Uhusiano wa dawa kutokufanya kazi na maziwa

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Nimeamua kuiweka hii thread huku kwa faida ya wote maana huku panatembelewa na wengi.

Mara nyingi utasikia watu wanasema nimeahirisha kunywa dawa maana asubuhi nilikunywa maziwa.

Je, ni kweli ukinywa dawa na maziwa hazifanyi kazi?

Au ndio tuseme kuna aina ya dawa hazikubaliani na maziwa.Kama zipo ni zipi?

Naombeni wenye taaluma ya madawa watujuze
 
Kwa njinsi mi ninavyojua ili dawa iweze kuingia mwilini lazima ikifika tumboni ifonzwe kwenda kwenye mfumo wa mzunguko wa damu,

Maziwa yanafonzwa haraka na mapema kuliko kitu kingine kutokana na nature yake(fat na protein)

Hivyo basi mtu akimeza dawa na kunywa maziwa,itachukua muda sana dawa kuingia mwilini,because maziwa yanapewa priority kwanza kuingia mwilini.

Pia chakula kina muda wake wa kukaa tumboni,so kisipofonzwa kwa huo muda hutolewa kama mabakia.

Ndio maana mtu akinywa sumu anapewa maziwa kwanza ili simu isienee mwilini hata kama ikiingia itakuwa kidogo baadae hupelekwa hospital ili kuitoa hiyo sumu kwa njia mbalimbali,

Umenipata?
 
Kama umesoma chemistry, utakumbuka kitu kinaitwa electrochemical series (table), kwa kifupi maziwa yana react na baadhi ya dawa kwa mfano rangi mbili(tetracycline) na kuunda kitu kingine kabisa ambacho hakiwezi kuwa absorbed kwenye utumbo mdogo
 
Sio dawa zote hazikubaliani na maziwa.
Dawa nyingi zina acid na maziwa yana base.
Acid+base=salt+water. Huko tumboni ukinywa dawa(acid) kisha ukanywa maziwa kinatokea chumvi na maji, kwa hiyo dawa inapotezwa kabisa.
Ndio maana mtu akinywa sumu(acid) tunampa maziwa au tunamkologea majivu tunamywesha ili kuiua hiyo acid(sumu).
NB: mimi sio mwanasayansi wa darasani ni mwanasayansi wa mtaani. Sayansi yangu ni ya vitendo zaidi....
 
hata kwenye pombe vs maziwa == 0
Nasikia mama anayenyonyesha akikamulia maziwa kwenye bilauri ya bia ...mnywaji akiinywa anatapika na kuacha pombee moja kwa moja
 
Sio dawa zote hazikubaliani na maziwa.
Dawa nyingi zina acid na maziwa yana base.
Acid+base=salt+water. Huko tumboni ukinywa dawa(acid) kisha ukanywa maziwa kinatokea chumvi na maji, kwa hiyo dawa inapotezwa kabisa.
Ndio maana mtu akinywa sumu(acid) tunampa maziwa au tunamkologea majivu tunamywesha ili kuiua hiyo acid(sumu).
NB: mimi sio mwanasayansi wa darasani ni mwanasayansi wa mtaani. Sayansi yangu ni ya vitendo zaidi....
Umejitahidi sana, kwa kukuongezea tu kidogo alkali ni sumu kali sana kuliko acid
 
Sio dawa zote hazikubaliani na maziwa.
Dawa nyingi zina acid na maziwa yana base.
Acid+base=salt+water. Huko tumboni ukinywa dawa(acid) kisha ukanywa maziwa kinatokea chumvi na maji, kwa hiyo dawa inapotezwa kabisa.
Ndio maana mtu akinywa sumu(acid) tunampa maziwa au tunamkologea majivu tunamywesha ili kuiua hiyo acid(sumu).
NB: mimi sio mwanasayansi wa darasani ni mwanasayansi wa mtaani. Sayansi yangu ni ya vitendo zaidi....
Ila si wongo umejitahidi kueleza kisayansi.Ila nikuambie tu sio sumu zote ni asidi.Sumu zingine ni alkaloids mfano quinine,caffeine n.k
 
Sawa mkuu, ngoja tuwasikie na wataalam wengine.
 
Kwa njinsi mi ninavyojua ili dawa iweze kuingia mwilini lazima ikifika tumboni ifonzwe kwenda kwenye mfumo wa mzunguko wa damu,

Maziwa yanafonzwa haraka na mapema kuliko kitu kingine kutokana na nature yake(fat na protein)

Hivyo basi mtu akimeza dawa na kunywa maziwa,itachukua muda sana dawa kuingia mwilini,because maziwa yanapewa priority kwanza kuingia mwilini.

Pia chakula kina muda wake wa kukaa tumboni,so kisipofonzwa kwa huo muda hutolewa kama mabakia.

Ndio maana mtu akinywa sumu anapewa maziwa kwanza ili simu isienee mwilini hata kama ikiingia itakuwa kidogo baadae hupelekwa hospital ili kuitoa hiyo sumu kwa njia mbalimbali,

Umenipata?
Umejitahidi but sio kweli kwa asilimia nyingi.

Kuna dawa nyingine ukinywa maziwa ndo umeziongezea kupiga kazi vzr zaidi, mf Alu. Hii unashauriwa unywe na maziwa ndo ifanye tiba vzr.

Absorption ya dawa inategemeana na formation yake, mf kuna topical drugs, mf tubes nyingi, kuna zinazofanya absorption kwenye airways mf aerosols kama Salbutamol, pia kuna zinazofanya absorption kupitia chini ya ulimi, kwenye anus like Anusol, nyingine kwenye uke mf pessaries. Zipo pia huwa absorbed kwenye njia ya chakula (sio tumboni tu) mf solid and semi solid drugs kama tablets, suspensions, syrups and capsules.

Sasa dawa hizi zipo za aina mbali mbali na mifumo ya utendaji mbali mbali. Maziwa huwa na kitu tunakiita "contraindication" na baadhi ya dawa, ndiyo maana maana utashauriwa usitumie maziwa wakati wa matumizi. Nyingins hazina shida kabisa.

Case hii ni same to pombe.

Pia si kila sumu utai-netralize na maziwa, nyingine ukiweka maziwa ndo inakuua vizuri na kirahisi (ni somo refu hili)

Ushauri: Kabla ya kutumia dawa muulize mfamasia ni kipi hakifai kunywa au kula na kitaharibu dawa.
 
Jumong umejibu deeply kitaalamu nahisi utakuwa mtaalamu wa fani hii
 
Kama unataka kujifunza tafuta kitu inaitwa drugs interaction ndani yake utakutana na kitu inaitwa drug-nutrient/food interaction utaielewa kwa undani.
Nimeamua kuiweka hii thread huku kwa faida ya wote maana huku panatembelewa na wengi.

Mara nyingi utasikia watu wanasema nimeahirisha kunywa dawa maana asubuhi nilikunywa maziwa.

Je, ni kweli ukinywa dawa na maziwa hazifanyi kazi?

Au ndio tuseme kuna aina ya dawa hazikubaliani na maziwa.Kama zipo ni zipi?

Naombeni wenye taaluma ya madawa watujuze
 
Cheki majibu mengine humo.
 
Back
Top Bottom