Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunongoneze basi mkuu.. ni ipiMie ni mdau tangia enzi za Dar hot-wire!
ID yangu ya zamani ipo na inatumika
Naondoa stress kwa ID mpya
James Jason
Challenge "B"
Wanaotaka niandike hadi kumaliza sehemu yote ya 13 waweke like kwenye post ya Challenge "A" hapo juu.
Watakaoshinda hadi ni wenye likes nyingi kwenye post husika
Mwisho wa kupiga like kwa challenge hii ni saa tatu kamili leo usiku kwa saa za Africa Mashariki.
James Jason
James Jason
Baba naomba zile za kula tunda kimasihara uziweke hapa. Maana kama unavyofaham ule uzi ulivyomrefu tunahangaika kuipata post yako. Nakuomba baba kwa unyenyekevu uoilete hapa.Bado sana
Sijapeleka posa
Itaishia nitakapozaa naye mtoto wa kwanza 1984, sasa ni 1982
Kuna mengi ya kujifunza kwa vijana
Kwa wakongwe ni kumbukizi nzuri pia.
Endeleeni 'kupiga' LIKEs ziniondolee maumivu ya kufinywa na kusukumwa sukumwa mabegani
The More the likes, the more the writting moral.
James Jason
Vespa na batavuzi ni tofauti,batavuzi zilikuwa na pedeli na vespa ilikuwa sharti upinde kiuno wakati wa kuendesha ili kuibalance kwani injini ilifungwa pembeni
SEHEMU YA 13 - A
*******************
Zilipita wiki mbili bila kuonana na kipenzi changu Hamida, niliendeleza ule utaratibu wa kufuata juisi mara mbili kwa wiki labda nitaonana na Hamida, lakini wapi. Sikuwa na sababu ya kuwauliza mle ndani kwa maana kilichokuwa kinasababisha tukutane mara kwa mara kilimalizika, maalim wa kunifundisha alikuwa ameshapatika na niliendelea vyema na msomo ya awli ya dini.
Nilitamani nimuandikie barua lakini ningeandika anuani gani, nilitamani nimpigie simu lakini sikujuwa yuko wapi. Kuna siku nilienda posta (sikuhizi posta ya zamani- baharini, Dar) nikanunua 'post card' nzuri yenye ujumbe 'I miss you', ina picha ya ua zuri kwa mbele na nyuma ni sehemu ya kuandika ujumbe mfupi.
Tayari katika masomo yangu ya dini nilikuwa nimehifadhi sura kadhaa za juzuu amma (juzuu ya 30 katika mpangilio wa Qur'an tukufu), hivyo maalimu alianza kunikazania kunifundisha mambo mengine muhimu. Hakika niliyafurahia mafundisho kwa kupata uelewa na ufafanuzi wa mambo mengi ambayo mtaani niliyasikia tofauti.
Mavazi yangu baada ya kazi yalibadilika, niliongeza kanzu nyingine ya rangi khaki kwa mbali, ikawa kila baada ya muda wa kazi navaa kanzu na kuendana na maadili ya dini.
Zile chupa pombe kali za nyumbani sikuendelea kunywa, lakini mziki sikuweza kuacha kusikikiza ama kwenda dansi DDC mara moja.
***********
Afisini kwangu pia nilibadilisha mienendo yangu hadi Marry akawa 'ananiogopa' kuniomba ‘nimsaidie’
"Ama kweli, Hamida amekubadilisha" alikuwa akipumua kwa kusema maneno hayo.
Hali ya upatikanaji wa bidhaa kwa ajili ya maduka ya ushirika ilizidi kudorora kutokana na hali ngumu ya nchi kiuchumi, hivyo ilibidi kuanza kugawa bidhaa kwa utaratibu maalum kubana bajeti kama ilivyoelekezwa na mamlaka.
Nilifanya uadilifu sana kuweka utaratibu wa maduka kupata mgao wa bidhaa, kila mtu alikuwa anafurahia lakini changamoto zilikuwa kwenye walaji wa mwisho yaani madukani kwenyewe.
Wiki ya nne ilivyofika uvumikivu ukanishinda, wakati napokea juisi kutoka kwa mama Fungameza, yule mama wa kiafrika ndani ya nyumba ya mzee Burhani nilimuuliza...
"Hamida kaolewa?"
