Uhuru wa wanachama dhidi ya wenyeviti wao CHADEMA as sample

Uhuru wa wanachama dhidi ya wenyeviti wao CHADEMA as sample

Magufuli alipomwambia Lisu aachane na kugombea kwa ahadi ya kutafutiwa kazi hukuona?
Alitaka afanye nae kazi ila ajirudi na aache kutumika. Kwamba we ni mzuri usipotumika na watu wasioitakia mema tz.
 
Ukitaka kujiunga Chadema ili ujulikane, uheshimiwe na hata kupewa nafasi mbali mbali ndani ya chama ni lazima ukubaliane na mambo mawili ambayo ni:

1- Ukubali kuwa mtumwa wa kimawazo kwa mwenyekiti wa chama, nikiwa na maana kuwa mtu ukishakuwa katika stage hiyo hauwezi kuwa na uhuru wa kuamua jambo lolote linakuhusu wewe au familia yako bila kumshirikisha mwenyekiti na kuchukua mawazo au maamuzi yake kuwa ndio njia mbadala wa kutatua au kuamua jambo linalokuhusu ww au familia. Waliojaribu kutumia uhuru wao binafsi bila kumshirikisha mwenyekiti kila mtu aliona walivyoshambuliwa na genge la mwenyekiti bila kujali nyadhifa na heshima zao ndani ya chama, refer kwa P Msigwa na wengine wa aina yake.

2- Uwe mzee wa ndio, nikiwa na maana kwamba jambo lolote litakaloamuliwa na chama chini ya mwenyekiti wao hata kama halina tija, faida au maana yoyote kwa taifa na chama unatakiwa ukubali, na ukipinga utashambuliwa na genge la mwenyekiti kama ilivyotokea kwa hao wabunge 19 wa viti maalum nk.

Kwahiyo kwa Tanzania bado sana kupata chama cha upinzani ambacho kinaweza angalau kuonesha mfano wa utawala bora pale kitakapokamata nchi.
Hii imemkuta lema na msigwa. Sugu anaonekana ana maamuzi yake linapokuja suala la familia ndio maana m/kiti hajamuweka karibu sana pamoja na sugu kumfagilia kote hadi kumuita mtoto wake freeman.

Tofauti na msigwa ambaye hata akiitwa saa hizi na mbowe atawasha gari kutoka iringa aje dar, sugu huwezi kumtoa kiivyo.

Profesa J pia ana maamuzi yake tofauti na kina heche bendera fuata upepo.
 
Magufuli alipomwambia Lisu aachane na kugombea kwa ahadi ya kutafutiwa kazi hukuona?
Alimwambia kua hataweza kushinda kwa ustaarabu aili kupunguza ghalama za uchaguzi basi amuachie lakini sio hili la hongo kwa mdee

Sasa tunauliza baada ya mdee kukataa hiyo mafasi alipewa nani mwingine?

Au hiyo nafasi ilikua ya mdee peke yake na sii wengine endapo mdee atakataa?
#kataa wahuni kwenye vyama.
 
Mkuu kuna vijana wapo mitandaoni,ukitoa hoja ya kumjadili mwenyekiti utaoga matusi hadi ushangae..

Kwahiyo hivyo ndivyowalivyo.ni hatari sana,waache hivyohivyo na mwenyekiti wao wa kudumu.
leo kasema ni supreme leader
 
Najaribu kuwaza pia Mtu ambaye anashawishiwa na M/K "at individual capacity" kwa ahadi ya kutafutiwa kazi Nje ya Nchi, ili aachane na maamuzi yake, akikubali kufanya hivyo, uhuru wake utakuwaje ndani ya Chama!!.
Hii inatakiwa kuitafakari bila Muhemko
Wala matusi

Bado najiuliza pia anayetoa offer ya kupatia Watu kazi kutoka kwenye Ubunge, linapofika suala la Wabunge kununuliwa na kuahidiwa vyeo kama ambavyo madai yaliyokuwepo unyoofu wa maelezo hayo unahitaji kutafakari kidogo hasa likija jambo la kuwanyooshea vidole wengine.

