Uhusiano wangu kimapenzi na "Hamida"

Hapa inabidi tukutambue kama Jamali kwa sasa
 
hapo naisi kama muvi ndio inaanza upya nimenda hii stori kama ninavyopenda JUMONG
 
Baba Shikamoo, Leo tunapata kipande kingine samahani!??

Typed Using KIDOLE
 
vip hukuwa na ndugu mbona mpaka now sjaona ndugu yoyote ukim M pesa as ulikuwa boss wa RTC

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu walikuwepo wengi, ukiacha wa tumbo moja walikuwepo wengine waliojitokeza... Extended family.

Lakini katika simulizi hii najaribu kuelezea sehemu inayohusu mchakato wa mimi kumpata Hamida na kuwa mke wangu, nilipitia changamoto nyingi ambazo tutaziona mbele.

Aidha, wakati huo hakukuwa na huduma za mpesa nk, simu zenyewe za mkononi hazikuwepo hadi miaka kama kumi na miwili hivi baadaye ndipo niashika simu nangu ya kwanza "Thuraya" (satellite phone), hapo hata mobitel hawajaanza ambao baadaye wakajiita buzz kisha tiGo

Japokuwa kulikuwa na huduma za kutuma fedha kupitia Shirika la Posta na Simu (TMO - Tanzania Money Order) kwa mfano wa western union hivi sasa.

Endelea kufuatilia na ku LIKE.

James Jason
 
SEHEMU YA 13-B
**************

"Nyie nanyi kwa mapenzi ya Kihindi!!! Hebu kata simu huko, kesho si aja huyo!"

Hamida ndipo akakata simu nami nikakata.

Nikawa mwenye furaha zaidi. Kuongea na umpendaye ni raha sana hasa ukiwa unapata uzani sawa na ule uzani unao uonesha hata kama yeye anadanganya.

Nilijisomea kitabu kidogo, kisha nikaenda kujimwagia maji ili nianze kuutafuta usingizi.

Nikaweka santuri moja ya siku nyingi sana (1972) ya Harry Nilson, na katika colletion ile wimbo wa kwanza ulikuwa unaitwa "Without You"

Maneno ya ule wimbo yalinifanya nijione kama mimi ndiye namuimbia Hamida. Hebu sikiliza:-



Without You (1972)
Harry Nilsson

[emoji443]
"No, I can't forget this evening,

Or your face as you were leaving,

But I guess that's just the way the story goes,

You always smile but in your eyes your sorrow shows,

Yes, it shows,

No, I can't forget tomorrow,

When I think of all my sorrows,

When I had you there but then I let you go,

And now it's only fair that I should let you know,

What you should know,

I can't live, if living is without you,

I can't live, I can't give any more,

Can't live, if living is without you,

I can't give, I can't give any more..."
*****

Nilikuja kushtua saa kumi za usiku nilipo banwa na haja ndogo, baada ya kutoka msalani niliamua nisilale bali nijiegeshe nikisubiria mida isogee kidogo niende masjid.

Alfajiri nilikuwa napenda kuswalia msikiti wa Mwembechai, palikuwa jirani zaidi kuliko masjid nuur.

Ibada ya kuswali huwa haichukuwi dakika nyingi, kama dakika tano tu, lakini maalim Juma alinihimiza kuendelea kufanya ibada za tasbihi (kama rozali) ili kumtaja Mwenyezi Mungu kwa majina ya sifa zake mbalimbali ili kujipatia thawabu zaidi.

Hivyo nilikuwa nakaa msikitini hadi karibu jua linapoanza kuchomoza ndipo huwa natoka kurudi nyumbani kujiandaa kwenda ama kazini ama shughuli ngingine.

Waliokuwa wanabaki kwa ibada za tasbihi walikuwa wengi, karibu nusu ya waliohudhuria ibada ya swala, hivyo tulikuwa tuna 'vuta uradi' (tasbihi) kwa pamoja, ilikuwa ni experience ya aina yake kwa jinsi sauti na hali unayojisikia wakati ukifanya tasbih.