"Bado hajaolewa, Hamida bado amebaki na msimamo wake wa kukataa kuolewa Oman, shangazi yake pia anamsimamia hivi walikuwa na kikao wiki kama siku 26 au 27 hivi zilizopita na shangazi yake aligombana na mzee Burhani kwa nini wanataka kumtesa binti kwa kumuoza kwa mzee ilhali vijana wengi wapo, hivyo aliamua kuondoka na Hamida kwenda Msasani, lakini nasikia yupo Unguja hivi sasa"
Nilipata faraja kidogo lakini bado sikuwa najuwa nifanyeje ili nimuone tena.
Hamida alikuwa amenikaa moyoni, sioni wanawake wengine tena, lakini nikawa najipa moyo kuwa kwa kuwa ana namba ya simu ya nyumbani ipo siku atanipigia.
Moja katika mafundisho ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimwendee) ni kuwa na subira katika mambo, kwani Allah yupo pamoja na wenye kusubiri. Nilijipa matumaini.
Moyo wangu uliendelea kujisafisha kwa mafundisho ya dini sasa nikawa sikosi katika madarada (vikao) vya masomo baada ya swala ya magharibi hadi iingiapo swala ya isha, uvivu wa kuamka alfajiri kwa ajili ya ibada ukaanza kupungua kidogo kidogo, siku za mwisho wa juma nilikuwa naenda Bagamoyo maeneo ya Sanzale ambapo nilinunua shamba kutoka kwa mzee Athumani. Pickup yangu ikawa inanisaidia kubeba mihogo na nazi zilizofuliwa (kuondolewa maganda) na kuja nazo Dar kuziuza na kujiwekea akiba katika benki ya NBC.
Kazini nilikuwa natembelewa na mabosi wangu mara ka mara kwa kuwa katika eneo langu hapakuwa na malalamiko kutoka maduka ya ushirika yanayonizunguka, hivyo walikuwa wanakuja kujifunza mbinu ninazotumia.
Pale Shibamu nikawa sionekani mara kwa mara isipokuwa siku moja moja ambazo mara nyingi ilikuwa Ijumaa ama Jumamosi kama sikwenda Bagamoyo shambani. Wale wazee waliendelea kunipa mafundisho ya dini kwa njia ya maongezi na walikuwa wananipenda sana (sijui kwa sababu ya round za kahawa!)
**********
"Grrriiiin griiiin, Grrriiiin grrrin"
Simu ya nyumbani iliita, wakati huo nilikuwa nimejilaza kitandani, saa ya mkononi ambayo sikuwa nimeivua bado, ilionesha ni saa tatu kasoro usiku.
Ndio nilikuwa nimetoka masjid Nuur kwa ajili ya ibada ya isha, hata kanzu nilikuwa sijavua, nilikuwa nahisi uchovu fulani hivi hivyo nilijiegesha kitandani miguu ikiwa chini.
"Halo"
Nilisema kwa sauti nzito baada ya kupokea.
"Saaleko!"
Sauti laini iliyolegea kutoka upande wa pili ilisikika. Haikuwa sauti ya Hamida...
"Wa aleikum salaam wa rahmatullah wa barakatu"
Nilijibu kwa kirefu maana Maalim Juma aliniambia nikijibu hivyo nitapata faida tatu, ilhali aliyetoa kwa ufupi atapata faida moja.
"Mtume (Rehema na Amani zimwendee) ametuusia tukitaka kupendana basi tuwe tunasalimiana..."
Sauti ya Maalim Juma ilinijia mara moja kichwani.
"Hamjambo jambo, habari za huko ,mmeshindaje?"
Sauti ile ya upande wa pili iliuliza maswali mfululizo.
Nilimjibu kuwa sijambo.
"Hapo ni kwa bwana Jamaal?"
Aliuliza tena.
"Ndiyo, naomba nikusaidie"
Nilisema kwa utaratibu huku kichwani kikijaribu kutafuta sauti hii ni ya nani bila kupata majawabu.
"Mie ni ma-Mkuu wake Hamida, wamfahamu eeh!"
Ile sauti ilisema.
"Naam, namfahamu, yupo wapi Hamida?"
Nilimuuliza.
"Hamida nipo naye huku Migombani Unguja wiki ya tatu sasa"
Alisita kisha akaendelea
"Hamida ametueleza kuhusu wewe, lakini mie na ndugunzangu wengine tunataka tukuone, hivyo fanya ufanyavyo jumamosi ijayo uje Unguja, sie tutakupokea bandarini"
"Naomba kuongea na Hamida"
Niliongea nikiwa na wasiwasi kidogo, hii ni nini tena!
