Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 79
- 1,444
Huko bondeni kwa Madiba hali ya chama kilicholeta uhuru ANC ni mbaya sana tangu kuanzishwa kwake. Kwa mazingira haya hakiwezi kuunda serikali kwa sababu kimekosa 50% ya kura zote zilizopigwa.
Mambo kama haya ndio yanaifanya CCM ikatae #KatibaMpya na Tume huru. Nawaambia hizo trillion 6 ambazo mama Abdul anakopa Korea kazi yake itakuwa kununua magari ya polisi, mabomu, bunduki na kununua wapinzani 2025. Msitegemee pesa hizi zitaenda kujenga madarasa au barabara.
Wananchi wa Africa kusini wamekataa kuipigia ANC kura na kupigia vyama vya upinzani kwa sababu ya chama hicho kukumbwa na kashfa za rushwa, ufisadi na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Kitu kimoja ambacho sisi wapigania haki tutamkumbuka Mandela, ni namna alivyojenga misingi bora ya kimfumo na kiutawala. Mandela aliona mbali kwamba hata bila uwepo wake nchi iendeshwe kitaasisi na sio mtu mmoja ndio anatawala kila kitu kama ilivyo hapa nchini. Katiba bora ya South Africa ndio imezaa taasisi imara ikiwemo mahakama na Tume Huru ya Uchaguzi.
Moja ya kitu ambacho mimi binafsi ninamlaumu Nyerere ni kutengeneza mfumo wa utawala unaopeleka nguvu yote kwa mtu mmoja na sio taasisi. Kwamba taasisi zote zinakuwa chini ya mtawala na yeye ndio anateua na kufukuza watu kwenye hizo taasisi ikowemo Tume ya Uchaguzi, Mahakama na Bunge. Mtawala huyo anaweza kuiba mali za umma na kuuza rasilimali za nchi bila kuwajibishwa. Pamoja na mazuri yake mwalimu Nyerere lakini kwa hili alitukosea Watanzania. Nchi inaliwa, rasilimali za nchi zinauzwa kwa mikataba mibovu lakini wananchi hatuna cha kufanya . Tiukitaka tuamue kupitia kura mtawala anatumia bunduki kujitangazia ushindi wa uchaguzi .
Anyway tusife moyo nguvu ya Umma wananchi kwa umoja wetu tunaweza kuamua hatma ya nchi yetu ipate katiba mpya yenye taasisi huru kama wenzetu hawa.
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu ibariki Zanzibar
Mungu ibariki Tanzania
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.