Bado mtu bila kuogopa anataja hadharani kwamba nilimuita kumshawishi je kwanini asiseme chama kimewaita Au ninewaita Kwa niaba ya chama

Unasema umemlea mtu tokea chuo ili ashike nafasi ya chama inamaana chama hakina kamati kadhaa za kukaa na kuamua mpaka mtu mmoja?

Kwa kifupi tunasafari ndefu kidogo na Vyama vyetu, ukuaji na ushawishi wake dhidi ya watu waliomo kwenye Vyama hivyo na ukwasi wao.

Labda niazime mawazo ya wanaosema tujenge Taasisi siyo watu, maelezo ya Mwenyeketi na Ushawishi wake kuna Wakati unanijaza hofu juu ya Uhuru wa Wanachama dhidi yake.

Vyama vyetu bado vina kazi kubwa kujenga Taasisi kuliko kuhimiza nguvu ya mtu mmoja mmoja ndani ya chama

KATIBA za Vyama vyetu uwenda ndio ziko hivyo mbovu mbovu

Britanicca
Haya tunayoyaona ni matokeo ya mifumo yetu tangu malezi na tabia ndani ya familia zetu,mifumo ya utendaji kazi katika mataasisi na maidira ,zimelea tamaduni za kutengeneza matabaka,ya wakupata maslahi ,matabaka ya kunyonywa na matabaka ya kuhakikisha maslahi ya wanyonyaji hayahojiwi wala kuathiriwa kwa namna yeyote bila kujali waajira wao au walio wapa madaraka.
 
..Chadema wanamkosoa na kumsema Mwenyekiti wao kwa uwazi na uhuru kuliko Ccm.

..Kwa mfano, Mbowe alikuwa na msimamo wake kuhusu maridhiano, lakini wanachama walipiga kelele kwamba kuna ulaghai. Mbowe ali-resist kwa muda, lakini alikuja kukubaliana na msimamo wa wanachama wake.

..Ccm Mwenyekiti wao hata akiamua jambo la kipumbavu, wanachama humuunga mkono, na vyombo vya dola hutumika kulazimisha maamuzi haramu ya Mwenyekiti.

..Kwa mfano, serikali nimenunua gari la kinyesi liko kwenye msafara wa Mwenyekiti wao. Jambo la kipumbavu na kifisadi. Lakini hakuna mwana Ccm aliyejitokeza na kupinga upumbavu huo.

..Chadema na vyama vya upinzani kwa ujumla kuna uhuru wa mawazo, na kujieleza, kuliko Ccm.
 
Ukitaka kujiunga Chadema ili ujulikane, uheshimiwe na hata kupewa nafasi mbali mbali ndani ya chama ni lazima ukubaliane na mambo mawili ambayo ni:

1- Ukubali kuwa mtumwa wa kimawazo kwa mwenyekiti wa chama, nikiwa na maana kuwa mtu ukishakuwa katika stage hiyo hauwezi kuwa na uhuru wa kuamua jambo lolote linakuhusu wewe au familia yako bila kumshirikisha mwenyekiti na kuchukua mawazo au maamuzi yake kuwa ndio njia mbadala wa kutatua au kuamua jambo linalokuhusu ww au familia. Waliojaribu kutumia uhuru wao binafsi bila kumshirikisha mwenyekiti kila mtu aliona walivyoshambuliwa na genge la mwenyekiti bila kujali nyadhifa na heshima zao ndani ya chama, refer kwa P Msigwa na wengine wa aina yake.

2- Uwe mzee wa ndio, nikiwa na maana kwamba jambo lolote litakaloamuliwa na chama chini ya mwenyekiti wao hata kama halina tija, faida au maana yoyote kwa taifa na chama unatakiwa ukubali, na ukipinga utashambuliwa na genge la mwenyekiti kama ilivyotokea kwa hao wabunge 19 wa viti maalum nk.

Kwahiyo kwa Tanzania bado sana kupata chama cha upinzani ambacho kinaweza angalau kuonesha mfano wa utawala bora pale kitakapokamata nchi.
How
 
Back
Top Bottom