaagiza wapigwe. Huku ni kuyatumia vibaya majeshi. Ukiona hata katuni unakasirika. Ebo.!! Kiongozi ni lazima ujifunze kuzuia mihemko yako. Mtu amepigwa risasi, watu wamekusanyika kwa amani ili wamuombee, unaagiza Polisi kuwasambaratisha kwa mabomu. Kama kusanyiko la kumuombea tu mtu linakupa mihemko, vp ukisikia kuna kiongozi anataka kujiapisha kama Raila?

Kuna wakati viongozi husababisha maafa bila sababu yoyote kwa kuvitumia vibaya vyombo vya ulinzi na usalama. Ni muhimu viongozi wa Afrika wajifunze busara ya Uhuru kwamba si lazima matumizi ya nguvu kila mahali. Uhuru anajua hamna Ikulu mbili, hakuna cabinet mbili, hakuna mabunge mawili. Anajua Raila amejiapisha kujifurahisha tu na kukata kiu ya wafuasi wake. Lakini at last atarudi nyumbani akale "gideri" na mke wake. Sasa kwanini ajihangaishe kupiga mabomu na kuua watu bure? This is the true meaning of democracy.

Salaam kwa Faru John.!

Malisa GJ.
Kwanini watz ni wepesi sana wa kusahau? Na hii tabia ndio wanaitumia hata wanasiasa kutuhadaa.

Yani eti kwa sababu ya tukio hili tu tena ambalo linaonekana la kimkakati maana sura halisi imeonekana upande mwingine (kufungia media) ujinga wa watawala wa kiafrika (Uhuru included) tunausahau ghafla? Leo Uhuru anaitwa mpenda haki na mwanademokrasia, hizi akili finyu siku zote zinasababishwa na ushabiki. Mara hii tumesahahu watu waliouawa kwenye maandamano hapo Kenya wiki chache kabla, wakati na baada ya uchaguzi huu uliomuidhinisha Uhuru? Tumesahahu nini Kenyatta alimwambia Jaji mkuu na mahakama yake atafanya akichaguliwa?

Kimsingi "maigizo" aliyofanya jana Raila wala si chochote ni vile nae tu anataka aonekane yupo
 
Bavicha wamejipanga kusifia kila linalotokea Kenya hasa kuhusu Kenyata.Hujikuta wakielezea mapungufu yyt ya Kenyatta.Naweza sema Chadema kimekuwa chombo cha propaganda cha Kenyatta kwa upande wa Tanzania na EA.
Whatever you speak, when comes to democracy and economy Kenya is ahead of us by a 1000 miles kwa nini tusiwasifie.
 
Kweli wewe ni shithole, kwani ukifungamana na A huwezi kumpongeza B? Yaani kama mtu akikosea ukampinga kwa makosa yake kwahiyo ndiyo kusema unampinga milele? Hizi shule mlizoenda mlisoma ujinga tu
Lakini lisu na lema walipomponda mamvi alipokwenda ikulu kumpongeza JPM uliona sawa, ila leo ndio unaona ni tofauti!!
mtu aliyewapa lile jina la wale wanyama maarufu kule serengeti hakika hakukosea!
 
Whatever you speak, when comes to democracy and economy Kenya is ahead of us by a 1000 miles kwa nini tusiwasifie.
Basi muwe mnaenda hadi kufanya maandamano kusifia uongoz wa UK
 
Ingekua Tanzania wengine saivi wangekua wanachimba makaburi, wengine wako hospital na wengine wako rumande
 
Kwanini watz ni wepesi sana wa kusahau? Na hii tabia ndio wanaitumia hata wanasiasa kutuhadaa.

Yani eti kwa sababu ya tukio hili tu tena ambalo linaonekana la kimkakati maana sura halisi imeonekana upande mwingine (kufungia media) ujinga wa watawala wa kiafrika (Uhuru included) tunausahau ghafla? Leo Uhuru anaitwa mpenda haki na mwanademokrasia, hizi akili finyu siku zote zinasababishwa na ushabiki. Mara hii tumesahahu watu waliouawa kwenye maandamano hapo Kenya wiki chache kabla, wakati na baada ya uchaguzi huu uliomuidhinisha Uhuru? Tumesahahu nini Kenyatta alimwambia Jaji mkuu na mahakama yake atafanya akichaguliwa?

Kimsingi "maigizo" aliyofanya jana Raila wala si chochote ni vile nae tu anataka aonekane yupo
Ok, hebu muweke rais Magufuli kwenye viatu vya jana vya rais Uhuru na Chadema waandae mkutano Jangwani wa kumuapisha rais wa mioyo yao Lowassa, sincerely tuambie unadhani nini kingetokea?
 
Nguchiro kutukana msasi kaona shimo, kuna uwezekano mkubwa ana nguvu ya ziada somewhere tusikojua
 
LAO is far greater daunting than UMK. Kina cha maji hakipimwi kwa miguu!
 
23e6c63f165bf0d4accc08c48a1ed689.jpg

Vurugu Arusha: Mke wa Dk. Slaa akiwa amejeruhiwa baada ya kudaiwa kupigwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU).
Asante kwa kutukumbusha kwa picha, ingekuwa Tanzania leo mortuary za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Mloganzila zote zingefurika maiti.
 
