Uhusiano uliopo kati ya kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe na tukio la jambazi

Hapana, mimi sijahukumu...

Tunachojaribu kufanya hapa ni kufikiri tu na kutoa description ya tukio lenyewe...

Kwa sababu huu ni ujambazi wa ajabu kidogo...

Na kumbuka maneno ya Rais Samia leo akizungumza na polisi kuwa;

"....Magaidi tunao, tunaishi nao mitaani mpaka sasa...."

Baada ya kauli hiyo tu, masaa machache tukio hilo linalosemekana la ujambazi likatokea...

Yaani ni kama tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi lilivyotokea September, 2017....

Rais Magufuli anapokea ripoti ya madini ya kina Prof Mruma huko DSM, akahutubia na kusema;

"....wote wanaopinga haya mambo (aliyoyaita kama vita ya uchumi) si wazalendo, ni wasaliti na askari mnajua msaliti katika vita hufanywaje...."

Ile Rais Magufuli anamaliza tu kutamka maneno hayo, kule Dodoma saa saba mchana kweupe katikati ya mji, Tundu Lissu akamiminiwa risasi 37 na "watu wasiojulikana", na kati ya hizo 16 zikazama mwilini lakini kimiujiza jamaa hakufa, yu hai mpaka Leo...!!

Kwa hiyo, ni lazima watu tuhoji kila tukio lisilo la kawaida linalotokea hapa nchini kwetu. Hili siyo la kawaida...!!
 
Mbona kama sijaona damu?
 
sijakuelewa mkuu kwamba majeshi hata mipaka kulindwa yaache ? na umejuaje kuwa ana uhusiano nao na kuwa wamekasirika?
Unauliza majibu mkuu, umewasikia mashuhuda lakini. MAGAIDI yapo Dar
 
View attachment 1907849
MaCCM hivi akili mlipeleka wapi..huyu ni JAMBAZI Ila Mbowe ni GAIDI. Nyie jifanyeni hamnazo tu. Majeshi mliopeleka msumbiji, mjiandae na visasi vya MAGAIDI.
Huyu ni kijana. Anakaa upanga. Wanaasili ya kisomalo
Babake Tajir. Wanaishi hapo. Hana akili timamu
Alisoma almutazir.akashindwa aliposjindwa wazazi wakampeleka kusoma dini. Hajarudi home hana cha kufanya baba ana silaha inashinda nyumbani... amechukua silaha ya baba akaenda kuchukua silaha ndogo ya baba akashambulia police wala rushwa goigigoi pale corner ya kwenda kwa vogogo masaki.anatumia akili ndogo sana.
Huo ugaidi upo wapi hapo
 
Uko sahihi
 
The palm tree mimi nakuunga mkono. Ni lazima tuwe na uwezo sio wa kuona vilivyo wazi bali kuona vulivyofichika.

Kuna kamchezo hapo

hawa watawala they can do anything.
 
Kweli. Thay can do anything. Say anything.
 
Kuwa mpole kwetu Sisi wenye idea kidogo ya ujasusi huyu jamaa anaweza asiwe gaidi wala agent wa issue yoyote inayohudisha serikali. Bali huenda kukawa na mambo ya kudhulumiana Kati yake na polisi so lengo likawa kulipa kisasi.
Kama watajaribu kuhusisha hili jambo na kesi mbowe itakuwa nikufeli Kwa ujasusi Kwa kiwango cha juu sana
 
Huyu ni kijana. Anakaa upanga. Wanaasili ya kisomalo
Babake Tajir. Wanaishi hapo. Hana akili timamu
MaCCM toka lini wakawa na akili , huo ndio Utimamu wa MaCCM wote, wanachoweza ni UGAIDI, kuteka , kutesa, na kuua watanzania. Mjumbe UVCCM yule.
CCM ni laana nchi hii.
 
Unasema huu ni ugaidi na kulinganisha na ugaidi wa Mbowe.
Nikuulize kwani Mbowe kamtuma huyu msomali?
Wewe ndiyo gaidi umemtuma huyo Msomali ili upate kuwabambikia kesi familia yake yote ukapore mgodi wao hapo mbeya
 
Atakuwa anawadai Polisiccm huenda kuna uonevu ulitendeka dhidi yake kaamua kulipa kisasi
 
Acha Acha Kuropoka,kwani umeambiwa na wale 6 waliojeruhiwa waemelazwa hospitali wote ni askari polisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…