Wigelekelo
JF-Expert Member
- Sep 2, 2018
- 8,758
- 26,885
Duh![emoji848]SEHEMU YA 11
*************
[Picha zote ni kwa hisani ya google, hazina uhusiano wa moja kwa moja na simulizi hii. Majina yaliyotumika si halisi, bali majina machache sana kwa sababu maalum. Hii ni simulizi ya kweli lakini imeongezwa chumvi kidogo na maji kidogo sehemu nyingine ili kukidhi ladha ya usomaji na kupunguza uhalisia]
*****************
=
Siku hazigandi, mara Ijumaa hii hapa nipo kazini na muda wa kufunga ofisi imekaribia...
Nilimuaga Marry na kutoka na Batavuz yangu. Sikuwa napenda kwenda na gari ofisini.
Wiki hiyo yote nilikuwa namuhadithia Marry maendeleo ya mimi na Hamida, akawa ananiambia kweli umedhamiria...
"Atakuweza kweli na nanihii lako kubwa hivyo!" Alisema huku sasa akiwa anaamini kabisa nipo serious kuhusu Hamida.
"Maana mie mwenyewe niliweza kwa tabu japo nimezaa watoto wawili tena kwa kusukuma, lakini shughuli niliipata..."
Aliendelea kusema huku akionesha dalili za kutamani tena. Zaidi ya siku ishirini sasa sijapata msichana wa kustarehe naye, nami wala sikuwa na 'moto' zaidi ya kumuwaza Hamida.
***
Jumatatu ya wiki hiyo baada ya kuripoti afisini, nilitoka kuelekea peugeot house, nilionana na afisa mhusika na akaniambia yanayopaswa kufanywa ili kukamikisha utaratibu wa kiforodha na kibiashara kwa upande wao.
Kesho yake taratibu zote zikikamilika, nikapewa kadi ya gari (ilikuwa ya rangi ya orange iliyokolea, kadi ilikuwa ya kukunja mara moja.)
Niliwafuata maafisa wa bima makao makuu kwa ajili ya kupatiwa bima kubwa. Nilikamilisha siku hiyo hiyo na kuitoa gari yangu.
=
Mwaka 1976 baada ya kutoka NMC kabla sijaingia RTC nilipata mafunzo ya udereva mkoa wa Tanga (Tanga Driving School), wakati huo kilikuwa chuo bora sana, sijui kama bado kipo au kilichakufa.., nilipata cheti cha umahiri (CC) baada ya majaribio ya nadharia na vitendo nilivyofanyiwa na afisa mkaguzi msaidizi (Assistant Inspector) wa Polisi. Tulitumia Landrover 109 na baadaye alinijaribu kwa pikipiki ya Polisi kwa umbali mfupi.
Hivyo sikuhitaji usaidizi wa dereva mwingine, niliitoa gari pale na kuchukuwa njia ya Bibi titi (sasa) na kupinda kulia kufuata barabara ya Morogoro, huyoo mdogo mdogo hadi nyumbani.
Miaka hiyo usalama ulikuwa mkubwa sana, watu wengi walikuwa wanapaki magari yao nje ya nyumba zao usiku kucha bila hofu wala wasiwasi. Nami nilikuwa naipaki nje ya nyumba lakini pia bahati nzuri kwa jinsi nyumba zile zilivyojengwa kulikuwa na nafasi kubwa kutoka njia ya mtaa hadi kuufikia mlango wa mbele wa nyumba.
***
Ratiba yangu ya mwisho wa juma hili Marry alikuwa anaijuwa yote kwa kuwa nilimshirikisha.
=
Nilifika nyumbani, kabla sijaingia ndani nilifungua mlango wa gari na kuiwasha (baada ya ukaguzi wa kawaida), kwa kuwa asubuhi nilichelewa kuamka hivyo sikuiwasha.
Nikaingia ndani huku gari inaunguruma nje. Ilikuwa pijo ya kisasa wakati huo, ilikuwa na 'staff gear lever', yaani ile gia liva ya kwenye usukani pembeni. Ilikuwa inatumia petroli supa, ilikuwa inatumia kitu kinaitwa distributor, pistoni nne, cc 1,796 , gia nne ya tano 'rivas'
Nikawa naendelea kupitia user's manual, ambayo nimekuwa nikiipitia tangia Jumanne kila siku jioni baada ya kutoka madrasa (isiyo rasmi) kwa akina Hamida.
Baada kama ya dakika thelethini hivi niliona tayari inatosha niliamua kwenda kuizima.
Baada ya kuizima kabla sijaingia ndani naona Marry huyu hapa anakuja...
"Karibu" nilisema huku nikiwa nawaza kuna kitu gani kimetokea, maana si kawaida yake kuja kwangu bila kunijulisha.
"Karibu sana" nilisema tena huku nikifungua mlango wa nyumba.