"Hajarejea bado, walitoka na wenzie kwenda forodhani, ndio mida yao hii ya kurudi lakini"
Sauti ile ilisikika.
Haikuwa sauti ya ukali, wala ya kuonya. Hii kidogo iliniondolea hofu ya kuingia mtego nisioujua.
"Basi akirudi mwambie anipigie"
Nilisema.
"Haina tabu, ushafaham, maana aliniachia namba akisema akirudi tukupigie mie ndiyo nikajaribu kama namba hiyo inafanya kazi, kwa kuwa nimeshafaham basi akirejea tu n'takupigia tena, ushafaham?"
Alisema.
"Sawa, basi nasubiri simu hiyo"
Nilisema, kisha naye akasema
"In shaa Allah"
Halafu akakata simu.
Ilikuwa siku ya Jumanne, nikawa nawaza je hiyo Jumamosi niende nisiende, hatimaye nikapata jibu kwamba kesho usiku niende kwa mzee Katibu Kata ili kumuelezea taarifa hii.
Mara kwa mara nilikuwa nampatia mrejesho kuhusu hatua nilizopiga kuhusu azma ya kumposa Hamida ingawaje sikuelezea habari za ujio wake mara mbili kwangu.
***
Saa nne kasoro robo usiku simu ikaita tena.
"Halo"
Nilipokea
"Assalaam aleikum"
Sauti ya Hamida ikisikika
"Oh, Hamida, wa aleikum salaam wa rahmatullah wa barakatu"
Nilisema kwa bashasha.
"Habari za siku tele, hujambo?"
Alisema huku akicheka chinichini
"Ndiyo nini kunitesa kijana mwenzio!"
Nililalama badala ya kujibu swali lake.
"Pole Jamaal, lakini usijali, tutaonana tena, si utakuja Jumamosi?"
Aliuliza
"Eeee nitawajibu kesho jioni, hebu nipatie namba ya hapo"
Enzi hizo, ilikuwa huwezi kuona namba ya simu ya anayekupigia maana simu hazikuwa zina ‘display’.
Alinitajia nami nikaiandika kwenye sehemu ya kuandikia namba za simu kwenye 'directory' iliyokuwepo.
"Nitafurahi ukija, kwa sababu ndiyo itakuwa njia nyepesi ya wewe kuendelea na azma yako kama ulivyosema"
Alisisitiza Hamida
Sikutaka kumuhoji mengi kwa siku hiyo, lakini nilifurahi sana kupata namna ya kuwasiliana naye.
Tuliongea kiasi kisha tukakata simu. Nililala kwa furaha sana siku hiyo.
***
Baada ya kutoka kazini na darasani, usiku nilienda kwa mzee Katibu Kata, nilitumia batavuz kwa kuwa kuna chochoro nyingi kabla ya kufika kwake, Mwananyamala - Ali maua.
Nilimuelezea yaliyojili naye akanishauri, kama nataka kutimiza azma yangu basi nisisite kwenda...
"Hamida tayari ana zaidi ya miaka 18, hivyo usiwe na wasiwasi, pili kama kuna lolote, jambo 'baya' wanaloweza kufanya ni kuwafungisheni ndoa ya haraka haraka, kitu ambacho ndiyo malengo yako, hivyo kesho mapema uende bandarini ukakate tikiti mapema usije ukapata sehemu mbaya maana huwa inajaza sana siku za mwisho wa Juma maana itaenda hadi Pemba..."
Alisema mzee Katibu Kata.
Nilishiba maelezo yake, tukala chakula cha usiku pamoja kisha nikaaga na kuondoka hadi nyumbani.
***
Nilifika afisi za kukatisha tikiti za MV Mapinduzi majira ya saa nne hivi, nikapata tikiti ya daraja la pili kisha nikapitia afisi za airt Tanzania pale mtaa wa ohio na Bustani kufanya utaratibubwa kurudi, kisha nikarejea kazini.
"Sikuhizi unanukia vizuri"
Marry hakuacha kutupia madogo ya mbali
Nilikuwa nimebadili manukato, sasa nilianza kutumia 'al oud' kutoka U.A.E.
Manukato yalikuwa yametulia sana, hata baada ya kufua nguo, ukiipiga pasi utayasikia tena kama vile ndio kwanza umeipulizia.