Jumamosi hiyo nilifanya kazi muhimu zote za pale nyumbani kwa kuwa nilikuwa najuwa Jumapili nitarudi usiku sana, nilipaweka vizuri hadi kufikia saa sita na nusu mchana nilikuwa tayari.
******

Saa kumi na moja na nusu nilikuwa bandarini, nilikuwa nimevaa kanzu yangu ya khaki, kofia nzuri ya mkono, sandals za kahawia, ndani ya kanzu nilikuwa nimevaa suruali fupi nyepesi ya kuvalia kanzu, nilikuwa pia nimevaa fulana (vest / singlet) nyeupe. Kwenye mfuko wa kanzu nilikuwa na kile kijitabu kidogo cha dua, post card ile niliyonunua mjini posta, pamoja na passport book, mfuko mwingine niliweka tasbihi fupi yanya goroli 11. Nilikuwa nimebeba rasket (kama kibegi hivi kidogo) ambapo ndani yake niliweka shuka jepesi la bluu, chupi mbili, bahasha yenye kadi na kanzu nyeupe.

Muda ulipowadia wa kuingia kwenye meli niliingia na nikafika kwenye nafasi yangu daraja la pili.

Saa kumi na mbili na nusu meli iling'oa nanga na kuanza kuondoka. Meli ilikuwa kubwa na yenye nafasi ya kutosha, watu wengi tena waongeaji sana na masihara (utani) mengi.

Nikakumbuka safari yangu ya kwenda Lindi kwa mara ya kwanza, nikatabasamu na kupotezea.

Kwenda kisiwani Unguja ndiyo ilikuwa mara ya kwanza, niliandika ile namba ya simu (kwenye kile kijitabu cha dua) ya nyumbani kwa ma-mkuu wa Hamida kama akiba.

Meli ilikuwa inatembea taratibu sana na hali ya bahari ilikuwa shwari.

"Swalaa swalaa swalaa"
Nilisikia sauti ya mtu akisema hivyo huku akitembea..., nikaangalia muda kwenye saa yangu ilikuwa na saa mbili usiku.

Baadhi ya watu kwa zamu wakawa wanaelekea sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuchukulia udhu na kufanya ibada ya swala, nami kwa kuwa kipindi cha magharibi kilinipita nikaona ni fursa ya kwenda kuswali swala zote mbili.

Maalim Juma alinifundisha kuwa kwa msafiri imeruhusiwa kukusanya baadhi vya vipindi vya swali na kuswali wakati mmoja tena kwa kupunguza idadi ya rakaa.

Hivyo kabla sijaswali isha, niliswali rakaa tatu za magharibi, kisha nikaswali isha kwa kumfuata muumini mmoja ambaye alikuwa imamu kwa wakati huo. Hivyo tuliswali rakaa nne kama kawaida.

Wakati meli ikiendelea na safari tulikuwa tunaburudishwa na nyimbo laini za kimwambao hususan taarab.

Hali ilikuwa tulivu hadi nikaanza kusikia usingizi, nikatoa shuka nikajifunika nikaegesha na usingizi ukanichukuwa.
***

Saa kumi na nusu hivi nikasikia tena ile sauti ya swalaa swalaa japo safari hii kwa mbali, nikaamka na kwenda kwa ajili ya ibada ya asubuhi ambayo ni rakaa mbili tu. Ajabu meli ilikuwa imesimama lakini hatujafika bandarini ila kwa mbali bandani inaonekana.

Kumbe tulifika hapo muda mrefu kidogo lakini Nahodha wa meli alikuwa anasubiri pakuche vizuri asogeze meli gatini.

Saa kumi na mbili tukawa tunatia nanga bandarini Unguja. Kwa ukaribu niliyaona majengo ya kale ya Unguja na vyombo vingine vya majini hapo bandarini.

Tulianza kushuka, ilipofika sehemu ya kugongesha passport yule afisa aliniangaliaaa kisha akasema karibu Zanzibar James.

Kwenye passport yangu majina yalikuwa Bourne Jason James.

