Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu (blood group) na Uchumba/Mimba/Ujauzito/Mtoto

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu (blood group) na Uchumba/Mimba/Ujauzito/Mtoto

karv

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
1,802
Reaction score
3,253
1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe

2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen. Kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen:
• Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A
• Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B
• Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB
• Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O

3. Katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor:
(a) Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya +
- mfano A+, B+, AB+ au O+
(b) Mtu ambaye cell zake nyekundu hazina hii antigen D, blood group yake inaandikwa na alama
-mfano A-, B-, AB- au O-

4. hii alama ya + au - inapatikana je?
(a) Baba hutoa Rh moja kwa mtoto, inaweza kuwa Rh+ au Rh- na mama hutoa Rh moja inaweza kuwa Rh+ au Rh-
(b) mtoto akizaliwa akiwa na Rh - manake baba alitoa Rh- na mama alitoa Rh -
(c) Mtoto akiwa Rh+ anaweza kuwa baba alitoa Rh+ na mama alitoa Rh+ mtoto mwenye Rh + anaweza kuwa alipata Rh- na Rh + ila hatuoandika Rh+Rh- kwa sababu Rh- ni kma haipo

UCHUMBA NA KUZAA /UJAUZITO
• Mvulana akiwa na damu yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ )
• Anaweza kuoana na msichana yeyote mwenye damu group yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ ) na watapata watoto bila tatizo lolote.
• Mvulana akiwa na group mfano ( A+, B+, AB+ au O+) akioa msichana mwenye A-, B-, AB- au O-

5. (a) Mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri, na ikitokea MSICHANA AMEJIFUNGULIA NYUMBANI au NJE YA HOSPITAL, ambako hakugundulika kwamba ana damu negative. Mtoto wa kwanza ataishi vizuri kabisa na afya nzuri. ila watoto wanaofata hawataweza kuishi au watakufa kabla hawajazaliwa kwa sababu

(b) Msichana mwenye negative blood group ( Rh-) yaani hana D antigen, alipojifungua mtoto wa kwanza mwili wake unakuwa sasa umeandaa kujikinga (antibodies kupambana na D antigen ( Rh +) kwa baadaye

• MTOTO WA PILI akitungwa mwili wa mama tayari una Antibodies dhidi ya Rh+ ( mtoto anazo hizi Rh+), hivyo matokeo yake ni kuwa seli nyekundu za mtoto zitashambuliwa na kufa.

• Mtoto akibahatika kuzaliwa hai, atapoteza uhai muda sio mrefu kwa vile anakuwa hana seli nyekundu za kusambaza damu mwilini.

6. Endapo Msichana huyu alijifungulia MTOTO WA KWANZA HOSPITAL, madaktari wanakuwa wameshajua kwamba ana damu negative, hivyo wanasaidiana na mmewe kufanya maandalizi ya sindano yenye dawa ( SIITAJI HAPA ) halafu msichana akijifungua tuu MTOTO WA KWANZA anachomwa hiyo sindano na akija kupata mimba baada atachomwa hiyo sindano wakati wa mimba na pindi anapojifungua.

Source: wellclinictz
 
Kichwa cha habari mkuu.. uhusino wa group la damu na kutopata ukimwi.. nijazie jazie hii mkuu kidogo napenda kufahamu?
 
Somo murua kabisa.......swali linakuja,unaweza kugundua uhalali wa mtoto kwa baba kwa kuangalia hayo makundi ya damu katika hatua ya awali kabla ya kwenda kwenye kipimo cha vinasaba?
 
Somo murua kabisa.......swali linakuja,unaweza kugundua uhalali wa mtoto kwa baba kwa kuangalia hayo makundi ya damu katika hatua ya awali kabla ya kwenda kwenye kipimo cha vinasaba?
Ndio inawezekana kabisa yani kwa kufuata mendelian principles lakini yenyewe ni prediction unacross kwanza ukishapata majibu 4 unachukua ya jinsia ya mtoto halafu unaenda kumpima damu

Tatizo la hii ni moja muda mwingine makundi yetu ya damu huwa yanafanana utakuta ww una A+ na huyo mwanaume ana A+ basi ukicross utapata majibu yale yale kama yako kumbe mimba ni ya mwingine
 
Waswahili utasikia " karogwa asibebe mimba au Kila mtoto afe*.
Kumbe uchawi elimu ya biologia!!! [emoji3]
Ipo hivyo hata ile ishu mtoto akizaliwa hapumui hadi anakufa na yenyewe ni swala la kibaolojia tu ila bado sijajua kama kuna njia ya kujikinga ile
 
Somo zuri mkuu, naomba kuuliza kazi ya hizo antigen A, B huwa ni ipi na je mtu mwenye damu ambayo cell haina antigen yoyote huwa nini kinatokea?
 
Kichwa cha habari mkuu.. uhusino wa group la damu na kutopata ukimwi.. nijazie jazie hii mkuu kidogo napenda kufahamu?
Hapo sijafahamu lakini watu wengi wenye hizi antigen huwa wanasumbuliwa sana na magonjwa kama hufahamu hebu chunguza watu wengi ambao hawana izo antigen A&B huwa wanaumwa umwa hovyo lakini wale ambao hawana O namaanisha wengi huwa wapo strong sana hawaumwi umwi hovyo
 
Somo zuri mkuu, naomba kuuliza kazi ya hizo antigen A, B huwa ni ipi na je mtu mwenye damu ambayo cell haina antigen yoyote huwa nini kinatokea?
Hizo antigen A&B ni protini zenyewe zipo tu kama mtu hana ndio wale wenye blood group O

Lakini wewe swali lako unauliza kuhusu rhesus factor Rh+ au Rh- sasa hizi ndio zina leta shida sasa
 
Kichwa cha habari mkuu.. uhusino wa group la damu na kutopata ukimwi.. nijazie jazie hii mkuu kidogo napenda kufahamu?

Nimepata kusikia sehemu kuwa kuna group fulani la damu ni gumu kidogo kuambukizwa magonjwa hususani magonjwa yanayoambukizwa mf -ukimwi.. yaani mtu mwenye group flani la damu akitembea na mtu mwenye virus vya ukimwi kwake inakuwa ngumu kupata ugonjwa huo je? Ni kweli.. kama ni kweli ni group? Gani? La damu na kwa nini? Ni gumu kupata mapgonjwa group hilo la damu.. kwako MKUU
 
Group hilo la damu ni O kwa sababu hawana iyo antigeni A, B au AB hao wenye O
Lakini sio kwa virusi vya ukimwi
 
Group hilo la damu ni O kwa sababu hawana iyo antigeni A, B au AB hao wenye O
Lakini sio kwa virusi vya ukimwi

Maana huku kwetu ukimwi mwingi sasa kuna jamaa zetu kama watatu wanawake zao tahabani kwa vitusi vya ukimwi wao wanajipapatua kuwa wamepime na hawana virus.. sasa nilipenda nijue kwa tahadhari maana wanapenda sana wanawake za watu..
 
Inabidi wapime mara 3 kila baada ya muda fulani maana unaweza kuwa na ukimwi halafu kwa dalili za awali usionekane
 
Back
Top Bottom