Nilianza kufunga ndevu chini ya kidevu (low cut) na kupunguza mustachi (moustache)
Kofia ya mkono sasa ilianza kuwa kawaida kwangu hata nikiwa ofisini, nilianza kufurahia maisha ndani ya uislamu.
Mzee Katibu Kata alinipa kitabu kidogo chenye muongozo ya namna ya kujiombea kwa Mwenyezi Mungu mambo mbalimbali, katika safari yangu hii ya kwenda Unguja nilisoma sana dua za kunilinda na ubaya, ubaya utakanao na binadamu na utokanao na viumbe wengine tunaowaona na tusiowaona, tunaowajuwa na tusiowajuwa. Hofu yote ya safari ilinitoka nikiamini nina ulinzi wa Muumba.
"Ahsante, nawe uje katika uislamu unukie, Uislamu ni Amani, ni usafi, ni mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu"
Nilimjibu Marry huku nikiongeza na somo kidogo.
"Jumamosi natarajia kwenda kufunga pamvu (uchumba) Unguja"
Nilichombeza kwa Marry
"Unguja tena?! Si uliniambia ni binti wa Magomeni!?"
Alihoji na kushangaa
"Au umepata mwingine, maana we nawe!"
Alisema huku akichukuwa makaratasi fulani mezani kwangu ili atoke nayo...
"Ni yule yule, harakati kamili zikianza utakuwemo kwenye kamati ya maandalizi"
Nilimwambia.
**
Siku ya alhamisi iliishia na Ijumaa ikafika. Ijumaa huanza alhamisi jioni baada ya jua kuzama. Hivyo siku kwa mujibu wa dini ya Kiislam huishia na kuanzia Magharibi na siyo saa sita usiku.
Baada ya ibada ya saa mbili usiku na kupata chakula Butiama Restaurant, nilirudi nyumbani na kuanza kupiga simu Unguja...
"Halo saaleku"
Sauti kutoka upande wa pili ilisikika, ilikuwa sauti ya binti mdogo kwa kukadiria chini ya miaka kumi.
"Wa aleikum salaam, nipe niongee na ma-Mkuu au Hamida"
Nilisema kwa upole.
"Bibi antoka na anti Hamida answali ndani"
Kale katoto kalijibu.
"Sawa, nitapiga baada ya dakika tano, kwa herieee!"
Nikakata simu hata kabla hajajibu.
Baada ya dakika tatu hivi nikasikia simu inaita, nikajuwa huyu moja kwa moja ni Hamida, nilivyopokea nikaanza...
"Cheichei bibie!"
"Cheichei Bwana"
Alijibu kwa kubana pua kidogo, wote tukacheka sana!
"Enhe, habari za kutokea jana?"
Nilimuuliza baada ya kuacha kufurahi kwa kucheka
"Sie wazima huko, hofu kwenu huko bara, huku twala boflo na chai saa hii, haya mwatunyimani huko?
Aliongea kama Wazanzibari wanavyoongea.
“Wallah sikupata kuwaza kuwa unaweza kuongea namna hiyo, mnawezaje kulegeza ulimi hivyo?"
Niliuliza
"Ndio uje tukupe urojo, chaza, ngisi, vipoopoo uone kama nawe hujaanza kubadilika"
Tukacheka tena kiasi
"Kesho tunakusubiri kwa hamu, usikose kuja..."
Aliniambia hata kabla sijampa jibu langu la kwamba nitaenda ama la.
"Kwa ajili yako, nitakuja Hamida, ondoa shaka, nimeshafanya mengi kwa ajili yako, hivyo Jumapili asubuhi usikose kunipokea, sijawahi kufika Unguja", Nilisema.
Wakati huo, meli ya Mv Mapinduzi ilikuwa ikitoka bandarini Dar saa kumi na mbili jioni, na kufika Unguja alfajiri. Hivyo ningefika Unguja Jumapili asubuhi na jioni yake nilitarajia kurudi kwa ndege ambayo ingeondoka Unguja saa nne usiku kuelekea Pemba, kisha Tanga halafu Dar.
"Ukija mpenzi utakuwa umefanya vizuri sana, maana aunt wa Msasani Mumewe ana rafiki askari kanzu, ndiyo maana nilikuambia utachunguzwa, hivyo mambo yako yote aunt na mumewe wanayo, mie wamenidokeza tu lakini hayakuwa mageni kwangu kwa kuwa ulishaniambia..."