"Nimekuja kuiangalia kwa karibu pijo yako" alisema kwa kutania.
"Aaaaah, hiyo hapo, mwari mpya kabisa" nilisema kwa kulisifia gari.
Hii ilikuwa ni mara ya nne kwa Marry kufika nyumbani, mara ya kwanza ilikuwa kwa nia ya kupafahamu, mara ya pili ilikuwa kwa kunielezea matatizo ya nyumbani kwake (ndoa), mara ya tatu tulikuja wote kwa ajili ya 'one night stand'. Tulikubaliana tusirudie tena.
***
Aliketi kwenye kochi (yale ya mninga na cussion), mimi nikaenda kwenye friji nikamtolea pilsiner (ndio nilikuwa namaliIa bia za mwisho zilizokiwepo home, ila Brand bado zilikuwepo chupa kadhaa ambazo nilikuwa nazipata kule mtaa wa Mkwepu / Jamuhuri. Nilikuwa napenda Cognac kwa sababu ndiyo niliyo jifundishia kunywa nikiwa Uingereza.
"Karibu Marry" nilisema huku nikimmiminia pombe kwenye bilauli (hosco brand)
"Ahasate" alisema na kukaa kimya.
Mie kwa kuwa baadaye nilitaka kwenda kwa akina hamida kumfikishia memo niliyoiandaa, sikunywa pombe, bali nilimalizia juisi ambayo nilikuja nayo jana kutoka kwa mama Warda.
"Mbona wewe hunywi" aliuliza Marry
"Si nilikuambia mimi nimeanza kuacha, nimesilimu hivyo wewe enjoy, ukiweza beba zote hizi uende nazo (zilibakia kama tano hivi kwenye friji)
"Hahahhah, yani hadi pombe umeacha! We kiboko! Hamida anakupeleka puta eee"
Alisema kilevilevi, maana Marry ni mbovu kwa pombe, bia mbili tu anachangamka.
"Ukisikia mwisho wa reli basi ndio pale, Hamida nadhani ndio itakuwa 'Kigoma yangu'
Nilisema huku nikionesha msisitizo.
" Enhe, kulikoni umekuja bila taarifa badala ya kumuwahi Mangi nyumbani?" Nilimuuliza huku nikichagiza
"Mmhhh!"
Alishusha pumzi kisha akaendelea
"Mwezi wa tatu huu sasa tangia nipate haki yangu ya ndoa, tena mara ya mwisho wala sikufika, nguvu zake zinazidi kupungua na kisukari nacho kinazidi kumkondesha"
Alisema kisha akachukuwa chupa na kumimina bia kwenye glasi yake.
Mume wa Marry alipata maradhi ya kisukari kiasi ya kumsababishia upungufu wa nguvu za kiume, kukawa na mgogoro sana kwenye ndoa yake, bado anaendelea na dawa za kila siku huku akihudhuria kliniki.
"Leo nimezidiwa, ndio maana nimekuja ili unisaidie, maana hata wewe wajuwa kuwa mimi si malaya na sipendi kuanzisha uhusiano na mwanamume mwingine bora wewe ulinisaidia siku ile basi nakuomba na leo tafadhali nimezidiwa"
Alisema huku akilegeza macho kwa ulevi na nye*ge.
"Marry Hapana, si tulikubaliana kuwa ni mara moja tu siku ile na nilikutimizia!!, mie nimebadilika siku hizi, siyo kito*mbi kama zamani, nilifikiri umekuja na jambo muhimu la kikazi kumbe...."
Akanikatisha
"Tafadhali Boss, hebu angalia..."
Akajipekenyua na kuingiza vidole viwili, kisha akatoa ulendaulenda (ule ute transparent mzito unaoteleza na usiokatika haraka)
Macho hayana pazia, kitumbua nikakiona kilivyotuna, mashavu ya papuchi yaleee, amenyoa fresh, lakini huu ute si yupo heat period huyu! Nikiwaza kimya kimya faster.
"Ona nilivyo" alinionesha tena baada ya kuingiza vidole tena.
Moyoni nikawa na mawazo mkingamo, nina ukame wa karibu wiki tatu, lakini nilitaka nimuwekee Hamida, mara mawazo ya kishetani yakanijia (yani sina shaka hapa ni Shetani kabisa alini-push)
"Aaah, kwanza Hamida ni bikira kama anasema kweli, siku ya kumpata atasumbua sana ninaweza kujichafua hata kabla sijamuingilia na hamu ikapungua, ngoja nizipunguze kwa huyu..."
Niliwaza haraka haraka kisha nikamuuliza...
"Wewe si upo danger period?"
"Ndiyo, lakini ninatumia majivu tangu juzi na pia nitameza pills just incase" alijibu kwa kujihamini.
"Okay, basi nenda kaoge"
Nilisema huku nikiinuka na kuzitoa chupa za bia na glasi pale mezani na kuzipeleka jikoni.
