Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Kengele ya Mwaka Mpya wa 2025 imelia, na kuashiria mwisho wa mwaka 2024. Katika mwaka uliopita, uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika umeendelezwa zaidi.
Mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka 2024, Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika Beijing.
Takriban wageni 6,000, wakiwemo viongozi wa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kibalozi na China, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, walikutana mjini Beijing.
Washiriki hao walijadili kwa kina uhusiano na ushirikiano kati ya China na Afrika kufuatia kauli mbiu ya kuangazia kaulimbiu ya “Kuendeleza Usasa kwa pamoja, Kujenga Jumuiya ya Hali ya Juu yenye Hatma ya Pamoja ya China na Afrika”.
Katika mkutano huo, China ilitangaza kuinua uhusiano kati yake na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kibalozi na China kuwa kiwango cha uhusiano wa kimkakati, na uhusiano kati ya China na Afrika kuwa Jumuiya yenye Hatma ya Pamoja kwa Siku zote katika Zama Mpya.
Mkutano huo pia ulitangaza mapendekezo sita na hatua kumi za kiwenzi, ili kukuza zaidi uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika.
Mwezi Novemba mwaka 2024, Maonesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE) yalifanyika mjini Shanghai. Bidhaa mbalimbali za Afrika kama parachichi za Afrika Kusini, asali ya Tanzania na sukari maalum ya Mauritius zilioneshwa na kuwavutia wateja wengi.
Ikiwa ni nchi mwanachama wa asili wa Dunia ya Kusini, China siku zote inasaidia nchi zinazoendelea, haswa nchi za Afrika kuingia katika soko kubwa la China, ili zinufaike na maendeleo ya China.
Katika mwezi huo huo, Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Minyororo ya Ugavi ya China yalifanyika Beijing. Ili kutimiza ahadi iliyotolewa kwenye Mkutano wa Beijing wa FOCAC, China iliongeza uungaji mkono kwa makampuni ya Afrika kushiriki katika maonesho hayo na kuyapa mabanda na huduma za bure.
Tangu kuingia katika zama mpya, China na Afrika zimeendelea kuimarisha ushirikiano katika mnyororo wa viwanda, na kuunganisha pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, na mikakati ya maendeleo ya nchi za Afrika.
Kuanzia Desemba 1, 2024, China imesamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa zote za nchi 33 za Afrika, ili kuzisaidia nchi hizo kujiendeleza na kupunguza umaskini. Hatua hiyo inaonesha nia ya China ya kufungua mlango na kuwa mwenzi thabiti wa nchi za Afrika katika mchakato wa kupata maendeleo.
Mnamo mwezi Machi mwaka 2024, wasomi kutoka China na nchi 49 za Afrika walitoa “Makubaliano ya Dar es Salaam kati ya China na Afrika”, na kuonesha kuwa nchi za Afrika zina shauku ya kuendeleza uchumi kwa uhuru na kujiamua, na kutaka kutafuta njia inayofaa zaidi ya kutimiza mambo ya kisasa barani Afrika.
Katika mwaka mpya wa 2025, China na Afrika zitaendelea kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kirafiki kati yao, ili kupata mafanikio mapya ya pamoja.