"Ahsante" nilimjibu huku nikichukuwa passport book yangu. Nafikiri aliona nuru ya uislam kwenye uso wangu lakini majina kwenye hati ya kusafiria yalikuwa 'hayafananii'

Nilitoka hadi geti la kutokea nje ya bandari na hapo ndipo Hamida aliniona na kuniita kwa sauti...

"Jamaal"

Nikageuka na kuangaza, nikamuona Hamida wangu. Hakuwa peke yake, alikuwa na mvulana mmoja na mama mtu mzima mmoja.

"Assalaam aleikum wa rahmatullah wa barakatu"

Nilisalimia kwa maamkizi mema kabisa ya kiislamu.

"Waa aleikum salaam wa rahmatullah wa barakatu"

Wote watatu waliitikia na yule kijana alinipa mkono kwa ishara ya kusalimia nami nikaupokea.

"Karibu Zanziba shekhe"
Alisema yule kijana, ambaya baadaye nilikuja kujuwa ni mtoto wa ma-Mkuu wa Hamida, alikuwa anaitwa Shaha.

"Jamaal, huyu hapa ndio ma-Mkubwa Saada, huyu hapa ni Shaha mdogo wangu mtoto wa ma-mkubwa,"

Alisema Hamida kwa kuwatambulisha kisha akawageukia wenzake akawaambia ,

"Jamani huyu ndiye Jamaal"

Wakaangaliana, wakatabasamu kisha wakasema kwa pamoja

"Tunashukuru kukufahamu"

Tukaanza kutembea kuelekea sijui wapi...

Tukakatisha vichochoro vingi sana, nikawa naona magorofa kuukuu ya mawe, tukawa tunapishana na baiskeli nyingi sana, batavuz chache na vespa mojamoja..

Tukatokea sehemu kuna nafasi kidogo na kuna barabara kuu, na upande huo tulipotokea kulikuwa na soko kubwa...

"Jamaal, hapa ndiyo Markiti"

Alisema Hamida huku akionesha soko.

"Ahaa, ndiyo market hii ya Unguja!"
Nilimrekebisha kidogo lakini wote wakacheka..

"Panaitwa marikiti, markit umeelewa?"

Niliitikia tu "eeeh"

Shaha akawa anaelekea kwenye sehemu ya kuegeshea magari, tukawa tunamfuata.

"Napenda kuliacha huku gari siku za meli, maa'ke kule vurugu watu na vipando vingi, hapa aaaa! Shwari baridiii" aliendelea kusema Shaha.

"Haya ingieni 'nkupeleken chap" alisema Shaha uku akifunguwa mlango wa gari.

Ilikuwa gari aina ya Austin, rangi ya maziwa hivi. Tukaingia tukaanza kuondoka, sijui hata mwelekeo, naona watu wengi tu barabarani tukawa kama tunaacha mji hivi, watu wakipungua sana barabarani, nikaona bahari ipo kwa upande wetu wa kulia,.

"N'kushushieni Migombani au n'pitilize hadi Mazizini!?" Aliuliza Shaha.

Ndio nikajuwa hapa tunaelekea Migombani labda kisha Mazizini.

Mara akili ya picha ya migomba ikanijia, halafu mazizi nayo yakajitokeza kichwani, hofu ikaja kidogo, "isije nikawa ndio naenda kuchinjiwa migombani halafu kutupwa mazizini" nikawaza.

Kwenye gari, mbele kushoto nilipishwa mimi kukaa, Shaha alikuwa anaendesha na nyuma walikaa mamkuu na Hamida akiwa nyuma ya dereva.

"Leo huwezi kuifaidi Zanzibar kwa kuwa muda wako hauruhusu, lakini kama ukija siku nyingine tutakutembeza sana, ufanye utalii wa mji mkongwe hadi 'mashambani'"

Hamida alisema kuondoa ukimya ulioanza kutawala.

Nikageuza shingo kumwangalia Hamida, akasema...

"Maa shaa Allah, umependeza"

Mie nikatabasamu tu. Nilikuwa namuheshimu mamkuu vinginevyo nami ningemfanyia vituko.

Mara gari ikakunja kulia, tukaenda mbele kidogo bahari ikawa inaonekana, tukapinda kulia tena dereva akasimamisha gari kwenye nyumba fulani mpya hivi nzuri sana.

Akina mama fulani wengine wawili wakatoka ndani ya ile nyumba na kuja kutupokea.

"Karibuni wageni"
Alisikika mama mmoja mtu mzima naye mnene hivi akisema.

Tukashuka, nikawa nawafuata wenyeji wangu, Shaha akarudi kwenye gari huyo akatoka...

"N'tawafwaten baada ya alsir" alisema huku akipungia mkono.
***

Nilijikuta nipo katika sebule kubwa sana, busati zuri lakini pia kuna makochi pembeni. Nyumba ilikuwa tulivu na upepo kutoka baharini ulikuwa unaingia moja kwa moja.

"Hamida, muoneshe chumba kisha aende akajimwagie maji"

Yule mamkuu alisema.

Nikamwangalia Hamida, akanikonyeza kwa mkono ili nimfuate, tukaingia kwenye chumba kimojawapo

"Taulo hilo hapo, na bafu sukuma mlango huo"

Hamida alisema kisha akatoka.

Kilikuwa ni chumba chenye choo na bafu mumo humo. Nikaingia kuoga, kisha nikabadili chupi, kanzu nilivaa ile nyeupe kisha nikakikagua chumba kwa haraka haraka.

Chumba kikubwa, kitanda kipo kimoja futi sita kwa sita, godoro lilikuwa limefunikwa na bedcover nene hivi, kuna kabati kubwa sana la milango mitatu na meza yenye vipodozi vingi ikiwa na kioo kidogo. Nikatoka mle chumbani nikiwa safi na fresh nikinukia perfume yangu al oud ambayo sikujanayo lakini nilipulizia kabla sijaweka kwenye rasket yangu.

"Assalaam aleikum"
Nilisalimia tena wakati naingia sebuleni.

Waliitikia na mamkuu akasema tukaribie kwenye mkeka tuapte chai.

Ilikuwa ni ule mkeka mdogo wenyewe wakiita masala, japo misala niijuayo mimi haipo hivyo. Tukaketi wote watano kuuzunguka mkeka.

Kulikuwa kuna makawa matatu yaliyoandikwa jumbe za kimahaba, yalifunika sinia tatu tofauti, sinia moja lilipofunuliwa lilikuwa na mikate ya boflo, sinia lingine kilikuwa na mikane ya kumimina (imetengenezwa kwa mchele) na sinia ya tatu ilikuwa na chapati za kusukuma. Pia kulikuwa na bakuli la mchuzi wa nyama ya ng'ombe, chupa kubwa ya chai na sahani tupu tano na vibakuli vidogo pamoja na vikombe vitano...

Tulianza kunywa chai pale taratiibu huku tukiongea, aisee wale wamama walikuwa wanaongea balaa, ilikuwa ni maongezi ya kawaida tu lakini utapenda jinsi wanvyofinyanga ndimi zao laini.

Wakati tunaendelea kula mamkuu alinitambulisha kwa rafiki yake yule mama mnene sana na mwingine alisema ni jirani yao. Baba mwenye nyumba alikuwa ametoka kwenza Mazizini, si mbali kutokea hapo.

Baada ya chai, tulianza kuongea, walianza kwa kunihoji baadhi ya maswali.

Yalikuwa maswali ya kawaida tu kama vile mie asili yetu ni wapi, ukoo wetu, nafanya kazi gani, kwa nini nimempenda binti yao yani maswali yote ambayo Hamida angeweza kuwajibu bila hata mimi kuja huku Unguja.

Wakaniuliza kuhusu kusilimu kwangu, nimeshajifunza nini katika dini na kama nina nia ya dhati ya kuishi na binti yao.

Niliwajibu kwa kuchukuwa tahadhari sana, kila jibu nilikuwa sitengenezi nafasi ya swali lingine litokanalo na jibu la awali.

Kila mmoja wao alishusha pumzi tu kwa kuridhika na majibu, kasoro mwenyewe Hamida ambaye alikuwa muda wote akitabasamu.

Muda wa kuswali swala ya adhuhuri ulikuwa umewadia, wote wakatoka kueleke chumba kingine kujiandaa na kuswali hukuo huko (wanawake wa kiislamu wameshauriwa kuswalia nyumbani kuliko kwenda msikitini, lakini wanaume wao kwenda msikitini ni bora zaidi kuliko kuswalia nyumbani.

Mara Hamida akarudi akaniambia

"Nimeshakuandalia pakuswalia, chumba kilekile"

Nikaenda kuchukuwa udhu (kunawa kwa ajili ya kuwa tayari kwa ibada), nikaanza kuswali..

Katika rakaa nne zile za adhuhuri, hizi rakaa tatu nilitoka kabisa nje ya utulivu katika swala, nilikuwa na maswali mengi sana, "yaani nimeitwa kwa ajili ya kuulizwa vimaswali hivi tu" niliwaza

Baada ya kumaliza kuswali adhuhuri rakaa mbili na kuunganisha alasir rakaa mbili, nilibaki kwa dakika chache nikijisomea dua na kuvuta uradi. Halafu ndio nikatoka kwenda sebuleni.

"Karibu, chakula kipo tayari" alisema yule mama mnene.

Tulikaribia wote kuzunguka msala kama wakati wa chai. Baada ya kufunuliwa makawa, ndipo nikaona sinia dogo lenye wali mweupe, kitoweo kilikuwa samaki aina ya kolekole, ameungwa vizuri kwa nazi, pamoja na vinywaji.

Kwa kuwa tayari nilikuwa mzoefu wa namna ya kula wali kwa mkono wala sikuwa na wasiwasi.

Tulikula ule wali wote ukaongezwa na mwingine kama ule, tuliumaliza, kulikuwa na siki (achali) ya mbilimbi na pilipili za kusaga ndizo zilitupa hamu ya kula.

Baada ya hapo tuliendelea na stori tu za kawaida. Mara Hamida akanikonyeza tena nimfuate, nikainuka kumfuata huku wale wengine wakituangalia.

Tukaingia kile chumba nilichoingia awali. Tukakaa kitandani, mlango upo wazi ila kuna pazia.

"Huyu ma-mkuu ni mke wa baba mkubwa ambaye wana udugu na mzee Burhani kiukoo, Babu yetu kwa baba alikuwa akiishi Mazizini ambapo baadaye utapelekwa huko ndipo utakutana na wazee ambao wameandaliwa kwa ajili ya kukuona na kujiridhisha ili wawe na nguvu kumweleza mzee Burhani juu ya mimi nisiolewe Oman kwa mbabu kwa kuwa tayari nimeshakupenda wewe."

Alisema Hamida kwa sauti ya kunong'ona, kisha akaendelea

"Huu ni mpango wa Shangazi na Mumewe, baada ya kuwaelezea suala langu ndipo mume wake aunt alitoa wazo niletwe huku kwa mamkuu kwa ajili ya kufundwa"

Alisita kidogo halafu akasema

"Umemuona yule mama mwembamba, yeye ndiye somo yangu, nilivunja ungo nikiwa huku naye ndiye 'aliyeniokota' (hapa sikumuelewa mara moja), hivyo ndiyo nimeletwa huku kwa ajili ya maelekezo kabla ya ndoa."

Akaenda kuchungulia mlangoni kwenye pazia kisha akarudi na kuendelea...

"Mume wa mamkuu naye akawashirikisha baadhi ya wazee wenye busara ambao ndio utakutana nao huko Mazizini ili wakuhoji..."

Akameza mate halafu akaendelea

"Wala usipanic, ukiwajibu vizuri wala hawatakuwa na tatizo, muhimu jieleze vizuri"

"Mambo yakienda sawia mpango kwa kuolewa Oman utakufa rasmi, nawe utapata fursa ya kuniposa"

"HamidaaaAa"

Sauti iliita kutoka sebuleni.

Alitoka kuelekea sebuleni na kurudi na kuniambia...

"Shaha amekuja kukuchukuwa, twende"

Nikatoka kwenda sebuleni, tukaagana na wote pale, yani walibaki wote isipokiwa Shaha na mimi ndio tuliondoka.

Nikajisemea moyoni, kumbe hapa ilikuwa ni kituo tu, sasa ndio naenda 'kuchinjwa' mazizini. Ila nikajipa moyo kwa maneno ya Hamida.
***

Dakika mbili tatu tu tukafika Mazizini, tulikunja kushoto kisha kulia tukawa tumefika kwenye uwanja mkubwa na nyumba ya kizamani kidogo ila kubwa.

Gari likaegeshwa, Shaha akanikaribisha ndani.

"Assalaam aleikum wa rahmatullah wa barakatu"

Niliwasalimia kwa mpigo halafu nikaanza kuwapa mkono mmoja mmoja kuanzia upande wa kulia kwangu, walikuwa wazee wa kiarabu na mchanganyiko wa kiarabu na kiafrika (halfcast), walikuwa watatu nasi tukafanya idadi iwe watano.

Niliwekwa 'kiti moto' cha kama saa mbili hivi, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu nilikuwa mzuri kwa kujieleza tena kwa lugha fasaha ya kiswahil kwa lafudhi ambayo haikuwa rahisi mtu kujuwa kama mimi ni 'mtu wa kuja' kutoka bara ndani ndani huko.

Mimi ni Mtaturu (siyo Mnyaturu) ambaye nilipata bahati ya kuto-togwa masikio, niliyesoma na kukulia katika maadili ya kikatoliki lakini nikaja kusilimu tayari nikiwa nimeanza kuipa nyongo dunia hususan baada ya kumuona Hamida na 'moyo wangu kumdondokea palepale', wajihi wangu na tabia yangu wakati wa maongezi na kula ikiwa pamoja na utendaji wangu kazini vilinipa sifa ambayo mbele ya wazee wa Hamida sikumwangusha hata kidogo.

Wapo waliohoji kuhusu kuharibu kikazi chao kwa kuingiza ngozi nyeusi, lakini niliwashindia kwa mafundisho aliyonipa Hamida mwenyewe wakati nikimhoji kuhusu sifa za kuchaguwa mchumba pamoja na elimu chache niliyoipata kutoka kwa Maalim Juma.

Baada ya saa mbili hivi (2hrs) palikuwa na ukimya ambao uliashiria kushibishwa na maelezo yangu. Sikuonesha udhaifu katika hoja na nilijibu kwa hekima kubwa.

Wazee wakaniruhusu kurudi Migombani, wao wakaendelea na kikao...
***

Tulifika Migombani aroundi saa kumi na mbili jioni, tulipokelewa, nikaandaliwa chai nikanywa.

Ma-Mkubwa akaanza ushawishi wa kutaka nisiondoke siku ile ili niondoke Jumatatu kwa ndege ya mchana.

Wote wakanishambulia nisiondoke, hapo tayari nina tikiti ya kurudi Dar es Salaam saa nne usiku, siku hiyo.

"Usiondoke tukupeleke Forodhani ukapaone"

Hamida naye alikazania.

Mie moyoni natamani kubaki, lakini nikawa nawaza kuhusu kazini kesho. Hatimaye nilipata wazo lililosababisha nikubaliane nao. Nikaomba nipige simu Air Tanzania kuahirisha safari, nikakatwa asilimia kadhaa nikapewa ndege ya mchana kesho ambapo nilitakiwa niongeze nauli kabla ya ku-check in.

Walifurahi sana, na baada ya swala ya magaharibi (na isha kwa upande wangu maana niliswali kabisa - safar) tulitoka, mie, mamkubwa, Hamida na Shaha akiwa dereva.

Tulienda moja kwa moja hadi Bwawani Hotel, wakanitembeza tembeza kiasi, giza lilivyoanza kukolea tukatoka kwenda Forodhani.

Forodhani palikuwa pamejaa watu na pilika nyingi za kibiashara na burudani, nilikula pweza kwa mara ya kwanza, ngisi na prowns. Mashokishoki na 'ubuge ubuge' kibao.