Nyumba ina vyumba viwili vikubwa, vyote havina vyoo vya ndani, lakini bafu na choo pia vipo ndani kama unaelekea nje kwa mlango wa nyuma.
Aliingia chumba kingine (tulichokitumia mara ya mwisho) kwa ajili ya kubadilisha nguo aende kuoga.
**
=
Saa moja na nusu jioni nilikuwa tayari niko safi na fresh kutoka. Nilimsindikiza Marry hadi kwao Mabibo (mabwawa 7, siku hizi wanapaita 'beach' ama maji machafu), kisha nikarudi moja kwa moja hadi kwa mzee Burhani.
Nikapaki gari nje, nikabisha hodi.
"Nimeleta dumu hili" nilimuambia Hamida huku nikimpatia dumu pamoja na ile memo kama ambavyo tumekuwa tukipeana. Kisha nikamuaga na kumwambia awasalimie ndani maana nina haraka kuna sehemu naenda.
Huyoo nikatoka hadi Moroco, kisha nikachukuwa njia ya kwenda mjini (Ali Hassan Mwinyi rd), vuuuu hadi ikafika 60kph, nikapita taa za kuongozea mahari za Namanga nikiwa 80kph, vuuuuuu hadi taa za Ohio/Bibi titi nikiwa nimebalansi 80kph, vuuuu hadi taa za Nkruma / Lumumba, bado nipo 80kph, vuuuu hadi taa za Tazara, 80kph bado, vuuuu hadi Airport. Nikazunguka kugeuza (ilikuwa terminal one wakati huo) na kurudi kwa mtindo ule ule...
Kuna rafiki yangu wa kisingasinga aliwahi kuniambia kuwa hizi taa kutokea airpot hadi Moroco kama ukipita kwa spidi ya 80kph, utapita taa zote zikiwa kijani kama taa za awali ulipita kwa spidi hiyo...
Niliwahi kujaribu kwa batavuz lakini sikufanikisha kwa sababu ya uwezo wake, hivyo siku hiyo nilipata fursa ya kujaribu na nili-prove kuwa ni kweli.
Nilirudi hadi nyumbani na kupumzika. Sikwenda kuangalia sinema, nilitaka kupumzika baada ya kumsaidia Marry ipasavyo.
***
=
"Tafadhali, fanya ufanyavyo kesho asubuhi uje tumalizie mazungumzo yetu, muhimu sana, usikose"
Hiyo ndiyo nilikuwa memo niliyomuandikia Hamida na kumpatia kabla sijaenda kufanya fujo barabarani kuelekea airport.
Nilipumzika chumbani huku nikiwaza, je Hamida atafanikiwa kuja? Kama akija nimshauri nini au nimuambie nini?
Nikawa nawaza weee mara taa ya idea mpya ikawaka [emoji362]
Roho ikatulia nikaanza kutafuta usingizi. Zile pilsner nne zilizobakia nilimpatia Marry. Kwenye kabati nilibakiwa na chupa tatu ya brand.
******
Baada ya kutoka kumsindikiza Hamida kwa shangazi yake Jumpili iliyopita, Jumatatu nilihudhuria kipindi kwa mzee Burhani kama kawaida.
Mwalimu maalum bado alikuwa hajapatikana hivyo Hamida aliendelea kunifundisha.
Alianza kunifundisha kusoma baadhi ya 'sura' katika juzuu ili nizitumie katika ibada ya swala.
Niliipenda sana 'suratil fatha', maana niliona kama inafanana na sala ya Baba yetu uliye Mbinguni...
Aliniambia kuwa suratil fatha (maarufu kama alhamdu) ni sura ya ufunguzi katika Qur'an. Ndiyo sura ya mwanzo kabisa katika msahafu. Ikisomwa mara moja kwa dhati kabisa inakuwa na uzito kuliko sura nyingine zote zilizobakia kwa pamoja. Ni sura ambayo ibada ya swala haikamiliki bila kusomwa, hivyo alinisistizia sana niijuwe kwa kuihifadhi moyoni (kukariri)
Siku hiyo Jumatatu alianza kwa kunikaririsha aya nne za mwazo. Nilizihifadhi haraka tu, akanikazania nizurudie rudie akiwa ameniacha peke yangu...
Kwakuwa mashuleni na vyuoni tulishazoea ‘kumeza’ maandishi, haikuwa tabu kwangu kumeza sura ile kwa siku ile moja kwa saa chache nilizo kaa pale...
Ila nilikuwa nafanya ujanja, nasoma aya nne za mwanzo kwa sauti kisha zilizofuata nasoma kimya kimya.
Aliporudi alitaka anisikilize kama nimehifadhi zile aya nne.
Nikazisoma, akafurahi.
Kumbuka katika kukaa, yeye anakaa kulia kwangu halafu kwa nyuma kidogo, hivyo nilikuwa simfaidi sana. Na hata mie wakati huo sikuwa mwenye papara ya kuonesha ubazazi. Nilikuwa mwanfunzi mtulivu kwelikweli.
