Uhusiano unapovunjika inauma lakini kuna haya yafuatayo

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Ni sawa kuumia kwasababu mnakumbukumbu pamoja na mwenza wako ambazo huwezi kuzifuta mara moja na kuzisahau ghafla

Ila tambua kwamba mlipitia machungu pamoja wakati wa maisha yenu ya kimapenzi,hivyo hiyo iwe ni sababu ya kuku kumbusha kwamba,kuna wakati ambao mlishea maumivu pamoja,hivyo ni sehemu ya maisha

Tambua kuna kipindi mlielewana vizur sana na kufurahia maisha yenu ya mapenzi mpaka mkajihisi mpo katika dunia ya peke yenu,hivyo itoshe kujua kwamba maisha ni hatua,na ulipitia hatua hiyo

Kuna kipindi mlitiana moyo na kusonga mbele pamoja,hivyo mlipata uzoefu mkubwa sana katika mapenzi yenu,na iwe chachu ya kufanya hivyo katika penzi jipya

Vile vile fahamu kwamba uhusiano wako huo ambao sasa haupo tena,ulikufundisha kuyajua mambo mengi ambayo huku yajua hapo kabla na umepata uzoefu mpya

Kwahiyo sio kila uhusiano upo kudumu milele mwengine upo kukupa uzoefu wa mda mfupi na kukutayarisha kwa ajili ya uhusiano wa kudumu au wa muda mrefu

Tambua kuna mahusiano mengine yatakuja kukupa kila unachokihitaji huko mbele ya safari

Jua kwamba hayo maumivu ambayo unayo sasa hayata dumu milele hivyo hayo nayo yatapita,kuwa imara zaidi

Tambua kwamba utaendelea kusonga mbele na utazidi kuimarika zaidi siku baada ya siku

Jua kwamba watu unaokutana nao katika maisha wengine walipita tu kuwa sehemu ya maisha yako au kukamilisha kurasa za kitabu chako

Ni hayo tu!
 
Kuvunjika kwa mahusiano hakuumii kinachokufanya upate maumivu ni FIKRA zako ambazo zinatafsiri kuvunjika kwa mahusiano lazima upate maumivu hapo ndo tatizo lipo kwa wengi.
 
Kuvunjika kwa mahusiano hakuumii kinachokufanya upate maumivu ni FIKRA zako ambazo zinatafsiri kuvunjika kwa mahusiano lazima upate maumivu hapo ndo tatizo lipo kwa wengi.
Ni kweli kabisa kuna ambao wanaweza kuhandle situation na kusonga mbele mapema ila wenye shida mingi ni wale ambao wanachukua mda kukubali ukweli kwamba it's over
 
Mausiano si kwa kilamutu wengine inabidi wawe single na maisha yataenda vizuri tu.
 
Mausiano si kwa kilamutu wengine inabidi wawe single na maisha yataenda vizuri tu.
Unapoint boss usikilizwe,,,ni kweli kabisa wengine hawakuumbwa kupambana na changamoto za mapenzi,ndio utasikia wameua na kujiua,very true
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…