Uhuru wa vyombo vya habari, vyombo vya habari vya Magharibi viko huru?

Uhuru wa vyombo vya habari, vyombo vya habari vya Magharibi viko huru?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Vita vya Russia na Ukraine vimenifumbua macho yangu. Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi ni vyombo ambavyo havitoi habari kuhusu kile kinachoendelea kwenye vita, havisimami katikati, vimeegemea upande. Iko siku vyombo hivi vitatumika kurudisha ukoloni Afrika.

Je, vyombo vya habari vya magharibi (BBC, DW, France, VOA, Facebook, You tube, nk) ni mfano wa kuigwa wa uhuru wa habari nchini?
 
Ni Vyomba vya ajabu kama ilivyo TBC ya Tanzania. Sikutegemea kabisa. Ni wanafiki was kiwango cha planet Neptune
 
Vita vya Russia na Ukraine vimenifumbua macho yangu. Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi ni vyombo ambavyo havitoi habari kuhusu kile kinachoendelea kwenye vita, havisimami katikati, vimeegemea upande. Iko siku vyombo hivi vitatumika kurudisha ukoloni Afrika.

Je, vyombo vya habari vya magharibi (BBC, DW, France, VOA, Facebook, You tube, nk) ni mfano wa kuigwa wa uhuru wa habari nchini?
Huwa nazimia naamka kisha tena hata zaidi ya mara 70 kwa siku nikiwa naona nyota nyota tu wabongo tunapopumbazwa na ujinga uitwao "democracy" toka Ulaya magharibi nakati ni usanii mtupu tu wa kwenye makaratasi lakini kiuhalisia wanakupangia na kukuamuru ufate watakavyo wakati wowote.

Haya wapumbavu wa unazi toka USA na EU popote mlipo jipigeni makofi vifuani penu mara tatu mkisema kwa sauti kuuuubwa kuwa "sisi ni wapumbavu kupindukia" [emoji847]
 
Vita vya Ukraine vimetoa somo kubwa ssna kuhusu Uhuru na Haki

1) Tunaambiwa mara zote tusichanganye Siasa na Michezo na hata Serikali ikitia mguu kidogo kwny vyama vya soka vya nchi husika FIFA huwa wakali sana lakin kwny Vita hii wameingia wazima wazima kwa kuizuia FIFA na hata kwny team ya Chelsea tumejionea!

2)Tunaambiwa uhuru wa kujieleza na uvumilivu wa kusikia usiyoyapenda lakin vyombo vya habari vya Russia vimepigwa kufuli kusikika maeneo mengine

3) Kuna Matajiri kadhaa mali zao zimeshikiliwa kwa kuwa tu wana urafiki na Putin wakati haikuwa kusemwa ni kosa na hata Mtoto wa kike wa Putin kawekewa vikwazo kadhaa ikiwemo vya kusafiri
 
Huwa nazimia naamka kisha tena hata zaidi ya mara 70 kwa siku nikiwa naona nyota nyota tu wabongo tunapopumbazwa na ujinga uitwao "democracy" toka Ulaya magharibi nakati ni usanii mtupu tu wa kwenye makaratasi lakini kiuhalisia wanakupangia na kukuamuru ufate watakavyo wakati wowote.

Haya wapumbavu wa unazi toka USA na EU popote mlipo jipigeni makofi vifuani penu mara tatu mkisema kwa sauti kuuuubwa kuwa "sisi ni wapumbavu kupindukia" [emoji847]
Watu wetu wanaangamia kwa kukosa maarifa na exposure. Yaani unapomuona mswahili anaandamana akidai demokrasia kama ya magharibi unamhurumia sana. Huko Magharibi hakuna demokrasia hata kidogo. Media zao zote zinawatumia watu wa Magharibi TU, ni vyombo vya propaganda.

Hebu fikiria kama siku nchi jirani na Marekani kama Mexico na Cuba kama siku wakisema kuwa wanaumgana na Russia kuweka mifumo ya ulinzi ya Urusi nchini mwao unadhani Marekani hatafanya anachokifanya Putin Leo kwa Ukraine?
 
Back
Top Bottom