Uhuru unaopiganiwa na wachache huwanufaisha wachache. Uhuru unaopiganiwa na wengi huwanufaisha wengi.

Uhuru unaopiganiwa na wachache huwanufaisha wachache. Uhuru unaopiganiwa na wengi huwanufaisha wengi.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UHURU UNAOPIGANIWA NA WACHACHE HUWANUFAISHA WACHACHE. UHURU UNAOPIGANIWA NA WENGI HUWANUFAISHA WENGI.

Anaandika Robert Heriel
Mtibeli

Viongozi wanakula Sana. Viongozi wanajipendelea Sana. Viongozi wanajipimia minofu Mikubwa.

Huna haja ya kulalamika na kulaumu wengine.

Iko hivi, Uhuru ukipiganiwa na Wachache basi wanufaika wake watakuwa haohao Wachache. Na Uhuru ukipiganiwa na wengi wanufaika wake watakuwa wengi.

Uhuru wa Jambo lolote lile. Uwe Uhuru wa Kifikra, Uhuru wa kisiasa, Uhuru wa kiuchumi, Uhuru wa kidini n.k.

Kwenye ngazi ya kifamilia, Yule anayehangaika kupambana kwaajili ya kuleta Uhuru wa kiuchumi kwenye familia inategemewa kuwa yeye ndiye atakuwa mnufaika wa Kwanza katika Uhuru huo.
Sio ajabu Sisi wanaume kwenye jamii nyingi tupo huru zaidi kwenye familia kuliko wanawake kwa sababu Sisi kwa sehemu kubwa ndio tunahangaika kutafuta Uhuru wa kiuchumi ndani ya Familia.
Wanawake wengi hulalamika kukandamizwa, kuzongwa na kunyimwa Uhuru ndani ya nyumba lakini uhalisia wa Jambo hilo upo kwenye Nani ana-struggle zaidi kupigania Uhuru wa kiuchumi ndani ya nyumba.

Kisiasa, viongozi waliokuwa mstari wa mbele kupigania Uhuru wa kisiasa inategemewa wao ndio watakuwa wanufaika wakubwa wa Uhuru huo ndipo wengine wafuate.

Kwa mfano, CHADEMA au vyama vya upinzani vinavyopigana kufa na kupona huku wananchi wake wamelala wakitegemea watu Wachache wawatetee. Siku vyama hivyo vikifanikiwa kuchukua Dola. Haitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa kwa wananchi kwani waliohangaika kupigania Uhuru Fulani iwe wa kidemokrasia, au kiuchumi au vyovyote ni Wachache Sana tena ni kundi la chama Fulani.

Hii ni kusema kundi linalopigania Uhuru Fulani ndilo litanufaika zaidi ya makundi mengine.

Hakuna njia ya watu wote kunufaika na Uhuru wa kweli zaidi y watu wote kushiriki katika mapambano ya kupigania huo Uhuru.

Sisi watibeli tunajua yakuwa, mwananchi anayetegemea kupiganiwa ataendelea kuwa mtumwa au Uhuru wake utaendelea kudhibitiwa hata tawala zingebadilika kila mara.

Level ya Familia,
Familia inaweza kuwa na watoto watatu. Wazazi wakawa wanasomesha hao watoto watatu
Lakini mtoto Mmoja akawa anaonyesha jitihada ya zaidi kuliko wengine ambao hawataki kusoma.
Mwisho wa siku wale watoto wawili watafeli, huyu Mmoja atafaulu.
Baadaye atapata Kazi nzuri yenye kipato kizuri.
Wazazi watakuwa wanamuambia mtoto aliyefanikiwa kuwa walimsomesha ili awasaidie wao na ndugu zake. Lakini swali Linakuja atawasaidia Mpaka Lini?
Atawasaidia mwanzoni tuu tena sio kwa kiwango walichotarajia. Mwisho wa siku atachoka.
Yeye ndiye atanufaika zaidi kuliko wengine.

Uhuru wa kujieleza, Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa, Uhuru wa kisiasa utawahusu wale waliomstari wa mbele kuupigania kwa gharama zozote zile.

Kuna wakati watu wanalalamika, Mbona watu Fulani kwenye nchi wakiongea hawakamatwi na hata wakikamatwa haichukui muda wanatolewa. Tena wakikamatwa wanakamatwa kiheshima huku wengine wakikamatwa kiudhalilishaji.

Ndugu yangu, kama ndio mara yako ya Kwanza kukamatwa kisa Uhuru kwenye ukoo wenu lazima udhalilike na udhalilishwe.
Hiyo IPO kwenye Jambo lolote.

Kukamatwa kwa mara ya Kwanza ni tofauti na kukamatwa kwa mara ya pili na yatatu kuendelea.

Kama Baba yako aliwahi kukamatwa kwa level ya kitaifa, wewe ukikamatwa haitakuwa kidhalilishaji kama ambao hawajawahi kukamatwa.

Mtoto wa Lisu, au Mbowe, Sugh, au Wangwe, hawezi kuwa Sawa na wewe ambaye kwenye ukoo wenu hamkuwahi kulipa gharama.

Nazungumzia nini?
Ni kwamba, HAKI kwa wote au Uhuru kwa wote tafsiri yake ni watu wote lazima wapambane katika kiwango kinacholingana au kukaribiana.

Mimi acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom