Uhusiano wangu kimapenzi na "Hamida"

Watoto nilionao ni:-

1. Mmoja Kwa Marehemu Ruth
2. Sita kwa Hamida

Ila nina wasiwasi huenda Rose 'alisepa' na damu yangu. Wasiwasi tu.


James Jason
Napenda kujua uhusiano wa Hamida na ndugu zako ulikuwaje? Uliwahi kumpeleka UTATURUNI?
 
Mkuu, napenda kujua, ile miaka miwili uliyoyumba kiuchumu maisha yako/mahusiano yako ndoa yaliendaje? Hamida alikupiga jeki vipi?
 
Truth Joke!
Hamida ana elfu 5, Mimi nina elfu 10, Jumla ya hela zetu ni elfu 10.

Hamida ana laki 1, Mimi nina laki 3, Jumla ya hela zetu ni laki 3.

Mimi nina miliini 1, hamida ana Milioni 5, jumla ya hela zetu ni milioni 1.
(Hahhahhaha)
______

Kujibu swali lako ni kwamba, sikuyumba kivileee ila mapato yalishuka kulingana na kuhama ofisi ya biashara na kwenda ofisi nyingine ambapo hela ni za kupimiwa.

Hamida alikuwa mpishi mzuri, ilipotokea nahitaji msaada kwake wa kifedha alinipatia, alikuwa anafanya biashara ndogondogo na wateja wake walikuwa ni baadhi ya wana familia na majirani.

#Usije ukadharau elfu moja moja za mkeo anayeuza "maandazi", aisee ni nyingi sana akizikusanya.

#Wajibu wa Mume kwa mke ni pamoja na KUMLISHA, KUMVISHA, KUMPATIA MALAZI, JIMAI pamoja na mahitaji mengine.

#Tafuta pesa
#Jifunze namna bora ya kumridhisha mkeo kwa tendo la ndoa
#Fanya na mengine ya kulea ndoa, UTAISHI KWA FURAHA SANA.
 
Asante sana nimekupata Mkuu!
 
Karibu kila mwisho mwaka huwa tunaenda isipokuwa miaka miwili iliyopita mida hiyo nilikuwa nazurura nchi za jirani.

Uhusiano ni mzuri, changamoto za kawaida za kila familia, ila yote kwa yote hakuna pa kulaumu kwamba uhusiano ni mbaya.
 
Story nimeisoma leo, ila nikupe hongera mkuu, unajua kusimamia unaloliamini. Yaani mapenzi yalikubadilisha dini ndani ya siku chache tu??
Hongera sana mzee wangu. Glad that Hamida ndo unazeeka naye.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hii story mwaka jana nilikuwa naipita nikijua mambo ya Hamida kaniacha, jana nimesoma sehemu mtu akisema ni moja kati ya story yake Bora kusoma.

Hii story mwanzoni unapoanza/inavyoanza inakuwa kama haina mzuka vile ila kadiri inavyoendelea moto wake sio wa kitoto.
Yaani imenikumbusha ile simulizi ya Game Of the Thrones.

Hongera sana mkuu, kwa uandishi uliotukuka. Msalimie sana bibi Hamida, Kiukweli natamani sana ningepata bahati hata ya kukujua nikushike hata mkono tu.

Mimi ni umri wa mwanao hasa wa Pili au tatu maana nimezaliwa 1987. So wakati wa harakati zako hizi, sisi wengine bado maligafi za kutengeneza mbegu zetu zilikuwa mashambani huko.

Asante sana kwa kushare Mzee Jamaal.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ndo nimeiona mwaka huu naisoma sasa, niko sehemu ya 15!
Barikiwa ndugu mwandishi!!
 
Kwanza shikamoo mkuu,maaana mie n mwanao kama siyo wa mwisho bac ni mjukuu wako,,nmesoma stor yako nmefarijika sana na umri wangu mdogo kuwa mvumilivu na maisha na kupambania katika kile unachokiamini
 
Marhaba.