"Iyaaka na'abudu wa iyaaka na stai'n" alianza kusoma aya ya tano na kunitaka niisome.
"Maana yake nini" nilimuuliza
"Ni wewe tunakuabudu na ni wewe tunakuomba msaada" alijibu kisha akasisitiza nihifadhi kwanza kwakuwa mzee Burhani alisema kwa kuwa naendelea vizuri ataniletea msahafu wa tafsiri ya Kiswahili cha Sheikh Abdullah Saleh Farsi.
Nikaanza kusoma aya ya tano hadi mwisho!
Akashangaa sana, nikamwambia nimeshahifadhi. Akafurahi kisha akaniambia nisome kuanzia mwanzo hadi mwisho, nikaanza kusoma na akawa yeye anasoma kwa tafsiri yake:-
1. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, mwenye kurehemu,
2. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa viumbe vyote,
3. Mwingi wa Rehema, mwenye kurehemu,
4. Mwenye kumiliki siku ya malipo,
5. Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada,
6. Tuongoze njia iliyo nyooka,
7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio ghadhibikiwa (waliopotea)
Amin.
***
Alinifundisha hivyo japo tafsiri sikuhifadhi yote siku hiyo. Katika kukaa naye sikugusia habari za kwa aunt yake hata kidogo.
***
Siku ya Jumanne niliendelea na masomo, nikafanikiwa kuhifadhi tafsiri ya surat'l fatha.
Taarifa zikamfikia mzee Burhani, Jumatano baba yake Hamida aliniletea msahafu wa kijani wenye kiarabu na tafsiri ya kiswahili, nilifurahi sana na bila shaka mzee Burhani alikuwa anafurahia maendeleo yangu.
Siku hiyo Hamida alianza kunifundisha sura tatu za mwisho katika Qur'an tukufu, yaani surat'l Ikhlaas, surat'l Falaq na surat' Nnaas. (Sura ya 112, Sura ya 113 na Sura ya 114). Hivyo Qur’an ina Sura 114 tu.
Hadi kufikia alhamisi tayari nilikuwa nimeshaweza kuzisoma na kuzihifadhi, ila tafsiri nikawa najisomea nyumbani, kisha kupata ufafanuzi kwa Hamida.
***
Asubuhi niliamka mapema sana na kuanza kufanya usafi wa mazingira nje, kisha ndani, hadi kufikia saa mbili asubuhi nilikuwa tayari kwenda kuoga.
Mara ghafla mawazo ya jinsi nilivyo mtekelezea haja yake Marry yakanijia...
Hakika ilikuwa 'show ya kibabe' maana nilipiga mashine hadi alisema tayari nimeshamtoa ny*ege zote. Kwa kuwa sikuwa na mzuka naye sana, wazungu walikuwa wanachelewa kuja, jambo ambalo kwa upande wake ilikuwa faida na kumfanya 'afike' mara kadhaa. Bao zangu mbili tu zilimtosha.
Mara mawazo ya ujio wa Hamida yakaja, nikachukuwa mafuta ya kupikia (supa-ghee), nikaandaa mayai, nikaandaa vitunguu, pilipili mboga, chumvi, pilipili zile ndefu za kijani pia, carot, bila kusahau chupa ya cognac.
Katika ile memo niliyompajia jana, sikutaja muda wa yeye kuja maana sikujuwa mchakato wa kupata ruhusa ungekuwaje.
Kwangu hakuwahi kufika, lakini katika mazungumzo ya kila siku niliwahi kumuelekeza, na sasa ataona alama ya gari yangu nje na pia akiulizia kwa majirani ataelekezwa.
Nafasi yangu RTC ilinifanya nijulikane na watu wengi japo mie wengine sikuwafahamu.
Nikatoka kwa miguu kwenda duka la ushirika la jirani na kununua mkate wa siha. Tanbond na zesta red-palm jam zilikuwepo nyumbani.
Niliharakisha ili niwahi isije ikatokea Hamida amefika mie sipo.
Saa tatu na nusu bado bila bila, sioni dalili ya Hamida. Nikataka nikoroge simu nipige nyumbani kwao lakini roho ikasita. Nikajipa moyo kwamba atakuja tu kama ana nia kweli ya ushauri wangu, Jamaal mwenye busara [emoji4] nilijisemea na kutabasamu.
Saa nne asubuhi njaa ikaanza kuniuma, nikaanza kutengeneza chai. Majani ya chai ya wakati ule yalikuwa mazuri sana, Green-Lebel, chai ilivyokuwa tayari niliiweka kwenye chupa ya chai (thermos) iliyosalia kwenye surufia nilimimina kwenye kikombe, nikaweka maziwa (B&B condensed milk) kisha nikaanza kupooza njaa.
