SoC01 Uhusiano wa Siasa, Jamii na Uchumi

SoC01 Uhusiano wa Siasa, Jamii na Uchumi

Stories of Change - 2021 Competition

MaraVeteran

New Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
3
Reaction score
4
Maisha yana mitazamo mikuu mitatu, ambayo ni mtazamo wa kisiasa, mtazamo wa kijamii na mtazamo wa kiuchumi. Mitazamo yote mitatu kwa kila mmoja wapo huweza kuungana na mwingine ili kuzalisha mtazamo mdogo.

Kwa mfano Siasa ikiunganishwa na jamii huzalisha siasa jamii, uchumi ikiunganishwa na jamii huzalisha uchumijamii pia Siasa ikiunganishwa na uchumi huzalisha uchumi Siasa. Mitazamo yote hii ni Sawa na ina uwiyano sawa katika maisha, Hii inamaanisha kwamba kama mtazamo mmoja utakuwa mbovu basi mitazamo mingine itakuwa mibovu pia. Udadavuzi wa mlinganyo huu ni kama ifuatavyo:

Siasa

Huu mtazamo hudhibiti masuala yote ya kiutawala, uongozi, usimamizi na udhibiti wa shughuli miongoni mwa kundi la viumbe au binadam. Misingi ya Siasa huambatana na migawanyo ya majukumu katika kundi au jamii. Mtazamo huu huanzia katika ngazi ya familia, jamii Hadi taifa. Yaani kama ilivyo kwenye familia za jamii za mfumo dume, Baba huwa kiongozi wa familia au jamii za mfumo jike mama huwa kwa kawaida ni kiongozi wa familia. Jamii na Taifa pia huwa na taratibu zake za uongozi na usimamizi.

Uchumi

Huu mtazamo unajumuisha Taratibu zote za uzalishaji, utumiaji na udhibiti wa rasilimali zinazopatikana kwenye himaya ya jamii, Hii ni pamoja na viwanda, aridhi, madini, ubadilishanaji wa bidhaa (biashara), thamani ya fedha n.k. Uchumi ni muhimu katika kuendeleza jamii na kuimarisha, maana jamii ikiyumba kiuchumi hata jamii na Siasa havitakuwa Sawa.

Jamii

Huu ni mtazamo muhimu ambao hujumuisha sifa zote za kundi au vinavyopatikana katika kundi la watu. Hii ni pamoja na Hali za kimaisha, miundombinu, Huduma muhimu, elimu, utamaduni, lugha, ustaalabu, mahusiano na jamii zingine sambamba na historia ya jamii. Mtazamo huu ni muhimu kwa kuwa ndiyo unagusa watu moja kwa moja.

Maisha na mitazamo yake pamoja na maendeleo vinaweza kuelezewa kwa kutumia mfano wa basi linalosafili barabarani. Basi linakuwa kama Taifa, barabara ni dira, mafuta/nishati ni uchumi dereva na kondakta wao ni siasa na mfumo wa basi na abilia ni jamii.

Hivyo basi, jamii (basi na wasafiri), Uchumi (nishati au Mafuta), Siasa (dereva na kondakta) vyote hutegemeana. Kwa maana kwamba Basi na abilia (jamii) pamoja na Kondakta na dereva (Siasa) hawawezi kuondoka kama hapana nishati au Mafuta (uchumi). Vivyo hivyo jamii (basi na abilia) pamoja na Nishati au Mafuta (uchumi), haviwezi saidia basi (Taifa) kujongea (maendeleo) bila ya kuwepo kwa dereva (Siasa) mzuri. Endapo dereva atakuwa mlevi au kilema (siasa mibovu) itapelekea taifa (basi) kupata ajali (machafuko na uasi) hatimae kuhalibu mfumo wa jamii (basi) kama vile taa (elimu), Magurudumu(sera na falisafa) na usukani (katiba) na hivyo kukwamisha safari (malengo). Na Basi likijazwa Mafuta (uchumi) na dereva mzuri (Siasa) ila basi likawa na hitlafu au ubovu basi safari itakwama.

Kwa kuhitimisha, hakuna mtazamo ulio bora kuliko mwingine Bali mitazamo yote ni Sawa na inategemeana, kwa maana kwamba hakuna uchumi imara palipo na jamii mbovu (isiyo na maadili, elimu duni, njaa na rushwa, maradhi), hakuna Siasa safi kwenye jamii masikini maana kila mwanajamii atahitaji maslahi binafsi.

Mitazamo hii lazima ilingane ili kuleta uwiyano sawa katika maisha na kusukuma maendeleo, Uchumi ukipewa nguvu zaidi basi watu wataumia kwa kupoteza haki za msingi, Siasa ikipewa kipaumbele jamii itasahaulika kwani miundombinu na Huduma muhimu haitazingatiwa. Siasa pekee si maisha, uchumi pekee si maisha, jamii pekee haitoshi kuwa maisha, bali vyote kwa pamoja hutengeneza maisha ila kimoja kikisimama pekee ni mtazamo wa maisha
 
Upvote 6
Ulichokisema kinadharia ni sawa.

Lakini kivitendo nadhani mambo yapo more complicated.
 
Ulichokisema kinadharia ni sawa.

Lakini kivitendo nadhani mambo yapo more complicated.
Hapo ndipo changamoto ilipo, hata maisha yetu ni mabovu kwa kuwa mitazamo ya maisha yetu ni mibovu na hii imetokea pale tuliposhindwa kubalance mtazamo mmoja ukapewa nguvu na matokeo Ndo haya.
 
Back
Top Bottom