jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
- Thread starter
- #61
Si unaona hii habari Kibunango?
Especially pale nilipo highlight?
Sakata la mwafaka Zanzibar
2008-05-18 11:44:05
Na Simon Mhina
Chama cha Wananchi (CUF), kimesema kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kukitaka chama hicho kurejea kwenye meza ya mazungumzo na CCM, wanaichukulia kama porojo, vinginevyo ayatoe kimaandishi.
Kadhalika, Chama hicho kimesisitiza kuwa hakitakubali kamwe kukaa meza moja tena na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba kuzungumzia Mwafaka.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni Bw. Hamad Rashid Mohamed, alisema habari za Rais kuwaomba CUF warejee kwenye mazungumzo wamezisikia kwenye Redio na magazeti, hivyo hawajazitilia maanani.
Alisema hivi sasa CUF imeshachoka `kutapeliwa` kisiasa na CCM hivyo hawakubali maneno yoyote yasipopelekwa kwao kwa maandishi.
Alisema akiwa Mkuu wa Nchi, inashangaza kuona anatoa maagizo mazito yanayogusa ustawi wa Taifa, kupitia mlango wa nyuma.
Alisema Rais alikuwa na uwezo wa kuwasiliana nao moja kwa moja, badala ya kutoa maagizo hayo wakati anazungumza na Waziri anayeshughulikia mambo ya kimataifa wa Serikali ya Ufaransa aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
``Anavyosema CUF na CCM tukutane, wakati anazungumza na mfaransa huyo, alikuwa anamtuma aje atuambie au vipi?``alihoji.
Bw. Mohamed alisema kwa kiasi kikubwa CUF wanamheshimu mno Rais Kikwete na hawakusudii kupuuza wala kudharau mawazo yake.
Alisema ni kweli Rais akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu, anao wajibu wa kuhangaika ili kuhakikisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuwa ya amani.
``Tunamheshimu Rais Kikwete, lakini anapotoa maagizo makubwa kama hayo katika vyombo vya habari, kwa kweli tunabaki tunashangaa, maana hata majibu tunashindwa kutoa,``alisema.
Alisema angalau wakishapata waraka wa maandishi kutoka kwa Rais Kikwete wanaweza kujibu.
Hata hivyo, Bw. Mohamed alisisitiza kwamba mazungumzo hayo katika kiwango cha Makatibu wakuu, yameshapita.
Alisema Makatibu wakuu, wa CUF na CCM wamekaa mezani na kuchukua muda mrefu wa miezi 14, hivyo kikao chao hakiwezi tena kuwa na jipya.
Alisema japokuwa wakipata taarifa ya maandishi kutoka kwa Rais wataijadili, lakini ni wazi kwamba CUF haitakubali tena mazungumzo ya makatibu wakuu wa vyama hivyo.
``Iwapo atatuandikia, barua yake tutaitafakari vema, iwapo tu itataja watu wengine wakukutana na kuzungumza lakini si Seif na Makamba,``alisema Bw. Mohamed.
Alisema CUF kinaamini kwamba maelekezo atakayoyatoa Rais sasa ni Bw. Seif kukutana na Rais Karume.
Kuhusu madai ya CUF kuhusika na wananchi wa Pemba wanaotaka kisiwa hicho kijitenge, Bw. Mohamed alisema wananchi wote wana haki ya kutoa maoni yao.
Alisema eneo la Pemba pia kuna wanachama wa vyama vingine, kwa hiyo anaamini kati ya wananchi hao waliopeleka barua Umoja wa Mataifa kutoa madai hayo, wamo pia wanachama wa CCM.
Hata hivyo, kiongozi huyo alimshangaa Kada wa CCM Bw. Hiza Tambwe aliyekaririwa akisema wapemba hao ni wahaini, na wanapewa msukumo na CUF.
``Nataka umuulize Tambwe hivi wale wabunge 55 waliotaka iundwe Serikali ya Tanganyika walikuwa wa Chama gaini? Walikamatwa na kufikishwa Mahakamani?``alihoji.
Alisema kama kuna mtu ambaye ameigawa Zanzibar hadi hivi sasa ni Rais Aman Karume, ambaye ameunda Serikali ya upande mmoja.
Bw. Mohamed alisema hata katika ajenda namba tatu ya mazungumzo, wajumbe wote walikubaliana kwamba Karume ameigawa Zanzibar.
Alisema madai ya Tambwe kusema CUF ni chama cha vurugu, sio ya kujenga na wala maneno hayo hayana faida kwa CCM zaidi ya kuleta utengano.
``Kwanza hatujui hayo yalikuwa maneno ya CCM au ya Tambwe Hiza, sisi tumekaa na CCM meza moja kwa miezi 14, kwanini walijadiliana nasi mambo muhimu kama sisi ni magaidi?``alihoji.
Alisisitiza kwamba CUF kimeandikishwa kwa mujibu wa sheria, na hakijapata onyo lolote toka kwa Msajili wa vyama vya siasa kutokana na kukiuka misingi na kanuni za vyama vingi.
Aliionya CCM kwamba Tambwe atawafikisha pabaya kutokana na maneno yake yakufufua shari.
``Huku wanadai turejee kwenye meza ya mazungumzo, huku wanasema sisi ni magaidi, sasa tushike lipi?``alihoji.
- SOURCE: Nipashe
Haya sasa na hao waliodaiwa kuwa wahaini kuna CCM ndani?
Wanaoelewa watoe ufafanuzi..