Nilifurahia forodhani, mandhari ya bahari, uchangamfu na uaminifu wa wafanya biasharana wateja ili mradi raha na amani tu.

Baadaye mamkuu alitandika kimkeka kidogo tukakaa kando kidogo na kufurahia maisha.

Saa zile chache za forodhani zilinifanya niipende Zanzibar, niliona ukarimu wa watu wa Zanzibar na mienendo yao japo kwa saa zile chache.

"Kula ushibe, usiku huku hawapiki, sana sana chai na boflo tu"

Alisisitiza Hamida huku akinihimiza niendelee kula.

Nilishiba barabara. Tuliendelea kufurahia pale forodhani hadi saa tano za usiku ndipo tulipoondoka.
******

Tukiwa sebuleni peke yetu mie na Hamida (Migombani) kabla ya kulala, Hamida aliniambia...

"Nakushukuru kwa kuja, akina mama wamekufurahia, sijui huko kwa bamkuu labda"

Aliniambia kwa sauti ya chinichini,

"Kesho in shaa Allah nitamwambia Shaha akupeleke mji mkongwe ukatembee kwa miguu ndio utapafaidi"

Nikamkatisha,

"Kwani wewe utakuwa wapi?, mie sikuja kutalii bali niliitikia wito wako, hivyo siendi popote bila wewe"

Nilimpiga 'mkwara mbuzi'

"Basi nitaangalia kama mkuu ataniruhusu twende wote" alisema.

"Mwache mgeni akapumzike"

Mamkuu alisema alipokuja, alitoka bafuni kuoga.

Hamida alimuangalia tu mamkuu wake kisha akanikonyeza nielekee chumbani. Tukaagana kwa kutakiana usiku mwema.

Kwenye kile chumba niliona baadhi ya vipodozi vya Hamida, ndipo nikajuwa chumba hiki anakitumia yeye.

Nikaoga kisha nikavaa suruali ya kuvalia kanzu pamoja na ile vest yake, kisha nikaanza kujisomea kile kitabu.

Wakati nilipohisi uchovu, nikaenda kukiweka kitabu kwenye ile dressing table, nikaona kitu kama memo hivi chini ya chupa moja ya perfume, nikaivuta na kuisoma, "usifunge mlango", huo ndio ujumbe mfupi niliowekewa ambao ndio nauona sasa. Nikajifanya natoka chumbani kwenda sebuleni kama kuangalia kitu hivi kisha nikarudi na kujilaza kitandani bila kufunga mlango, ni pazia tu ndio lilisitiri nisionekane.
*****

Nilishituka kutoka usingizini baada ya kuhisi mikono baridi inanigusa begani.

" Shhhhhhhh! ni mimi"

Hamida alisema kwa kunong'ona

"Wewe! Siyo vizuri, tutakutwa"

Nilimuambia huku nikiamka na kukaa kwenye kingo ya kitanda.

"Mie usingizi hauji, nimeona bora nije tukumbatiane japo kwa dakika moja ndio niridhike"

Nikainuka, tukawa tumeaimama wote.

Alikuwa amevaa nguo ya kulalia, habari zote zaonekana vyema, mara mnara wangu juuu!

Sikuwa comfortable kabisa ila nitafanyaje, nikamfuata, nikamkumbatia, tukaanza french kisses pale huku mikono yangu ikiminyaminya makalio yake...

Mie hamu ikanizidi lakini sikuwa comfortable kufanya kwa mazingira yale, nikaamua nimkojoleshe yeye fasta.

Nikamwambia pandisha mguu mmoja kitandani, akapandisha, nikaanza kumchezea kis*imi, tayari alikuwa very wet na alianza kuguna...

Nikaona hii itakuwa soo (noma), nikamwambia lala kitandani, nikavua vest na kumuwekea mdomoni kisha nikaanza kumsugua kigoroli kwa mkono wa kulia kwa vidole vitatu, viwili vikiwa vinasugua mashavu ya papuchi kwa kufanya kama unakibana kigoroli, na kidole cha kati kati ya hivyo viwili kinasugua hicho kigoroli, aliendelea kuguna guna lakini safari hii sauti ikiwa imewekewa 'silencer', alivyoanza kujinyonganyoga nikaingiza kidole ndani kidogo kwa juu nikasugua kisponchi (gspot) kwa kasi sana hadi akafika kilele akajitoa mwenyewe ile vest akaiweka kitandani.