Awali nilikuwa nataka akija tunywe wote chai, kama akija mchana tule wote ili mradi wakati wa maongezi tuwe tunakula.
Nilivyomaliza kunywa chai, tano kasoro hiyo, si Simba wala Yanga, nikaenda kwenye meza ya music system, nikaangalia angalia santuri kisha nikachukuwa santuri mbili, moja ya Kenny Roggers na nyingine ya Bob Marley.
Nikaiweka ya Bob, Legend Colletion, ya Kenny ilikuwa nimeinasisha kwa juu (standby), Bob akaanza kuimba taratiiibu huku mie moyo kila mara unanilipuka kwa kuhisi Hamida anakuja...
Nyimbo zile za Bob na chai niliyokunywa zikanifanya nisinzie...
***
"Ngongongo" nilisikia sauti ya mlango ukigongwa
"Karibu" Nilijibu kwa sauti nzito ya kuzinduka usingizini
Nikainuka na kwenda kufungua mlango
"Karibu Hamida" nimwambia.
"Ahsante" alijibu huku akivua sandals zake na kuingia. Mie nikazichukuwa na kuziingiza ndani nikaziweka kwenye ‘rack’ ya viatu.
"Karibu uketi" nilisema huku nimwonesha kochi lililo kaa angle nzuri.
"Karibu sana Hamida, hapa ndiyo nyumbani." Nilimwambia kwa kujiamini, na kweli palikuwa pametulia, yaani pameenea kasoro mke tu, na leo ndio namuona huyu hapa kwangu japo hajui chochote kuhusu mimi kumtaka kimapenzi sembuse kumposa na kumuoa.
Mkononi alikuwa ameshika kikapu kidogo, ndani yake ameweka pochi yake kubwa ya rangi sawa na gauni, amevaa gauni la light blue, ushungi wake wa kadri mweupe, ananukia vizuri ili mradi kila sifa ya mwanamke mrembo naiona kwake. (Kupenda buana!)
"Kumbe unapenda nyimbo za Bob Marley" alisema.
Wakati huo wimbo uitwao "stir it up" ulikuwa ukiimba (ukicheza)
"Yes, mie napenda miziki, hasa yenye jumbe nzuri, Bob nyimbo zake zina maana na hisia kali sana.
***
Hakika wimbo huo ulicheza muda muafaka, maana lyrics zake ni mahaba tosha, hebu angalia:-
Stir it up, little darlin', stir it up.
Come on, baby
Come on and stir it up, little darlin', stir it up. O-oh!
It's been a long, long time, yeah! (Stir it, stir it, stir it together)
Since I've got you on my mind (oh-oh-oh-oh) Oh-oh!
Now you are here (stir it, stir it, stir it together), I said,
It's so clear
To see what we could do, baby, (oh-oh-oh-oh)
Just me and you
Come on and stir it up, little darlin'!
Stir it up, come on, baby!
Come on and stir it up, yeah!
Little darlin', stir it up! O-oh!
I'll push the wood (stir it, stir it, stir it together)
Then I blaze ya fire
Then I'll satisfy your heart's desire. (Oh-oh-oh-oh)
Said, I stir it together (stir it, stir it, stir it together)
Every minute
All you got to do, baby, (oh-oh-oh-oh)
Is keep it in, and oh…
********
*******
=
Wakati huo wimbo ndio ulikuwa unaishia...
"Ngoja ni rewind uusikilize vizuri" nilisema huku tayari nimesha nyanyuka na kurudisha nyuma kidogo ukaanza upya kuimba [emoji443]
"Eee ngoja nikuandalie chochote jikoni..."
Nilisema,
"Hapana mie nimeshakula nyumbani" alijibu kwa kunikatisha
"Hapana, umekula kwenu, ngoja nikioneshe nami ukarimu wangu" nikaingika jikoni.
Nilikiwa na jiko la umeme (TANALEC) sahani mbili (two plates), nikawasha, na kuweka kikaangio (kikaago) kipate moto, nikaweka mafuta (supa-ghee) yakaanza kuyeyuka, kisha nikaweka vitunguu kiasi, nikawa napiga (koroga) mayai matano, vitunguu vilipokuwa brown kidogo nikaweka kwenye kikaangio mchanganyiko wa mayai, chumvi kiasi, vitunguu vingine, carot, pilipili ndefu na hoho...
Kabla ya kuiva nikaongeza drops kadhaa za brand, kisha nikakunja (half circle) na kukandamiza na kijiko cha kukaangia...
Nikageuza kisha nikakandamiza tena ikiwa vivyo hivyo nusu duara.
Nilisubiri ikaiva vizuri nikaipua na kuiweka katika sahani flat ya udongo, nikapeleka alipo Hamida.
Nikaleta thermos yenye chai, na vikombe viwili, asali, sukari jam, maziwa ya kopo (ya maji mazito) pamoja na tanbond. Kisha nikaleta sles sita za mkate wa siha.
