Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Ila tambua kwamba mlipitia machungu pamoja wakati wa maisha yenu ya kimapenzi,hivyo hiyo iwe ni sababu ya kuku kumbusha kwamba,kuna wakati ambao mlishea maumivu pamoja,hivyo ni sehemu ya maisha
Tambua kuna kipindi mlielewana vizur sana na kufurahia maisha yenu ya mapenzi mpaka mkajihisi mpo katika dunia ya peke yenu,hivyo itoshe kujua kwamba maisha ni hatua,na ulipitia hatua hiyo
Kuna kipindi mlitiana moyo na kusonga mbele pamoja,hivyo mlipata uzoefu mkubwa sana katika mapenzi yenu,na iwe chachu ya kufanya hivyo katika penzi jipya
Vile vile fahamu kwamba uhusiano wako huo ambao sasa haupo tena,ulikufundisha kuyajua mambo mengi ambayo huku yajua hapo kabla na umepata uzoefu mpya
Kwahiyo sio kila uhusiano upo kudumu milele mwengine upo kukupa uzoefu wa mda mfupi na kukutayarisha kwa ajili ya uhusiano wa kudumu au wa muda mrefu
Tambua kuna mahusiano mengine yatakuja kukupa kila unachokihitaji huko mbele ya safari
Jua kwamba hayo maumivu ambayo unayo sasa hayata dumu milele hivyo hayo nayo yatapita,kuwa imara zaidi
Tambua kwamba utaendelea kusonga mbele na utazidi kuimarika zaidi siku baada ya siku
Jua kwamba watu unaokutana nao katika maisha wengine walipita tu kuwa sehemu ya maisha yako au kukamilisha kurasa za kitabu chako
Ni hayo tu!