Ok, hebu muweke rais Magufuli kwenye viatu vya jana vya rais Uhuru na Chadema waandae mkutano Jangwani wa kumuapisha rais wa mioyo yao Lowassa, sincerely tuambie unadhani nini kingetokea?
Sijui nini kitatokea maana hata yeye ni mwanasiasa wa kiafrika ambaye muda mwingine anacheza na akili ya watu. So, lolote kaweza kutokea. Maana uoga mwingine ni watu wamejivika, mfano kwa Tz hata hao wapinzani hawawezi kufanya alichofanya Raila jana, wanasimama majukwaani wanasema watz ni waoga ilhali wao tangu waambiwe "sijaribiwi" wameufyata. Huo uoga wetu ndio unafanya tuamini kuwa lile la Kenya haliwezi kutokea Tanzania
 
-Hili ni funzo kwa viongozi wengi wa vyama vya siasa barani Afrika. Sio unawaambia watu "pigeni kura matokeo niachieni mimi" lakini siku ya matokeo unajifungia ndani, halafu baada ya miaka miwili unaenda kupongeza juhudi. If people grant their trust on u, please learn to fight your battle to the last.
Na GJ Malisa

Kuna mambo mawili ya kujifunza Kenya.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; ni kuhusu Raila. Amekuwa jasiri, na mwenye msimamo thabiti wa kusimamia kile anachoamini hadi dakika ya mwisho. Ameongoza maelfu ya watu wake katika kuhitimisha safari ya "Kaanani". Kwenye kampeni aliwaambia wananchi wake atashinda, matokeo yalipotangazwa hakukubaliana nayo. Akawaaongoza watu wake kuyakataa. Na leo ameungana nao kujiapisha.

Bila kujali vitisho kutoka vyombo vya dola, bila kujali kuwa anaweza kushtakiwa kwa "uhaini" lakini amejivika ujasiri. Hili ni funzo kwa viongozi wengi wa vyama vya siasa barani Afrika. Sio unawaambia watu "pigeni kura matokeo niachieni mimi" lakini siku ya matokeo unajifungia ndani, halafu baada ya miaka miwili unaenda kupongeza juhudi. If people grant their trust on u, please learn to fight your battle to the last.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; ni kuhusu Uhuru. Huyu ni kielelezo cha kiongozi wa mfano bora kabisa wa demokrasia duniani. Ameonesha "political maturity" ya hali ya juu sana. Kama ni soka huyu ndiye "man of the match" kwa leo.

Mwanzoni vyombo vya usalama vilitishia kusambaratisha kusanyiko hilo la Raila. Ni wazi wangefanya hivyo yangetokea machafuko makubwa sana nchini humo na huenda sasa hivi tungekua tunasambaza picha za majeruhi na marehemu na hashtag isemayo "Pray 4Kenya"

Lakini Uhuru ametumia hekima ambayo viongozi wengi wa Afrika wamekosa. Ameamua kuwaacha wafuasi wa Raila waridhishe mioyo yao. Wakati wafuasi wa Raila wanafika uwanjani tayari Askari walikua wametanda viwanjani hapo na silaha nzito. Uhuru alijua kwamba pamoja na kuzuia askari wasishambulie raia, lakini wafuasi hao wangeweza kuwachokoza askari na hatimaye kuzusha taharuki. Kwahiyo akaamua kuwaondoa askari wote uwanjani.

Hii ni busara ya hali ya juu sana. Sio viongozi wengine wamejaa mihemko wakiona tu watu wamekusanyika na tishert za "Pray4Somebody" wanaagiza wapigwe. Huku ni kuyatumia vibaya majeshi. Ukiona hata katuni unakasirika. Ebo.!! Kiongozi ni lazima ujifunze kuzuia mihemko yako. Mtu amepigwa risasi, watu wamekusanyika kwa amani ili wamuombee, unaagiza Polisi kuwasambaratisha kwa mabomu. Kama kusanyiko la kumuombea tu mtu linakupa mihemko, vp ukisikia kuna kiongozi anataka kujiapisha kama Raila?

Kuna wakati viongozi husababisha maafa bila sababu yoyote kwa kuvitumia vibaya vyombo vya ulinzi na usalama. Ni muhimu viongozi wa Afrika wajifunze busara ya Uhuru kwamba si lazima matumizi ya nguvu kila mahali. Uhuru anajua hamna Ikulu mbili, hakuna cabinet mbili, hakuna mabunge mawili. Anajua Raila amejiapisha kujifurahisha tu na kukata kiu ya wafuasi wake. Lakini at last atarudi nyumbani akale "gideri" na mke wake. Sasa kwanini ajihangaishe kupiga mabomu na kuua watu bure? This is the true meaning of democracy.

Salaam kwa Faru John.!

Zero Brain wewe uliyeandika huu ujinga! Ni nchi ngapi za Kiafrika zilizopitia Kenya iliopitia 2007/08? Unafikiri Raisi wa nchi kutishiwa kufungwa nchi ya Muzungu ni jambo dogo?

Unajua wangeamua kuzuia nini kingetokea? Ule ulikuwa ni mtego wangethubutu hata kumshika Raila kingenuka na mambo ya icc yangeanza!

Next time jaribu kulinganisha vinavyolingana, Kenya Upinzani wana uwezo wa kufanya nchi isitawalike na ndo maana ni lzm wawasiklize na siyo hiari na hili halina uhusiano wowote ule na Demokrasia bali ni uwezo wa Upinzani kutumia nguvu kushinikiza, kwa maana nyingine ni lazima Serikali iwasikilize na siyo ombi!
 
Back
Top Bottom