Hamida ametulia tu.
"Karibu Hamida " nilisema huku nikimpatia maji ya kunawa. Akanawa bila kusema kitu.
Nikamuuliza unapenda chai ya rangi au ya maziwa, akajibu ya maziwa, nikamuwekea kwa kikombe chake maziwa kidogo (kiduchu), kisha nikamimina chai, na kumuambia, onja sukari maana hayo maziwa yana sukari, kisha nikamwambia ukitaka asali hiyo hapo na sukari hiyo hapo.
Mie nikawa napaka jam na tanbond kwenye slesi za mikate, nilipaka slesi nne tu, mbili jam na mbili tanbond kisha nikazigawa nusu (mshazali) na kuwa vipande vinne viwili vilivyoshikana kwa kila mtu.
Nami nikakoroga chai ya rangi tukaanza kunywa.
"Kumbe nawe ni mpishi mzuri hivi!?" Alisema alipoonja sehemu ya yai...
"Halafu yana ladha nzuri, umeweka nini humu?" Aliuliza huku akiongeza kipande kingine kikubwa.
"Nimeweka libwata la kukufanya kila jumamosi na jumapili uje kunywa chai hapa, hahahaha" nilijibu kwa kutania na kukwepa swali lake la msingi.
Tuliendelea kunywa na maongezi ya hapa na pale, mziki ulikuwa unaendelea kuimba na safari hii santuri ilianguka ile ya Kenny Roggers... Wimbo "Lady"
******
*******
"Lady"
Lady, I'm your knight in shining armor and I love you
You have made me what I am and I am yours
My love, there's so many ways I want to say I love you
Let me hold you in my arms forever more
You have gone and made me such a fool
I'm so lost in your love
And oh, we belong together
Won't you believe in my song
Lady, for so many years I thought I'd never find you
You have come into my life and made me whole
Forever let me wake to see you each and every morning
Let me hear you whisper softly in my ear
In my eyes I see no one else but you
There's no other love like our love
And yes, oh yes, I'll always want you near me
I've waited for you for so long
Lady, your love's the only love I need
And beside me is where I want you to be
'Cause, my love, there's something I want you to know
You're the love of my life, you're my lady
**********
Tuliendelea kunywa chai pale huku akisifia ladha ya mayai... Moyoni najisema angejuwa nilichoweka wala asingekula... Lakini nikakumbuka naye ni mpishi aliyesomea bila shaka anajuwa lakini asichojuwa ni pombe gani niliyoweka... Niliwaza tu...
Tulivyomaliza, nikainuka nikawa naanza kutoa vyombo, naye akasimama akanisaidia kupeleka jikoni, alitaka kuviosha lakini nilimkataza, moyoni niliona muda unapotea... Pia aliiona chupa ya pombe kali kule jikoni ikiwa imetumika kiasi.
"Enhee, nyumbani umeagaje?" Nilimuuliza baada ya kuwa tumerudi na kukaa kwenye makochi yanayo angaliana huku tukitenganishwa na cofee table.
"Nimeaga kuwa naenda kwa aunt Msasani, na nimewaambia nitarudi kesho" alisita kisha akaendelea...
"Wiki hii yote nimekuwa na kisirani tangia walivyoanza kunilazimisha nikubali posa, hivyo hawakuwa wagumu kuniruhusu na wanajuwa kuwa aunt ananipenda" Alisema
Nikamuuliza kuhusu siku ile Shangazi yake alisemaje, akanijibu kuwa yupo upande wake kwa maana ameniambia nifuate moyo wangu kwa kuwa mimi ni mtu mzima sasa, ningekuwa chini ya miaka 18 sawa, lakini nimepevuka na ninaweza kuona napenda nini na nini sipendi. Alimalizia hivyo.
Nikamwambia basi nitakupeleka kwa aunt yako baada ya chakula cha mchana, hapo ni mida ya saa sita kasoro hivi.
Ndani nina mchele, nina samaki wa kopo kwenye friji (saladin), viungo vingine vyote vipo kasoro mboga za majani tu. Hivyo sikuwa na waaiwasi wa kupoteza muda kutafuta vya kupika.
"Enhe, ulisema nije kupata ushauri ulioufanyia kazi, ndio nausubiri" alisema na kukaa vizuri kwenye kochi.
"Mbona leo tuna muda mrefu, nitakuambia tu usijali, pia usafiri tunao, utachaguwa batavuzi ama pijo" nilimjibu kibaharia..
Nikasimama nikachukuwa photo albam iliyokuwepo kwenye 'shelfu' la vitabu nikampatia.
Akaanza kupekuwa huku akiuliza hapa ni wapi, hapa ni wapi...
Baada ya hapa ni wapi ya tatu nikasimama na kuhamia upande wake nikakaa kwenye mbao ya juu ya kochi nikawa namjibu vizuri, na hata bila kuuliza nikawa natoa maelezo ya kutosha, akawa anafurahia sana nchi ya Uingereza ilivyo...