Chukuwa yale mazuri, mengine achana nayo.

Wape link na wengine wasome, ila wape tahadhari wasisome wakiwa wamefunga / swaum ama kusoma kwenye daladala, kuna sehemu zinaweza kuwafanya 'wa*loe' ama 'kudi*sa'
 
Mzee Jason maeneo uliyoyataja huko home iramba hususani ibaga chemchem hadi sibiti nimefika miaka ya 1984 nikiwa na miaka 14 nikitokea singida vijijini maeneo ya mgori nilikuja sibiti kuvua samaki nakumbuka niliombewa ruksa shuleni ya wiki mbili lakini kulingana na mazingira na usafiri kwa kipindi hicho nilijikuta nakaa sibiti miezi 2 tuliwakausha samaki kwa Mavi makavu ya ng'ombe na wakati tunaondoka mtoni sibiti tulikuwa na gari aina ya Isuzu iliyoletwa na bwana samaki wa singida mjini na gari haikua na taa hivyo kufanya tusafiri kwa msaada wa mbalamwezi lkn kuna shule siikumbuki jina kabla ya kufika ibaga stendi gari iligonga jiwe lililokua katikati ya barbara na kufanya tukae ibaga kwa takribani wiki moja tukisubiri spea toka sgd mjini hatukua na hata hela ya kula isipokua tulikuwa na samaki wengi sana hivyo samaki hao ndo ilikua chakula chetu na maji tulikuwa tunaenda kunywa kuna mto siukumbuki kwa jina ila ulikua jirani na stendi nyuma ya gest moja hivi sijui iliitwa ibaga gest lkn siikumbuki vzr nilikua bado mdogo na kulala tulilala kwenye Isuzu yetuiliyokua imepakiwa pembeni ya gest hiyo na tulikua tunafaidi mademu wanaoingizwa na kutoka gest kwa macho mazee yote kwa yote story ni nzuri sana nimeinjoi na imenikumbusha mambo mengi sana asante
 
Ahsante kwa kusoma na kuburudika.

Hiyo Isuzu bila shaka ilikuwa 'longbase' aka Mbaula, Zilitumika kuwapeleka askari Kagera kwenye vita 1980.

Wakati huo shule zilikuwa tatu tu Kata ya Mkalama, yaani Chemchem Primary School, Ibaga Primary School na Mkalama Primary School.

Mlipo haribikiwa palikuwa na mlima mdogo sana ila una mawe mengi makubwa barabarani, pembeni kulikuwa na mbuyu mkubwa upande mmoja na upande mwingine ni mlima wa mawe (wenyeji wanaita Kukulague)

Jirani hapo kulikuwa na nyumba moja tu ya kijana fulani very smart! Nyumba ilikuwa hiyo tu nyingine hadi usogee mbele kidogo.



Mwenye hiyo Guest House mliyolala, pia alikuwa ana duka ambalo nina historia nalo... [emoji23]

Huo mto mliokuwa mkienda kuchukuwa maji unaitwa mto Ibaga. Unachimba kidogo, kisha maji yanajaa, unaondoa maji machafu kwa kumwaga pembeni kisha maji masafi hujaa tena. Da, umenikumbusha mbali.
 
Marhaba.

Chukuwa yale mazuri, mengine achana nayo.

Wape link na wengine wasome, ila wape tahadhari wasisome wakiwa wamefunga / swaum ama kusoma kwenye daladala, kuna sehemu zinaweza kuwafanya 'wa*loe' ama 'kudi*sa'
Asante baba.
 
Kwakweli hu Uzi hata mimi nilikuaga na uruka kumbe ni Uzi wenye mafunzo tosha, haswa hapo kwenye mambo ya dini. Uzi una madini mengi ya kila aina. Shukrani sana Mzee
 
Hongera kwa kijana wa zaman, nilianza kusoma kula kwa masihara lkn nikauweka uzi pemben na leo ndio nimemaliza.
Kuna mengi nimejifunza na tunaendelea kujifunza na mwenza wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…