Akaamka, akanibusu huku akisema, "ahsante, sasa naweza kulala, nisingeweza kuvumilia"

Alivyotoka, mie nikapumua uhuuuu, lakini mnara upo full maximum, nikaona hapa hapalaliki, nikaenda kwenye dressing table, kulikuwa na mafuta fulani hivi ya mgano yanaitwa Shanti. Nikatumia yake kupiga selfie kwa taswira ya Hamida. Da! Selfie ya mwisho ilikuwa mwaka 1975 term ya pili Kibaha Sec, nilisikitika kwa kuvuja nadhiri ya kupiga punyeto.

Usingizi ukanipitia hadi niliposikia adhana ya kwanza ya alfajiri.

Nikaamka, nikaoga na kujiandaa kwa swala za utangulizi kabla ya swala ya alfajiri ambayo huswaliwa pindi alfajiri ya kweli inapoingia.

Baada ya kuswali, nilivuta uradi kidogo kisha nikapanda tena kitandani kulala. Safari hii usingizi ukanichukuwa hadi saa mbili asubuhi.

Nikakumbuka kazini, nikavaa kanzu nikaelekea sebuleni na kumkuta mamkuuu ameketi, baada ya salaam nikamwomba nipige simu afisini Dar ea Salaam.

Nilimpata Mary na kumuambia...

"Leo ni zamu yako kunisaidia"

"Sema lolote boss, nipo tayari" alijibu Mary.

"Bado nipo Unguja, nitarudi leo jioni, hivyo angalia namna ya kuwajibu wageni wangu watakaokuja siku ya leo, wakitembelea maboss pia utaona namna ya kuniokoa, halafu baadaye kabla hujatoka ofisini nitakupigia tena unipe mrejesho"

Nilimpa maelekezo na kumpa uhuru ya namna ya kujibu wageni wangu.
***

Nikawa na amani sasa, nikarudi chumbani, nikaoga na kuvaa vizuri na kuja sebuleni ambapo staftahi tayari ilikuwa imeandaliwa.

Kulikuwa na chapati za kumimina (chapati za maji), slesi za mikate ya siha, kulikaangwa mayai, mchuzi kidogo wa samaki na vitu vingine vidogo vidogo.

Baada ya chai na kupumzika kidogo, alifika Shaha. Akatupeleka hadi Markiti kisha yeye akaondoka zake, tukabaki mimi Hamida na mamkuu.

Wakanitembeza chohoro za mji mkonge, nikawa sijui wapi ni wapi, lakini wenyewe wanaelewa vizuri tu...

Tulipita madukani, nikanunua baadhi ya zawadi ndogo ndogo kwa ajili ya Mary, na zingine nilinunua kwa ajili ya Hamida japo sikumwambia kuwa ni zake mpaka nilipomkabidhi baadaye kabla sijaondoka. Nilimpatia pamoja na ile post card ambayo niliifunga vizuri kwenye bahasha na gundi (post card haziwekwi kwenye bahasha lakini, nilijisemea), nikapotezea kwa kusema lakini hii ni special case.

Adhuhuri tuliamua kurudi Migombani kwa kukodi vespa tatu.
****

Saa nane na nusu, baada ya chakula cha mchana, nilimpgia Mary, kila kitu kilienda vizuri kule, wenyeji wangu wakanisindikiza hadi airport, safari hii tulitembea kwa miguu, siyo mbali.

Tuliagana, kisha nikaenda kwenye sehemu ya kusubiria. Ndege ilipokuwa tayari tulitangaziwa tupande, na saa kumi na robo hivi tukapaa na kuiacha ardhi ya Unguja.
****


Itaendelea...



James Jason
 

Super.
 
Du! Kama ulianza kutumia Thuraya hata kabla ya mobile phones kuingia nchini, ntashangaa sana kama hukuwa mtu wa kitengo. 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…