"Na huyu nani? Aliuliza alipomwona Sue binti wa Hispania.
" Aaa huyo alikuwa mate wangu chuoni, actually alikuwa girl friend wangu..." Nikameza mate kisha nikaendelea...
"Tulishaachana miaka zaidi ya miaka miwili iliyopita..." Nilisema huku yeye bado akikodolea picha nyingine za huyo binti Paterson.
Kukawa na ukimya fulani hivi, muziki ulikuwa tayari umesimama, mara akasema, nioneshe msalani.
Nikatangulia nikamuonesha...
Nikamuacha humo mie nikarudi na kuwaza nianzeje.
Plani ya awali ilikuwa nimleweshe akichangamka nitumie faida hiyo kumteka kimapenzi, lakini akili ikawa inakataa, badala yake inaniambia nimtongoze akiwa yupo fresh bila pombe, naanzaje sasa! Mara [emoji362][emoji362][emoji362]
***
Aliporudi kutoka maliwatoni, akaketi nami nikawa upande wa wangu...
Nikajikuta nimesimama na kuzunguka meza na kukaa juu ya meza ile ndogo (cofee table) nikiangaliana naye uso kwa uso, magoti yanakaribia kugusana.
Yeye akachukuwa albam akawa anaendelea kupekua...
"What is love?!" Nilimuuliza huku nikimtazama usoni!
Kabla hajajibu nikampachika swali la pili
"Do you believe in love?!"
Nikamuona amekaa kimya! Akameza mate kisha akajibu kwa ufupi...
"Yes, I do believe in love, and love is tender feelings"
Baharia nikaona mwanzo huooooo! Nashangilia kimoyo moyo.
Nilikuwa naweza kumlazimisha na kumbaka, lakini sina tabia hizo, huwa napata mzuka pale mwanamke anaporidhia mwenyewe lakini hata kama anasema hapana (hapana ila ya mdomoni)
Nikaamua nimuanzie mbali, na wala sikuwa na wazo la kuunganisha naye vikojoleo siku hiyo, nilikuwa na malengo naye ya mbali, sikutaka ani-discredit hata kidogo...
"Hebu niambie, dini inasemaje kuhusu kuchaguwa mchumba" nilipachika swali lingine
"Imehimizwa kuangalia mambo muhimu kama nasaba (koo/ukoo), uchumi, tabia njema, maumbile na dini, lakini papohapo imesisitizwa kuangalia dini zaidi kwani kuna faida ya kupata mengine yote Allah akitaka. Hivyo muolewaji akiendewa na muoaji kama amempenda basi aangalie mambo mawili tu, yaani tabia njema na awe mwislamu"
Akasita kidogo kama kajistukia hivi kisha akaendelea...
"Na muoaji akimpenda mwanamke basi azingatie dini yake tu kwa maana mengine yanaweza kuondoka wakati wowote isipokiwa kama ni mcha Mungu basi atafaulu, na imeruhusiwa kwa muoaji kumuangalia mchumba wake uso na viganja vya mikono..."
Alisema maneno hayo huku akionesha kwa mkono wake sehemu ya uso inayotakiwa kuonekana na kuonesha kwenye kiganja pia.
Nikasema vizuri, nimeelewa, kisha nikmuuliza...
"Sasa huyo mchumba wako wa Omani ana tabia njema? Je ni Muislamu?, Je ameona uso wako na viganja vyako?
" Mchumba wa nani, hebu usiniudhi, siyo mchumba wangu yule...'" Aling'aka
"Sawa, sina maana hiyo, hebu jibu swali..." Nilimkazia macho
"Hapana, hajaniona, labda amepewa picha yangu kupitia kwa da-Sabra ila hanijui wala simjui..."
Baada ya jibu hilo nikamuuliza
"Kwani ili ndoa ikamilike mambo gani lazima yatimie (yatimizwe)?
Alijibu kwa kirefu kwamba...
“Ili ndoa ikamilike lazima mambo haya yawepo:-
1. Idhini ya Walii (Baba mzazi ama msimamizi halali),
2. Kuridhika kwa bibi harusi mtarajiwa,
3. Kutimia kwa tamko la ndoa,
4. Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu,
5. Kubalighe na kuwa na utambuzi baina ya wanandoa’’
“Je wewe umeridhika kuolewa na huyo mu-Oman?”nilimuuliza japo jibu nalijuwa
Akasema
“Hapana, sijaridhika”
Nikamwambia, basi poa moyo, maana hapo hakutokuwa na ndoa, ili ndoa itimie lazima bibi harusi mtarajiwa aridhie.
Nikaona kama amepata nguvu Fulani hivi. Nikawaza kumbe unaweza ukawa daktari wa magonjwa lakini siku ukipatwa na ugonjwa wewe daktari unaweza kusahau hata dawa za kutumia hadi ukumbushwe..
