Uhuru wa Kujieleza Unaendelea Kushambuliwa Katika Maeneo Mengi Duniani

Uhuru wa Kujieleza Unaendelea Kushambuliwa Katika Maeneo Mengi Duniani

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Udhibiti Uhuru Mtandaoni 2.jpg


Jinsi tunavyoiona dunia na kuitendea inategemea sana taarifa tulizo nazo. Hii ndiyo sababu uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari ni haki za kimsingi, na mtiririko huru wa mawazo ni kichocheo kikuu cha maendeleo jamii na ustawi wa binadamu.

Hata hivyo, uhuru wa mawazo na utoaji/upokeaji wa taarifa unaendelea kuzikwa katika maeneo mengi duniani. Moja kati ya mbinu ambazo zimekuwa zikitumiwa na mamlaka ni pamoja na kuuminya uhuru wa wananchi kujieleza kupitia mitandao ya kijamii.

Taasisi ya Freedom House kupitia ripoti yake ya Uhuru kwenye Mtandao iliyotolewa mwaka 2022 iligundua kuwa watumiaji wa mtandao katika nchi 53 walishitakiwa, kukamatwa, au kufungwa kwa sababu ya kuchapisha masuala ya kisiasa au kijamii.

Nchini Libya, kwa mfano, watumiaji walioshiriki maoni ya uhalifu au kuripoti mtandaoni walitoweka ghafla uraiani na baadaye kufahamika kuwa walikuwa kizuizini. Mfano mwingine ni pale ambapo mamlaka za Rwanda zilimhukumu aliyetoa maoni yaliyoikosoa Serikali kupitia YouTube kwa kifungo cha miaka 15 mnamo Septemba 2021.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa Mamlaka katika takribani nchi 40 zilizuia maudhui ya kijamii, kisiasa, au kidini mtandaoni, ambacho hicho ni kiwango kikubwa zaidi kurekodiwa na taasisi hiyo.

Katika takribani nchi 22, ripoti inaeleza, mamlaka za serikali zilizuia ufikiaji wa mitandao ya kijamii au majukwaa ya mawasiliano. Baadhi ya vikwazo viliwekwa ili kulazimisha makampuni kufuata sharti la kufungua ofisi kwenye nchi husika, kuhifadhi data ndani ya nchi hizo, au vinginevyo kutekeleza aina ya utendaji utakaowezesha udhibiti wa serikali au ufikiaji wa data.

UDHIBITI WA UHURU MTANDAONI.jpg

Kwa mfano, mnamo mwezi Juni 2021 mtandao wa Twitter ulifungiwa nchini Nigeria. Kusimamishwa huko kulikuja siku mbili baada ya Twitter kufuta tweet ya Rais Muhammadu Buhari ambayo ilichukuliwa kuwa ya kuudhi. Hata hivyo, mamlaka za Nigeria baadaye zilibatilisha kizuizi hicho kilichodumu kwa miezi saba zikidai kuwa kampuni hiyo ilikubali kusajili shughuli zake nchini Nigeria na kuwa na utaratibu mpya wa kodi.

Kuongezeka kwa ulazima wa upatikanaji wa mtandao kwa watu wote duniani kwa ajili ya mahitaji yahusuyo afya, elimu, ajira, sanaa, usawa wa kijinsia n.k – ina maana kwamba mwanadamu hawezi kutenganishwa na haki hiyo.

Kama Kifungu cha 27 cha Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu kinavyosema,“Kila mtu ana haki ya kushiriki kwa uhuru katika maisha ya kitamaduni ya jamii, kufurahia sanaa na kushiriki katika maendeleo ya kisayansi na manufaa yake”
 
Back
Top Bottom