Akasita kidogo kisha akaendelea
"Mengi tutaongea ukija huku, lakini ma-Mkuu na wenziwe wanataka kukuona. Niliwaonesha picha zako lakini wanataka wakuone ana kwa ana wapate kujenga hoja kwa mzee Burhan"
"Picha zangu tena!? Umezichukuwa lini ?" Nilihoji kwa kushangaa.
"Unakumbuka kuna siku ulisahau bahasha yako ndogo nyeupe, nilivyoona ni picha zako, nilienda mtaa wa Zanaki na Jamhuri Akber studio nikazidurufu, baada ya wiki tu zikatoka. Samahani sikukuambia, nilikuwa nataka nikuone vizuri, kaka Yasir aliniambia unafanyia RTC, nilikuwa sikufahamu kabla..."
Nikamkatisha maana alianza kujitetea sana..
"Zile nilizileta kwa ajili yako, lakini mazingira uliyonikabidhi upya nilishindwa kukuachia, hivyo lengo limetimia, bila shaka hata kuanguka kwa mtandio na bilauli zile ilikuwa ni mpango wa Mungu"
Tukacheka tena.
Tukaongea sana huku tukifurahi...
"Kata simu.."
"Kata wewe.."
"Anza wewe.."
"Wewe si ndiye uliyepiga.."
Tukawa ‘tunarushiana mpira’ pale kwa mahaba mara nikasikia sauti kwa mbali...
"Nyie nanyi kwa mapenzi ya kihindi!! hebu kata simu huko kesho si aja huyo!"
Hamida ndipo akakata simu.
******************************
Itaendelea...View attachment 1352500
James Jason
Wewe Mzee mtu hatari sana....simulizi yako imenivuta sanaSEHEMU YA 13 - A

Hivi kile kitabu kinaitwaje cha french sex art culture na mwandishi wake ni nani tafadhali
Makadirio yangu yalikuwa 57 pale uliposema difference yenu ni four years!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka na huku huwa unazurura....kuna mengi ya kujifunza na kuturudishia kumbukumbu za jiji letu la mzizimaUkiacha habari ya kwamba hii ni simulizi, kuna vitu vingi sana vya kujifunza.
Hongera sana mkuu JBourne59.
Mkuu ulishasikia kauli USIFANYE MAAMUZI WAKATI WA FURAHA SANA AMA HASIRA SANA? Ndicho kimenikuta hapa. Kwaheshima na taadhima naomba kufuta kauli hiyo. Ila mzee anajua hadi anakera kabisa. Huyu ni dhahabu kwenye jiwe.Mkuu umesema ''kitu pekee'' kinachokufanya uendelee kusoma simulizi hii ni kwa sababu mzee wetu JBourne59 ni mkweli akisema inaendelea leo inakua hivyo ?
Unamaanisha hauvutiwi na kitu kingine chochote ?
Nimejisikia vibaya sana kwa maneno hayo ''kitu pekee''.
Naona kama ni discredit, tafadhali mkuu naona ufute kauli yako vinginevyo ''NITASHIKILIA SHILINGI KWENYE MSHAHARA WA WAZIRI'' au ''nitakuwekea vikwazo vya kuingia kwenye taifa langu''...
Aiseee hapo kwenye show nimejikuta nacheka sana....awali nilitaka kuuliza kuhusu umri sababu ni jinsi unavyoweza kusimulia kwa lugha za sasa na zamani (lugha za mtaani au za vijana), nimepata jibu. Hongera sana mkuu jamaa uko vizuri. Ushawahi kuandika vitabu/novel?Wakati ule alikuwa kijana, mie amenizidi kiaka 10 na miezi kadhaa.
Sijazeeka 'kihivyoo', show napiga kama kawaida, na nguvu za kufanya kazi ninazo bado, nilizaliwa miaka miwili kabla ya Tanganyika kupata uhuru.
James Jason
Hata mimi sikifahamu mkuu ngoja tusubiri majibu ya JBourne59Hivi kile kitabu kinaitwaje cha french sex art culture na mwandishi wake ni nani tafadhali
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuuNimekitaja mara kadhaa kwenye stori nilizopost..! Zidisheni umakini na kujilazimisha kufanya rejea.
Kinaitwa French Sex Art Manners mwandishi ni Georges Valensin
James Jason