Hamida kiumri nimepishana naye kama miaka minne hivi, hivyo tunaendana sana. Nikamuuliza swali la uchokozi...
”Ulisema bikra yako utamzawadia mtu umpendaye, unaonaje ukinizawadia mimi?”
Kimyaaa! Akawa anaangalia chini.
”Ulisema pia bikra yako huwezi kuweka rehani kwa mbabu, mie si mbabu, mie ni kijana mwenzio...”
Kimyaaaa huku anachezesha vidole vya miguuni.
”Pia ulisema kuwa bikra yako utampa mumeo mtarajiwa, mie pia nafaa kuwa mumeo, maana nimesilimu juzi juzi tu, tabia zangu tangia unifahamu wazijuwa, mengine hayo ndiyo ulisema si ya kuzingatia sana lakini uwezo wa kukulisha, kukuvisha, kukupa malazi na jimai ninao”
Hamida yupo kimya tu amejiinamia na sasa vidole vyake vya mikononi navyo vimeanza kusuguana suguana...
Nikamshika mkono wake wa kushoto, kasha wa kulia, tukawa tumeshikana kama tunasalimiana...
“Hamida”nilimuita
“Abee” aliitika kwa sauti ya chini iliyonipa nguvu zaidi ya kushambulia...
“Jamaal anakupenda, Jamaal anakupenda sana. Tangia alipokuona mara ya kwanza hajaacha kukupenda wala kuacha kukuwaza. Jamaal amefanya jithada kubwa ili awe nawe muda wote, Jamaal ameweka uteja kwa kunywa juisi na togwa ili isipite siku bila kukuona, hakika Jamaal anakupenda sana. Jamaal amebadilisha dini kwa ajili yako, ili ukumkibalia akuoe. Jamaal yupo tayari kwa changamoto zote zitakazo jitokeza kwa sababu ya tofauti ya asili zetu. Najuwa kuwa wapo wengi waliojitokeza ama watakaojitokeza kukuposa, lakini sina uhakika kama utawapenda kwa kuwa wengi wanakuwa ni ndugu zenu. Pia tumefundishwa mashuleni kuchanganya nasaba ili kupata vizazi bora.”
Hamida kainama tu, bado nimemshika mikono. Nikamuachia mkono wake wa kushoto na kumshika bega lake la kushoto...
“Tafadhali Hamida nipe nafasi katika moyo wako. Love is tender feelings according to your definition, and I do have those feelings to you, so please accept my request”
Nikamshika mabega yake yote mawili huku yeye akizidi kuinama chini.
Nikasimama, nikamshika makwapani na kumuinua, aliinuka wala sikutumia nguvu, palikuwa kimya bado, hakuna mziki wala kelele zozote, pumzi zetu tu zinasikika...
Nikamkumbatia mikono yangu ikiwa mabegani mwake, nikauchukuwa mkono wangu wa kulia na kuushika wake wa kushoto na kumfanya anishike mgongoni, nikafanya hivyo na mkono wake wa kulia kasha mimi nikashusha mikono yangu hadi kiunoni mwake...
Lo salale! Manguo haya wanayovaa waislamu wa kike yanaficha mengi, mikono yangu iligunduwa kuwa Hamida ana mat*ako na hips balaa!
Tuliendelea kukumbatiana kwa sekunde kadhaa, mara shetani akanikumbusha kuwa akili zitamrudia Hamida, mpeleke chumbani...
Nikamwita, Hamida! Akatitia abee! Kwa sauti ile ya kuonesha hana ujanja tena, nikamwambia, twende huku, wala hata hakuuliza, nikamkokota hadi chumbani kwangu (siyo kule kwa jana na Marry)
Moja kwa moja hadi kitandani, shuka jeupe safi, nikawa nimesimama mbele yake yeye akekaa kitandani, nikamwita tena...
“Hamida”
Akaitikia
“mmh, abee!”kwa sauti ya mahaba sasa
Nikamwambia simama huku namuinua, akasimama, nikaanza kumbusu kwenye paji la uso, lisha puani, kisha kwenye lips (just short kisses), kisha shingoni, akahema sana..., nakarudia mdomoni sasa ni ile frech kiss, taratiiibu na kuongeza kasi kadri tulivyokuwa tunaendelea, mikono yangu ndio ikawa haitulii kabisa, nikaanza kutalii mgongoni, kiunoni hadi mat*akoni, nikafika kifuanim Hamida naye akaanza kutoa ushirikiano... nikaacha kumkiss mdomoni, nikahamia shingoni maana nilipagundua kuwa ndipo nywila ilipo, alianza kuguna miguno ya ajabu ajabu...
Itaendelea...View attachment 1347835View attachment 1347836View attachment 1347838View attachment 1347839
James Jason
Sent using Jamii Forums mobile app